Dkt. Mwigulu: Kiswahili kitumike katika usaili wa Watumishi Serikalini

Dkt. Mwigulu: Kiswahili kitumike katika usaili wa Watumishi Serikalini

Kuwe na option kwenye interview mtu achague lugha anayotaka kujieleza
Uko sahihi

Sababu nchi bado ina mifumo miwili ya swahili medium schools na English medium.schools Mtu achague interview ahojiwe kwa Lugha ipi.Ila kwa level ya digrii sidhani kama mtu atakubali interview ahojiwe kwa kiswahili.Atapata shida ya kufa mtu kutafuta maneno ya kiswahili

Fikiria umesoma electrical engineering

Halafu upigwe maswali ya kiswahili.Kwanza waandaaji maswali wenyewe ya kiswahili utawatoa wapi sababu wao wenyewe wamesoma kwa kiingereza hiyo fani

Ni.kupotezeana muda tu
 
Hii imekaa vizuri wengi wanashindwa kufanya interview sababu ya mkinzano na ujuzi mdogo wa kingereza
Labda kitumike kwa masomo ya arts yaliyojaa porojo

Daktari au engineer useme umfanyie interview kwa Lugha ya kiswahili hawezi kukubali
 
Imekaa vibaya,tuseme umesomea HR management au engineering,utaulizwa Nini Sasa kwa kiswahili ? Mimi binafsi ukiniuliza maswali kwa kiswahili vitu vingi sijui
Mimi naweza kusema nafahamu kiingereza vizuri kuliko kiswahili
Yaani bado tunaendelea kuonuesha ujinga wetu. Wee lugha ya malkia ndio ilishatawala. Tusiumizane vichwa tujadili vitu vya msingi na sio trivial matters
 
Uko sahihi

Sababu nchi bado ina mifumo miwili ya swahili medium schools na English medium.schools Mtu achague interview ahojiwe kwa Lugha ipi.Ila kwa level ya digrii sidhani kama mtu atakubali interview ahojiwe kwa kiswahili.Atapata shida ya kufa mtu kutafuta maneno ya kiswahili

Fikiria umesoma electrical engineering

Halafu upigwe maswali ya kiswahili.Kwanza waandaaji maswali wenyewe ya kiswahili utawatoa wapi sababu wao wenyewe wamesoma kwa kiingereza hiyo fani

Ni.kupotezeana muda tu
NImehudhuria interview kama 3 hivi kuwafanyia usaili watu wanapewa option hata kama una PhD unachagua lugha mwenyewe hiyo kwa kweli niliipenda sn hata ukichagua kiswahili huzuiwi kufafanua kwa kiingereza inakuwa Swahili-English
 
Imekaa vibaya,tuseme umesomea HR management au engineering,utaulizwa Nini Sasa kwa kiswahili ? Mimi binafsi ukiniuliza maswali kwa kiswahili vitu vingi sijui
Mimi naweza kusema nafahamu kiingereza vizuri kuliko kiswahili
Sio Kila Kazi zitasailiwa kwa kiswahili..Uliona mifano aliyoitoa?
 
Labda kitumike kwa masomo ya arts yaliyojaa porojo

Daktari au engineer useme umfanyie interview kwa Lugha ya kiswahili hawezi kukubali
Bora mimi nisailiwe kwa kiswahili hiyo hiyo engineering kwa sababu kila mtambo una jina lake
 
iwe kwa kiswanglish, hiki watanzania wengi tunakijua...

Elimu toka msingi mpaka chuo kikuu iwe kwa Kienglisn hapo itakuwa sawa....
Bila shaka usaili ni kwa kiswahili ila itatoa options ya matumizi ya lugha hasa kwenye oral au mahojiano..

Written inawezekana kulingana na maswali au written ifanyike kwa English..
 
Nchi hii kuna shida mahali

Rwanda imejipanga kuwa na high quality manpower in Africa Inasisitiza na ku sponsor kila mwenye fani ahakikishe anapata International certification ya fani yake ili kuuzika soko la kimataifa la ajira

Sisi tunataka swahili certified professionals!!! Na interview iwe kiswahili .Anyway ruksa Serikali kujaza waswahili kwenye ajira zake waliojaa uswahili swahili .Wakienda conference za kimataifa badala ya kuhutubia kuhusu water wataita water " mma"
 
Imekaa vibaya,tuseme umesomea HR management au engineering,utaulizwa Nini Sasa kwa kiswahili ? Mimi binafsi ukiniuliza maswali kwa kiswahili vitu vingi sijui
Mimi naweza kusema nafahamu kiingereza vizuri kuliko kiswahili
Watu wanafikiri wanakosa ajira kwasababu ya lugha ajira hakuna pia kiswahili ni kigumu sana kuliko kingereza
 
Fafanua kidogo, unamaanisha uelewa wa hizo fani hauna maneno ya kiswahili? Maana kwenye usaili tunataka kujua ni nini unachokijua kuhusu kazi unayoiomba, sasa ukisema unaweza kuyasema hayo kwa lugha moja, ina maana umekariri au???? Au ni wapi sijakuelewa.

JESUS IS LORD
 
Watu wanafikiri wanakosa ajira kwasababu ya lugha ajira hakuna pia kiswahili ni kigumu sana kuliko kingereza
Hiyo inaitwa Mbaazi akikosa maua husingizia jua

Sidhani hata kabla kuwa Serikali ilikuwa kuajiri mtu kwa kuwa anajua kiingereza!!!
 
Anayejuwa taaluma yake hashindwi kueleza afanyacho.

Kwani umeambiwa ueleze terminologies kwa kiswahili? Hata instructions hujapewa unaanza kutengeneza mashaka.
Shida kubwa ni elimu yetu tunasoma kujibu maswali ya mtihani. Sio kuweka maarifa akilini.

YESU NI BWANA
 
Imekaa vibaya,tuseme umesomea HR management au engineering,utaulizwa Nini Sasa kwa kiswahili ? Mimi binafsi ukiniuliza maswali kwa kiswahili vitu vingi sijui
Mimi naweza kusema nafahamu kiingereza vizuri kuliko kiswahili
Wengi watataka kuhojiwa kiingereza .

Wewe fikiria unaulizwa wewe kama Mkuu wa kitengo cha ajira leo ndio umemwajiri kazi Mkerengeza Mwandamizi.Utampangia majukumu gani huyo Mkerengeza Mwandamizi uliyemajiri ?

Hilo swali lazima ufeli sababu hata humjui huyo anayeitwa Mkerengeza ni mtu wa fani gani
 
Waanze kwanza kubadili lugha ya kujifunzia iwe kiswahili. Chuo ujifunzie English halafu usaili kisw misamiati mingine hata Kwa kiswahili hujui inaitwaje.
 
Basi na sisi mtu anapokwenda kuhojiwa kuhusu kazi ajieleze kiswahili.kama ana uwezo anao tu.
kiingereza kisiwe ndo kigezo Cha KUPATA kazi.
Kuna watoto nawajua kichwani 0.lakini kinachowabeba ni kujua kiingereza na wameajiliwa serikalini
Wewe unayeshindwa kujieleza kwa kiingereza unaonekana 0.
Wanafanya kwa Lugha zao na Vyuo hao kufundisha kwa Lugha zao

Tanzania Vyuo vyetu kiingereza ndio hutumia kufundishia sio.kiswahili
 
Kiswahili ndio lugha yetu inatambulika SADC na Umoja wa Afrika. Wazri wa fedha ahoji sababu ya kufanya usaili wa watumishi wa serikali kwa lugha ya kiingereza na kushindwa kukipa nguvu Kiswahili.

Ameshauri kishwahili kitumike katika usaili
Hiyo ni hotuba ya bajeti au ni hotuba ya Waziri Mkuu, wizara ya elimu au wizara ya utamadumi? Na hao watoto wetu wakishindwa kwenye usaili tutaomba na lugha yetu ya asili iwemo! Waendelewa hiyo huita "competition towards the bottom." Sawa na kupunguza kiwango cha ufaulu ili wanafunzi wengi wafuzu mitihani. Hivi Watanzania tunafikiri kweli!

Sent from my ONEPLUS A5000 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom