Kiukweli kuna wizara nyingine mtu anapewa siyo kwa kuwa ana uelewa, bali ni mweupe peee kichwani na ili kuficha aibu yake kutokana na kutimiza malengo fulani basi anapewa wizara ambayo ni vigumu kumgundua.
Mfano hai ni wizara ya ulinzi ambayo inaongoza majeshi ya ulinzi na usalama na waziri wake Dkt. Hussein Mwinyi. Hii wizara kwakuwa waziri wake ni kama hana kazi ya kumuweka kwenye vyombo vya habari mara nyingi basi ni vigumu kuutambua uelewa wa waziri husika.
Kiukweli sikujua kama waziri Hussein kichwani ni mweupe hivi hadi alipoanza kufuatwa fuatwa kwenye vyombo vya habari kutokana na hadhi yake aliyo nayo sasa. Itoshe kusema Hussein ni kama mgeni fulani asiyejua chochote kwenye siasa.
Amehojiwa sana na wana habari, majibu anayotoa ni kama mtoto anayelia lia! Hana hoja. Mfano kitendo chake cha kuelezea kura za wajumbe alizopata na jinsi alivyochanganua ni kama hajui jinsi anavyochimba kaburi lake kisiasa huko Zanzibar! Huyu angekuwa mfano waziri wa ardhi asingemaliza hata miezi sita ndani ya wizara hiyo.
Naamini kuwa, kama Hussein atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Magufuli kuwa Rais wa Bara basi Rais halisi wa Zanzibar atakuwa John Magufuli. Kwa mara ya kwanza kabisa Zanzibar itakuwa imepata Rais kamili kutokea Bara.
Aidha nimegundua kuwa ni kosa kubwa sana kumchagua Rais wa Zanzibar ambaye ametumika kwa muda mrefu ndani ya serikali ya Bara! Huyo ni kilaza kamili!
Ilikuwa ni vigumu sana kugundua competent ya Dkt. Hussein akiwa waziri wa majeshi maana waamuzi wakuu wa majeshi ni mkuu wa majeshi na Rais na ndiyo maana mkuu wa majeshi anapata heshima na ulinzi kuliko waziri wake ambaye kiitifaki ni boss wake! Wonders!
Namalizia kwa kusema, Waziri wa ulinzi na JKT wa Tanzania ndiye waziri asiye na kazi yoyote ya kimaamuzi ndani ya wizara zaidi ya kuwawakilisha bungeni! Na mbaya zaidi ulemavu mkubwa wa waziri husika unachangiwa na kauli ya "Majeshi yetu hayasemwi" Kwahiyo ni vigumu hata ndani ya bunge kujua uelewa wa waziri huyu kisiasa na kiuongozi kwa kuwa tu majeshi yetu hayajadiliwi!