Dkt. Mwigulu: Kiswahili kitumike katika usaili wa Watumishi Serikalini

Dkt. Mwigulu: Kiswahili kitumike katika usaili wa Watumishi Serikalini

Hapana, kiingereza kiendelee kutumika kwa usaili wa wasomi wa ngazi ya degree kwenda juu!
... ni njia sahihi kabisa ya kujua kama kuna chochote ndani ya fuvu husika!
Akihojiwa kingereza alichosomea sekondari hadi chuo kikuu huwezi jua kuwa kwenye kichwa ana kitu?

Ujue na anayeendesha interview kasoma Vyuo hivyo hivyo alivyosoma huyo anayemhoji au naye fuvu la kichwa kingereza hakipandi ndio maana anataka a interview kiswahili? Wakutane waswahili watupu Mafuvu matupu ambayo wote kingereza hakipandi kuanzia anaye hoji na anayehojiwa
 
Akihojiwa kingereza alichosomea sekondari hadi chuo kikuu huwezi jua kuwa kwenye kichwa ana kitu?

Ujue na anayeendesha interview kasema Vyuo hivyo hivyo alivyosoma huyo anayemhoji au naye fuvu la kichwa kingereza hakipandi ndio maana anataka a interview kiswahili? Wakutane waswahili watupu Mafuvu matupu ambayo wote kingereza hakipandi kuanzia anaye hoji ns anayehojiwa
Kama huwezi kufanyiwa interview kwa lugha uliyotumia kujifunza maana yake hujaambulia kitu kwenye mafunzo yako!
NB: VIJANA MSIDANGANYWE NA WANASIASA, JIFUNZENI KIINGEREZA, CHA KUONGEA NA KUANDIKA, KWA BIDII!
KIINGEREZA NDIO KISWAHILI CHA DUNIA!
 
Imekaa vibaya,tuseme umesomea HR management au engineering,utaulizwa Nini Sasa kwa kiswahili ? Mimi binafsi ukiniuliza maswali kwa kiswahili vitu vingi sijui
Mimi naweza kusema nafahamu kiingereza vizuri kuliko kiswahili
Hii ni kweli kabisa.
Mimi naona ni ujinga tu. Yaani miaka yote ya kufundishwa kwa kiingereza halafu maswali ya interview ya fani yangu uniulize kwa kiswahili? Nitafeli!
Nafahamu kiingereza vizuri kuliko kiswahili.
 
Imekaa vibaya,tuseme umesomea HR management au engineering,utaulizwa Nini Sasa kwa kiswahili ? Mimi binafsi ukiniuliza maswali kwa kiswahili vitu vingi sijui
Mimi naweza kusema nafahamu kiingereza vizuri kuliko kiswahili

Inaweza kuwa nafuu kwa baadhi ya watu
 
Kama huwezi kufanyiwa interview kwa lugha uliyotumia kujifunza maana yake hujaambulia kitu kwenye mafunzo yako!
NB: VIJANA MSIDANGANYWE NA WANASIASA, JIFUNZENI KIINGEREZA, CHA KUONGEA NA KUANDIKA, KWA BIDII!
KIINGEREZA NDIO KISWAHILI CHA DUNIA!
Mwigulu anajaribu kuwatetea Waandaa interview waliosoma shule za Kayumba sababu wakikutana na vijana waliosoma English medium wanamwaga kingereza ambacho muandaa interview anabaki midomo wazi vocabulary zinawaishia
 
Waziri anayehusika na ajira kaingiliwa eneo lake la utaalamu

Waziri wa fedha aombe radhi hadharani kwa kuingilia wizara ya mwenzie

Kafanya kama Simbachawene akiwa Waziri wa mambo ya ndani aliyeingilia taasisi za dini na kusema kuwa hazilipi kodi wakati yeye sio Waziri wa fedha wala TRA
Mambo ya ajira hayamhusu Waziri wa fedha
 
Ni ujuha wa hali ya juu kufanya usaili kwa kiswahili kwa mambo ya kitaalamu na kiweledi wakati lugha ya kufundishia na masomo kuanzia kidato cha kwanza mpaka chuo kikuu ni kiingereza.
Tunaposema kuna haja ya kuangalia upya lugha ya kufundishia, tunakuwa na maana hii ya kumuwezesha mwanafunzi anapohitimu elimu yake kuwa na uwezo katika nyanja nyingi kama kusailiwa, kuwasiliana, kujieleza,kiutendaji na pia kiufanisi.
Unaulizwa swali kwa kiingereza,unalitafasiri akilini kwa kiswahili na kuchakata, halafu unapata jibu, halafu tena unalileta kwenye kiingereza ndio ujibu!!!
Tuamue moja tu.
Kiswahili tangu darasa la awali mpaka chuo kikuu au kiingereza tangu darasa la awali mpaka chuo kikuu.
 
Kiswahili ndio lugha yetu inatambulika SADC na Umoja wa Afrika. Wazri wa fedha ahoji sababu ya kufanya usaili wa watumishi wa serikali kwa lugha ya kiingereza na kushindwa kukipa nguvu Kiswahili.

Ameshauri kishwahili kitumike katika usaili
Kwani Kiswahili kinahusikaje na Bajeti? Mwigulu amekuwa Waziri wa Utumishi?
 
Imekaa vibaya,tuseme umesomea HR management au engineering,utaulizwa Nini Sasa kwa kiswahili ? Mimi binafsi ukiniuliza maswali kwa kiswahili vitu vingi sijui
Mimi naweza kusema nafahamu kiingereza vizuri kuliko kiswahili
Unaelewa au umekariri?Anayeelewa anaweza shindwa kujieleza kwa lugha mama kama kweli alielewa alichokuwa anasoma?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ina maana mtu akikuuliza utakayofanya juu ya au kuhusiana na taaluma yako utashindwa kumwelezea kweli? Yaani utashindwa kujieleza kuwa nafanya au nitafanya hivi na vile? Labda umekariri tu na hujui unachokifanya au utakachofanya sambamba na taaluma yako.
Interviews ni zaid ya hayo. Hayo maswali uliyouliza ni mepesi sana. Kuna technical terminologies kuhusu taaluma yako. Probably umezisoma hizo terminologies for 4 years.. and umezifanyia kazi 2 to 3 years.. miaka hiyo yote hujawahi fundishwa kiswahili cha hizo terminologies.
Halaf unakutana na interview ya kiswahili?

Sisemi haiwezekani but itakuwa ngumu. Best approach ni kumpa mtu option ya kuchagua lugha or vyuo vikuu elimu iwe ya kiswahili ili mbeleni
 
Unaelewa au umekariri?Anayeelewa anaweza shindwa kujieleza kwa lugha mama kama kweli alielewa alichokuwa anasoma?.

Sent using Jamii Forums mobile app
MNhhh atakuwa anachanganya Kiswahili na terminologies za Taaluma aliyosomea... confusion ya kijinga tu, watu wasome kwa Kingereza na Usahili pia uwe kwa Kingereza.
 
Nia ya waziri mwigulu ni njema tatizo kubwa lipo kwenye utekelezaji haswa kwa watendaji wa Serikali walio pewa dhamana. baadhi yao bado wanakidharau sana kiswahili!!! yaani ukizungumza kizungu au kuandika ndio utaonekana umeelimika na umeiva!!! lkn ukizungumza kizungu kibovu au kuandika utaonekana hujaelimika vizuri na utadharaulika!!! hiii ni dhana potofu sana.
tubadilike.

Mfano kwenye mahakama zetu bado Kizungu ndio kimeshika htamu pamoja na sheria kubadilishwa lkn bado kiswahili hakipewi kipau mbele ktk kutoa Haki za watanzania.

tunahitaji viongozi wenye utashi wa dhati ktk matumizi ya Lugha yetu ya Kiswahili.

Awamu ya 5, ili dhamiria matumizi ya Lugha ya Kiswahili, tunaomba na awamu hii ya 6 ikazie palepale kama ilivyo kuwa imekusudiwa na awamu ya 5.

Lugha yetu na tunu yetu, ni kitambulisho chetu, kamwe tusiipuze.
 
Kiswahili ndio lugha yetu inatambulika SADC na Umoja wa Afrika. Wazri wa fedha ahoji sababu ya kufanya usaili wa watumishi wa serikali kwa lugha ya kiingereza na kushindwa kukipa nguvu Kiswahili.

Ameshauri kishwahili kitumike katika usaili
Acha tuendelee kula mtori......
 
Kusoma unasoma kwa kizungu. Interviews kwa kiswahili
Kama ulisoma kwa kukariri hicho kiingereza na kumeza masomo tu,basi ni wazi hauwezi kujieleza kwa lugha mama ambayo 90% wanaitumia.Na kwa hali hii ndiyo maana nyinyi mnaojulikana kuwa wasomi mmeshindwa kuleta mabadiliko kwa jamii kwa sababu hamuwezi kuifikishia jamii mipango ya maendeleo kwa lugha sahihi na hasa mkizingatia 90% ya wanajamii wanatumia kiswahili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akihojiwa kingereza alichosomea sekondari hadi chuo kikuu huwezi jua kuwa kwenye kichwa ana kitu?

Ujue na anayeendesha interview kasoma Vyuo hivyo hivyo alivyosoma huyo anayemhoji au naye fuvu la kichwa kingereza hakipandi ndio maana anataka a interview kiswahili? Wakutane waswahili watupu Mafuvu matupu ambayo wote kingereza hakipandi kuanzia anaye hoji na anayehojiwa
Lakini haiingii akilini unamfanyia interview kwa kiingereza wakati kazini kwake atatumia kiswahili kitupu muda wote. Kwa mfano mfanyakazi wa halmashauri unamfanyia interview kwa kiingereza wakati kazini kwake atawahudumia waswahili muda wote! Ni ujinga uliopita kiwango. Naona waziri anapointi hapo. Hao wanaoenda kufanyakazi kwenye mashirika yanayotumia kiingereza ni sawa kufanyiwa interview kwa kiingereza. Watz wengi tunasumbuliwa na slavery mentality tunafikiri kujua kiingereza ndio kuwa na maarifa ndio maana wasomi wengi wa kiingereza hawafanikiwi kwenye maisha ya kujiajiri.
 
Back
Top Bottom