Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama naweza kwa ung'eng'e nitashindwaje kwa lugha yangu adhimu niliyozaliwanayo..? Ila Binafsi Interview inayohusiana na professional husika kwa Kiswahili haimake sense..Ina maana mtu akikuuliza utakayofanya juu ya au kuhusiana na taaluma yako utashindwa kumwelezea kweli? Yaani utashindwa kujieleza kuwa nafanya au nitafanya hivi na vile? Labda umekariri tu na hujui unachokifanya au utakachofanya sambamba na taaluma yako.
Mimi sijasema kuwa najua kingereza mkuu sababu hyo lugha nimejifunzia ukubwani.. Ila mtu yeyote akiongea namuelewa na nikiulizwa swali siwezi kushindwa kujibu kwa sababu ya lugha ni ya kingereza, nitajipiga broken hivyohivyo Ila naamini muuliza swali atakuwa amejua kuwa nimemuelewa na nimemjibu LABDA kama hicho kitu sikijui kabisa maana unaweza kuulizwa swali kwa Kiswahili kama Hilo swali hulijui basi utashindwa kujibu Ila sio kwamba kiswahili/lugha hujui(Na ndo maana saili kama zinazofanywa PSRS wanaangalia zaidi CONTENT, unauliza swali toa ushirikiano ukimaliza unaamsha). kwahyo hata kama hapo nimeandika broken Ila mtu anayejua basi anajua kuwa nilikuwa na maana gani.. hiyo ndo point nazungumziaHiki ndo Kingereza unachovimbia.!!
Viwanja karibu 99% ni mali ya ccm baada ya kuanza vyama vingi 1992CCM haina timu bwashee.
Hii imekaa vizuri wengi wanashindwa kufanya interview sababu ya mkinzano na ujuzi mdogo wa kingereza
Hatua ya hovyo sana hii. Inalenga kushusha viwango vya elimu.
Haijakaa vizuri. Hatulazimiki kujua lugha moja tukasema basi. Elimu tuliyoopata imetolewa katika Kiingereza!! Ujuzi tulioupata umefundiswa kwetu katika Kiingereza.
Tusitumie udhaifu wa kutojua Kiingereza kukifanya Kiswahili kishike hatamu!! Taifa hili halifanyi mambo yake peke yake - kwa kushikilia Kiswahili huku tukijionesha tumepata maarifa kwa Kiingereza halafu Kiingereza kikatushinda - tunaonesha hatuna maarifa (waliopata ajira nje na mbali na eneo la Kiswahili wanatambua hili)!
Tufundishwe lugha zote mbili na tuzijue kwa ufasaha. Zipo nchi ni mfano!!! Tubadili mfumo na kuanza Kiingereza toka shule ya msingi - ingekuwa hivo tusingezungumzia hili.
Udhaifu wetu kwenye Kiingereza isiwe ndio ishara kwamba Kiswahili ni bora huku tumepewa maarifa kwa Kiingereza!!!
Hii ni sawa sina pingamizi hata kidogoKiswahili ndio lugha yetu inatambulika SADC na Umoja wa Afrika. Wazri wa fedha ahoji sababu ya kufanya usaili wa watumishi wa serikali kwa lugha ya kiingereza na kushindwa kukipa nguvu Kiswahili.
Ameshauri kishwahili kitumike katika usaili
Hapana mkuu makazini kinatumika kiswahili 80% hakuna sababu ya kufanya interview kwa kiingerezaKwani wamesoma kwa kutumia kiswahili??
Masomo yote ni kiinglish isipokua lugha ya kiswahili.
It doesn't make sense at all.
Mfano unaulizwa law kiswahili wewe umesoma fizikia? Unajibu ndiyoHii imekaa vizuri wengi wanashindwa kufanya interview sababu ya mkinzano na ujuzi mdogo wa kingereza
Elimu vyuoni inatolewa kwa lugha gani?wachina,warusi,waarabu Wana fanya usaili wa kazi kwa lugha gani?