Dkt. Mwingulu Nchemba awataka Wabunge kujadili sheria wakati wa Utungwaji na Siyo Wakati wa utekelezaji Wake

Dkt. Mwingulu Nchemba awataka Wabunge kujadili sheria wakati wa Utungwaji na Siyo Wakati wa utekelezaji Wake

😂

Nimewaona Wakenya wanajadili Finance Bill ya 2024/25 kwenye Media zote

Hapa Bongo wengi hawajui Finance Bill ni nini wanashabikia Mijadala ya sidiria tu

Dr Mwigullu yuko sahihi
Wabunge wa CCM wanapatikana kwa rushwa na ushirikina, wapo busy na kuiba mali za umma wapate utajiri
 
Sheria nyingi zilifanyiwa mabadiliko ya haraka haraka kipindi cha magufuli yote hayo ili akusanye hela nyingi kugharamia miradi yake baada ya wahisani au mabeberu kwa maneno yako kumpiga PIN.

Kuna haja ya hizo sheria kupitiwa upya ziwe na Maslahi ya wananchi na sio kukandamiza tu. Hii ni pamoja na sheria iliyoleta kikokotoo Kipya. Wizi mtupu, na itashangaza kuona waajiriwa bado wakiunga Foleni kuipigia kura CCM.
Tanzania ni nchi ya kijinga sn haina mifumo sahihi zaidi tunaishi kwa utashi na hisani ya Rais inategemea ameamkaje siku hiyo.
 
Hadithi ys walipakodi ni wachache ni ya kufikirika zaidi kuliko uhalisia. Walipa kodi Tangabyika ni wengi ila inategemea kodi unaiitaje.

Mfano wakulima wote ambao ni kaMa asilimia 65 ya watanganyika wanalipa kodi wakati wanapopata income kutokana na kuuza mazao yao ila kodi inayolipwa inaitwa cess na inachajiwa kwa kila kg ya mazao wanayouza, ingawa inaonekana kana inalipwa na mnunuzi lakini wanaolipa ni wao wakulima.

Mfanyakqzi yeye anaLipa kodi inayoitwa PAYE. Mfanyabiashara analipa incone taxi kila robo mwaka kwa kutegemeana na faida aliyopata.

Ikatikati kila mtu akinunua bidhaa au huduma analipa VAT sasa unasemaje walipakodi ni wachache, Nenda katika halmashauri angalia kwa-mwaka wanakusanya bilioni ngapi toka katika mazao mfano halmashauri zinazolima korosho , miti nk.
On top of that, Kila anayemiliki simu na tunaambiwa kuwa Kuna laini za simu zaidi ya milioni 60 nchini na Kila laini ya simu, Kila inapofanya muamala wa pesa, inalipa Kodi

Hivi unawezaje kusema walipa Kodi nchini ni less than 10%?😚
 
Bunge letu lina wabunge wengi sana wasomi. Pia mtu anaweza akawa na Elimu kubwa na akawa na mchango mdogo sana katika mijadala.maana hii inategemea na kile atakacho amua kusimamia kati ya UKWELI na siasa au propaganda.

Mwingine anaweza asiwe na Elimu lakini akawa na mawazo mazuri sana kutokana na uzoefu wake katika eneo fulani iwe ni katika biashara,madini,uvuvi,uchukuzi n.k.
Hawa waliopitisha mkataba wa bandari? We kijana no taka taka ya Taifa kabisa.
 
Kwani mkataba wa bandari una shida gani? Usipende kusikiliza porojo za watu mitandaoni wenye lengo la kupotosha ukweli
Wale mambwana wametupa account Mpya za kwao za kulipia tozo mbali mbali na hawajaweka hata mchanga kama kuendeleza so now wanakula vyetu.

Unajua Hilo? Nikikuambia wewe ni kijana takataka utakataa.
 
Sheria inaweza kupitishwa kwa dhamira njema na baadaye ikaonekana kuwa mzigo kwa watu. Ndio maana kunafanyika marejeo na masahihisho kuendana na wakati.
Umerudi pale pale na tumekubaliana Wanaozipinga sheria baada ya kupitishwa wanahoja na sio vitisho vya Mwigulu kwamba watu wahoji kipindi zinatungwa tu na zikishapitwa ni utekelezaji!
 
Ameyasema hayo kutokana na swali lililoulizwa na Mbunge wa Mbozi Mheshimiwa George Ranwell Mwenisongole aliyetaka kujuwa na kufahamu ni kwanini vyama vya ushirika vinalazimishwa na TRA kununua na kuwa na mashine ya EFD wakati havifanyi biashara na huuza mara moja tu kwa mwaka.
Kwa wabunge wa CCM kusoma muswada, kuulewa na kuuhoji kwa kina ni ndoto ya alinacha!
Wao kila kitu ni ndioooooooooooooooo!
 
Ndugu zangu Watanzania,

Waziri wa Fedha Mheshimiwa Daktari Mwingulu Lameck Nchemba Amewataka Waheshimiwa Wabunge pamoja na watanzania wote kujenga utamaduni wa kujadili sheria wakati wa mchakato wa Utungwaji wake na siyo wakati wa utekelezaji wake.

Ameyasema hayo kutokana na swali lililoulizwa na Mbunge wa Mbozi Mheshimiwa George Ranwell Mwenisongole aliyetaka kujuwa na kufahamu ni kwanini vyama vya ushirika vinalazimishwa na TRA kununua na kuwa na mashine ya EFD wakati havifanyi biashara na huuza mara moja tu kwa mwaka.

Akijibu swali hilo Mheshimiwa Dkt Mwigulu amesema kuwa Ukusanyaji wa kodi unafanyika kwa mujibu wa sheria namba 36(1) ya usimamizi wa kodi ya mwaka 2015. ambapo ni lazima mfanyabiashara anayesambaza bidhaa au kutoa huduma au kupokea malipo kutokana na malipo ya huduma aliyotoa anatakiwa kutoa risiti za kieletroniki.

Lakini pia amesema ya kuwa sheria inasema kuwa mfanyabiashara yeyote anayefanya mauzo ghafi ya millioni 11 na kuendelea kwa Mwaka anapaswa kuwa na mashine ya kielektroniki EFD. Ameendelea kusema ya kuwa lengo ni kuhamasisha utunzaji wa kumbukumbu ambapo EFD ni njia nzuri na rahisi yenye ufanisi mzuri wa utunzaji wa kumbukumbu kwa mfanyabiashara.

Amesema pia kuwa haiwezekani mwalimu wa shule ya msingi atozwe kodi halafu aende aachwe tajiri.au mtu mwenye kipato cha chini cha mauzo chini ya Millioni 3 kwa mwaka atozwe na kulipishwa kodi halafu aende aachwe anayepokea malipo ya millioni Mia Moja.Amesema hii haiwezekani na siyo haki. Na kwamba mwezi ujao bunge litajadili pia masuala ya Kodi ,hivyo kama kuna sheria wabunge wanaona haifai basi ndio wakati wa kuijadili ili kuangalia kama itolewe au kufutwa au kufanyiwa marekebisho.

Mimi Mwashambwa Lucas ningependa kusema ya kuwa Waheshimiwa wabunge wetu wawe na utaratibu mzuri wa kujisomea,kutafiti,kuomba ushauri na kusikiliza wananchi wanasema nini wakati wanapokuwa wanajadili na kupitisha sheria fulani Bungeni itakayotumika kwa wanachi na Taifa kwa ujumla wake.

Nasema hili kwa kuwa imekuwa inasikitisha sana ,kuleta aibu , kufedhehesha,kuonyesha kukosa umakini na kutoelewa kwa undani kile wanachokipitisha ndani ya Bunge. kwa sababu ni kawaida unakuta sheria fulani inapita kwa kishindo na kwa kura zote za ndio, halafu baada ya muda wananchi wakianza kulalamika na kukosoa sheria husika mitaani unaona kuna wabunge wanaanza kushangaa kana kwamba ni kitu kigeni masikioni mwao na wala hawajawa kukisikia wala kushiriki katika mjadala wake wala kuunga mkono.

Jambo linaloonyesha aidha waheshimiwa wabunge wanakuwa wakati mwingine hawajapitia vifungu vyote na makabrasha yote yaliyo mezani pao kujuwa maana ya kile wanacho kipitisha na kukiunga mkono. Wakati mwingine mpaka unajiuliza inakuwaje mwananchi wa kawaida aone kwa haraka na ndani ya muda mfupi tatizo la sheria fulani ,halafu Mbunge anayekaa bungeni na kulipwa posho kwa ajili ya kazi hiyo ashindwe kuona tatizo hilo mpaka anapokuja kuona wananchi wakilalamika na kukosoa kwa nguvu na ndipo sasa naye Mbunge aanze kulaumu na kulalamika kana kwamba hakuwepo wakati wa utungaji na upitishwaji wake?

Tatizo nini nini? Shida inakuwa wapi? Kwanini hili linatokea kwa sheria inatungwa leo halafu kesho inakuwa inahitaji mabadiliko na marekebisho? Ni wapi panakosekana umakini? Ni nani hatekelezi wajibu wake? Je, waheshimiwa huwa wanapigia makofi na kuunga mkono mambo wasiyo yajua? Nini kifanyike hali hii isiwe inatokea? Kwa sababu tumeona jambo hili katika suala la kikokotoo ambapo wabunge wakiwa wakali kana kwamba siyo wao waiopitisha na wala hawajawahi kushiriki katika mjadala wa aina yoyote ile unaohusu kikokotoo.

Naweka kalamu yangu chini na kuishia hapa, sitaki kuwachosheni. Lakini tujiulize pia kwanini walipa kodi Tanzania ni wachache sana kuliko idadi ya watu wanaostahili kulipa kodi? Kwanini watanzania hawapendi kulipa kodi na hutafuta njia za kukwepa kulipa kodi kuliko kwenda kulipa kwa hiyari? Je ni kutokutambua umuhimu wa kodi kwa maendeleo ya Taifa letu? Je, ni kutokujua kuwa nchi inaendeshwa kwa kodi na kila kitu tunachotaka kufanyiwa na serikali yetu kinatokana na kodi zetu, ambazo tunatakiwa tuone fahari kulipa badala ya kuwa wakwanza kutengeneza mifumo ya Ukwepaji kodi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Kwa hiyo nayo hii ni stori?
 
😂

Nimewaona Wakenya wanajadili Finance Bill ya 2024/25 kwenye Media zote

Hapa Bongo wengi hawajui Finance Bill ni nini wanashabikia Mijadala ya sidiria tu

Dr Mwigullu yuko sahihi
Hapana! Watawala wanafurahi na wanaweka mazingira magumu kwa wananchi ili wasishiriki ili iwe rahisi kuwaibia

Huyu dk anajifanya ana uchungu sana mwalimu kulipa Kodi alafu wafanyabiashara wasilipe Kodi.

Sawa lakini je wabunge na wakuu wenye nchi wanalipa Kodi, wanalipa nssf au bima ya afya??

Ccm huwalazomisha, huwaadaa, huwalewesha na kuwapumbaza wabunge kabla ya kupeleka miswada bungeni,

Wabunge hustuka ayari weishapitisha Sheria mbovu na kandamizi

Kwanza waache michexo michafu wawaache wabunge wawe huru
Watungie Sheria nzuri

Hivi ni kweli walipitisha uuzwaji wa bandari kwa hiari yao??
 
Simkubali Bwana Mwigulu PhD,lakini katika hili naunga mkono hoja yake.Ni Wabunge wachache sana ambao hujipa muda kusoma na kufanya tafiti juu ya mambo mbalimbali ya kibunge.

Zaidi walio wengi wanajua kupitisha maazimio tu,ambayo hayahitaji critical thinking.Hata Job Ndugai aliwahi kushangaa sheria fulani ya uhifadhi ilipitaje na wakati huo huo Yeye ndo alikuwa kwenye kiti wakati Sheria inapita.

Bure kabisa Wabunge wetu.
Alichosema waziri sio sahihi

Mfano.mimi nimeingia bungeni Leo Naona Kuna Sheria iliyopitishwa huko nyuma sio sahihi lazima nitaipinga bungeni Ukiniambia nilitakiwa kujadili wakati inapitishwa sio kweli.Kuna Sheria mfano zilipitishwa na wabunge Miaka ya sitini huko wakati hata wabunge wa Sasa hawakuwepo huwezi zuia wasijadili kuwa walitakiwa kujadili wakati inapitishwa
 
Kama kukipa Kodi kutenda Haki.kila mtu alipe Kodi ikiweko Raisi ,mawaziri na wabunge

Hilo jukumu.la kulipa Kodi ni la wananchi tu wengine ? Ncho hii Ina matabaka kwenye ulipaji Kodi bunge lijitafakari pamoja na Raisi mwenyewe
 
Back
Top Bottom