Dkt. Mwigulu: Kiswahili kitumike katika usaili wa Watumishi Serikalini

Dkt. Mwigulu: Kiswahili kitumike katika usaili wa Watumishi Serikalini

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Kiswahili ndio lugha yetu inatambulika SADC na Umoja wa Afrika. Wazri wa fedha ahoji sababu ya kufanya usaili wa watumishi wa serikali kwa lugha ya kiingereza na kushindwa kukipa nguvu Kiswahili.

Ameshauri kishwahili kitumike katika usaili
 
Kuna kitu amekisema kina ukakasi mbaya sana: kusamehe kodi kwa nyasi bandia kwa viwanja vya michezo/mpira kadhaa kama Arusha, Mwanza, Mbeya n.k. Maana yake ni kwamba ccm inaweka nyasi bandia viwanja vyake bila kulipia kodi.
 
Imekaa vibaya,tuseme umesomea HR management au engineering,utaulizwa Nini Sasa kwa kiswahili ? Mimi binafsi ukiniuliza maswali kwa kiswahili vitu vingi sijui
Mimi naweza kusema nafahamu kiingereza vizuri kuliko kiswahili
Hii imekaa vizuri wengi wanashindwa kufanya interview sababu ya mkinzano na ujuzi mdogo wa kmanagea
 
Kiswahili ndio lugha yetu inatambulika SADC na Umoja wa Afrika. Wazri wa fedha ahoji sababu ya kufanya usaili wa watumishi wa serikali kwa lugha ya kiingereza na kushindwa kukipa nguvu Kiswahili.

Ameshauri kishwahili kitumike katika usaili
Kusoma unasoma kwa kizungu. Interviews kwa kiswahili
 
Imekaa vibaya,tuseme umesomea HR manage management au engineering,utaulizwa Nini Sasa kwa kiswahili ? Mimi binafsi ukiniuliza maswali kwa kiswahili vitu vingi sijui
Mimi naweza kusema nafahamu kiingereza vizuri kuliko kiswahili

Unaulizwa ujuzi wako na mambo uliyofanya katika kipindi chako cha kazi. Sasa ukishindwa wewe kwa kiswahili ni sawa, wengine hawawezi kushindwa. Kama wewe ulivyokua unawashinda kwa kiingereza
 
Siwezi kusoma miaka 10 kumi kwa kingereza . Miaka minne O'level na miaka sita on my professional alafu mtu ani-intreview kwa Kiswahili, kwanza vitu nilivyosomea kwa kingereza hata kivichange kwa Kiswahili inakuwa ngumu yaan zile (terminologies) Sasa inakuwaje Kiswahili tena.

Leta ung'eng'e huohuo tutapambana tu.. kama ipo ipo tu.

I would be nimesoma taaluma yangu kwa Kiswahili hapo sawa, So kama wanataka hv basi na mavyuoni watumie kiswahili
 
Kuna kitu amekisema kina ukakasi mbaya sana: kusamehe kodi kwa nyasi bandia kwa viwanja vya michezo/mpira kadhaa kama Arusha, Mwanza, Mbeya n.k. Maana yake ni kwamba ccm inaweka nyasi bandia viwanja vyake bila kulipia kodi.
CCM haina timu bwashee.
 
Siwezi kusoma miaka 10 kumi kwa kingereza . Miaka minne O'level na miaka sita on my professional alafu mtu ani-intreview kwa Kiswahili,…….
Leta ung'eng'e huohuo tutapambana tu.. kama ipo ipo tu.
I would nimesoma taaluma yangu kwa Kiswahili hapo sawa, So kama wanataka hv basi na mavyuoni watumie kiswahili
Hiki ndo Kingereza unachovimbia.!!
 
Kusoma unasoma kwa kizungu. Interviews kwa kiswahili

Huu nao mtihani sasa maneno mengine kutafsiri sijui itakuwaje, Watanzania tusiogope lugha za kigeni tujifunze, hii ya Kiswahili ingekuwa kwa wale wanaoletewa interview za Kiswahili ila huku juu lugha iendelee au waruhusiwe kuchanganya lugha.
 
Siwezi kusoma miaka 10 kumi kwa kingereza . Miaka minne O'level na miaka sita on my professional alafu mtu ani-intreview kwa Kiswahili,...
Ina maana mtu akikuuliza utakayofanya juu ya au kuhusiana na taaluma yako utashindwa kumwelezea kweli? Yaani utashindwa kujieleza kuwa nafanya au nitafanya hivi na vile? Labda umekariri tu na hujui unachokifanya au utakachofanya sambamba na taaluma yako.
 
Huu nao mtihani sasa maneno mengine kutafsiri sijui itakuwaje, Watanzania tusiogope lugha za kigeni tujifunze, hii ya Kiswahili ingekuwa kwa wale wanaoletewa interview za Kiswahili ila huku juu lugha iendelee au waruhusiwe kuchanganya lugha.
Anayejuwa taaluma yake hashindwi kueleza afanyacho.

Kwani umeambiwa ueleze terminologies kwa kiswahili? Hata instructions hujapewa unaanza kutengeneza mashaka.
 
Back
Top Bottom