Dkt. Mwigulu: Kiswahili kitumike katika usaili wa Watumishi Serikalini

Dkt. Mwigulu: Kiswahili kitumike katika usaili wa Watumishi Serikalini

Kuna kitu amekisema kina ukakasi mbaya sana: kusamehe kodi kwa nyasi bandia kwa viwanja vya michezo/mpira kadhaa kama Arusha, Mwanza, Mbeya n.k. Maana yake ni kwamba ccm inaweka nyasi bandia viwanja vyake bila kulipia kodi.
Watumiaji ni watanzania
 
Lakini haiingii akilini unamfanyia interview kwa kiingereza wakati kazini kwake atatumia kiswahili kitupu muda wote.
What ??
Report unaandika kiswahili?. Ya
kuomba funds au progress report za miradi ya wafadhili? Unataka mkalimani? Miradi fadhiliwa iwe ya halmashauri au Serikali kuu?
 
Sio shule ni kwenye usaili wa kazi.
Sidhani

Shule za msingi wote darasa la saba hupewa mitihani mmoja wa taifa uwe umesoma kwa kiingereza au kiswahili

Wa kiingereza hupewa mitihani kwa kingereza alichosomea na aliyesoma kiswahili hupewa mtihani ule ule

Kaangalie matokeo ya darasa la Saba kitaifa shule ambazo huongoza kitaifa ni shule za msingi za kiingereza
 
Kiswahili ndio lugha yetu inatambulika SADC na Umoja wa Afrika. Wazri wa fedha ahoji sababu ya kufanya usaili wa watumishi wa serikali kwa lugha ya kiingereza na kushindwa kukipa nguvu Kiswahili.

Ameshauri kishwahili kitumike katika usaili
Kwanini wasipendekeze hivyo wenye taaluma za kada husika mpaka iwe kwa wanasiasa kila siku hapa tz, hili nalo ni tatizo kwa maslahi ya taaluma za watu wanao sahiliwa.
 
Kiswahili ndio lugha yetu inatambulika SADC na Umoja wa Afrika. Wazri wa fedha ahoji sababu ya kufanya usaili wa watumishi wa serikali kwa lugha ya kiingereza na kushindwa kukipa nguvu Kiswahili.

Ameshauri kishwahili kitumike katika usaili
Hata kama kinatambulika SADC au AU, bado kiswahili hakifai kwa kufundishia, kuna vitu vingi vinakosekana kwenye lugha ya kiswahili....maneno mengi ya science. Ebu acheni siasa, watoto wenu mnawafunza English, wetu wakajifunze Kiswahili? Huu ni ujinga mkubwa, kwani tukitumia English kuanzia darasa la kwanza tatizo lipo wapi? Pia kujua lugha zaidi ya moja ni kosa? Kuna rafiki anajua lugha tano...na huko kwenye kazi anapeta ile mbaya, yaani English ipo juu, French, Kiswahili, Kinyarwanda, Luganda na Espanol. Mbona hajapungukiwa chochote....mbona kuna watu wanaongea lugha zetu za kikabila vizuri, kwanini tushindwe English lugha rahisi, hapo uweze kupata kazi nzuri? Acheni uvivu watanzania.
 
Kama ni suala la usaili, kuwe na option ama mtu achague kiswahili au kiingereza,anayetaka kutiririka kwa kiswahili au kiingereza ni yeye mwenyewe tu, watanzania wengi wanaosailiwa unakuta wanajiandaa mwezi mzima kwa kukariri na kurudiarudia kila mara possible q&a za usaili karibu mwezi mzima hahah,halafu hao hao makazini ni kiswahili mwanzo mwishooo hapo umedhamiria kujenga (msingi )chini vizuri ila tofali ni za udongo...hizi lugha mbili at least ni vizuri zikaenda sambamba kwenye matumizi rasmi hapa nchini.
 
na watoto wote wa watumishi wa Serikali wasomeshwe kwa kiswahili katika shule zetu za umma ili tuenzi lugha yetu ya kiswahili inayokua kila kukicha katika ukanda wa SADC.

Mtumishi yoyote wa umma atakayebainika anasomesha watoto wake shule za Private kwa lugha ya kigeni basi huyo anakizana na Sera yetu ya kukuza kiswahili na si Mzalendo.

Nchi hii unafiki umejaa hasa wa viongozi

Wabunge wote,viongozi wa Serikali na mahakama watoto wao wanasoma English medium halafu kinafiki wanasisitiza kiswahili mbona hawapeleki watoto wao shule za kiswahili? Hata wakifaulu kwenda sekondari za Serikali hawataki wanapeleka shule private
images (3).jpg

Kuondoa unafiki shule zote za Serikali zibadilishwe kuwa English medium
 
Hata kama kinatambulika SADC au AU, bado kiswahili hakifai kwa kufundishia, kuna vitu vingi vinakosekana kwenye lugha ya kiswahili....maneno mengi ya science. Ebu acheni siasa, watoto wenu mnawafunza English, wetu wakajifunze Kiswahili? Huu ni ujinga mkubwa, kwani tukitumia English kuanzia darasa la kwanza tatizo lipo wapi? Pia kujua lugha zaidi ya moja ni kosa? Kuna rafiki anajua lugha tano...na huko kwenye kazi anapeta ile mbaya, yaani English ipo juu, French, Kiswahili, Kinyarwanda, Luganda na Espanol. Mbona hajapungukiwa chochote....mbona kuna watu wanaongea lugha zetu za kikabila vizuri, kwanini tushindwe English lugha rahisi, hapo uweze kupata kazi nzuri? Acheni uvivu watanzania.
ASANTE BABA!!

MWIGURU KAMA AMESHINDWA KAZI AKAE PEMBENI
 
Back
Top Bottom