Pre GE2025 Dkt. Nchimbi: Maendeleo aliyoleta Rais Samia kwa miaka 3 Madarakani ni kama miujiza

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu Choice wewe ni ME au KE?, upo vizuri kwenye utunzaji wa taarifa, hongera zako mkuu.
Me ila nime like pages mbalimbali na sources mbalimbali ambazo naweza pata taarifa fasta nikiihitaji Kwa sababu napenda mijadala so lazima niwe na ushahidi.Biashara ya uzushi kwangu hapana.

Samia ndio pekee hapa Tanzania hana kashfa ya Rushwa Wala Ufisadi,Lisu amefukunyua kashindwa na yeye alikiri Hilo.
 
Sasa,msiweke vibweka vya maneno yasiyoweza hata kueleweka.Kutueleza kwamba ni "tangia dunia iumbwe" ni kutudharau na kutufanya mabwege mtozeni.She might have been doing better all the time;lakini,hizo praises zenu mnakufuru na kutukana watu.
Wewe achana na maneno ya kuchombeza wewe angalia hoja na ushahidi ulioko mezani.

Je unajua Samia amejenga shule za Advance 26 Kila Mkoa Moja Zenye hadhi Ile ambayo Wakoloni waliacha? Shule hizo ni maalumu Kwa Wasichana ,zinafanania namna hii πŸ‘‡

View: https://www.instagram.com/p/C4svgZ0Mkgi/?igsh=MWsyNWJjbGkyY2p4YQ==
 
Basi maskini hawawezi kuisha wote chini ya Dunia,hata America wapo tena wengi sana ,ukitaka source na takwimu nitakupa.

Mwisho unaposema wengi uwe unataka takwimu Kwa idadi au asilimia, takwimu zilizopo hazisapoti hicho unachokisema ingawa wapo.
 
Vipi kuhusu yule mtoto wake wa kiume Abdul?. Wanadai anamiliki yale maghorofa yanayojengwa Kawe, upo ushahidi wowote kwenye suala hilo?.
 
Vipi kuhusu yule mtoto wake wa kiume Abdul?. Wanadai anamiliki yale maghorofa yanayojengwa Kawe, upo ushahidi wowote kwenye suala hilo?.
Atamiliki vipi magorofa Mali ya Serikali? Yaani miradi ya NHCiwe Mali ya Abdul? Hizo ni siasa za majitaka Lazima kumchafua Rais hizo ni siasa sawa na kipindi kile JK ni Rais Kila kitu tulikuwa tunaambiwa na Cha Riz1.

Pili ni mwana ccm yupi hamiliki magorofa hapa Tanzania au Nje ya Nchi?

Mwisho hao wanaoeleza hayo yasiyo na ushahidi wawe wanaelwza na haya yenye ushahidi πŸ‘‡πŸ‘‡

View: https://youtu.be/3yonEHW1D9k?si=0CeZdxggtEHNhIU6
 
Basi maskini hawawezi kuisha wote chini ya Dunia,hata America wapo tena wengi sana ,ukitaka source na takwimu nitakupa.
Na kama hii ndio attitude ya viongozi / watumishi wetu basi hawafai kuwa viongozi (You Should Aim for the Moon) na nataka Viongozi wanaoamini kwamba Poverty is Man made na kwenye dunia ambayo inazalisha chakula kingi cha kuweza kulisha kila mtu mara saba..., wakati katika kila watu saba mmoja kati ya watu saba ana njaa kuna sehemu tumekosea na haitakiwi kuwa hivyo... Na unaongelea nchi nyingine ambazo kuna mifumo ya welfare na Taasisi za kutoa chakula kwa wasionacho au pengine kuna unemployment benefits, nashindwa kukuelewa...; alafu wewe unaongelea umasikini wa kukosa gari number E mimi naongelea umasikni wa kukosa / kutokuwa na uhakika wa mlo mmoja kwa siku let alone mitatu....
Mwisho unaposema wengi uwe unataka takwimu Kwa idadi au asilimia, takwimu zilizopo hazisapoti hicho unachokisema ingawa wapo.
Kwahio nahitaji takwimu wakati najua kabisa majority ya watanzania hawana ajira zinazoeleweka hata wale walionazo ukipiga uwiano wa bei ya bidhaa na kile wanachopata hakitoshelezi hata siku 10 katika mwezi let alone mwezi mzima (na hao ndio wapo well-off) angalau wana uhakika Benki itasoma mwisho wa mwezi ?

Nahitaji takwimu za nini wakati naona walinzi waliojazana kwenye kazi ni mpaka wazee wanaokesha na kufanya kazi mwezi mzima bila kupumzika kwa malipo ambayo hata nauli tu hayatoshi hivyo inabidi watembee kwenda kwao (tena bora wanafanya ulinzi huenda wanapata sehemu ya kulala sababu huko wanapopanga wanapunguza kugongewa milango ya kudaiwa kodi); na mzee huyu siku akiugua anaogopa kwenda hata hospitali kwa kukosa pesa za matibabu...

Huo ndio uhalisia wa Mtanzania wa Kawaida....
 
Do you expect Samia atamaliza shida za Watanzania Kwa miaka 3,5 au 10? Yeye anafanya pale atakapoweza na Kwa mujibu wa makubaliano ya kwenye Ilani.

Mwisho ku aim kwenye moon ni Suala Moja na uhalisia wake ni jambo tofauti.Hakuja waliowahi kufaulu Hilo hapa Duniani ila wapo waliojitahidi zaidi na Hilo ndio lengi kujitahidi kadiri inavyowezekana.

Ndio maana Sasa Samia amebadili Sera ya Elimu na kuleta bima ya Afya na anaendelea na maboresho ya sera za Kodi.

View: https://twitter.com/CloudsMediaLive/status/1772864025627349407?t=blS0PlFa1JHmcIheYqxyDg&s=19
 
Mimi nawataka hawa,, Nawataka hawa uchaguzi mkuu 2025,,

Nawataka hawa!!!!tuwanyooshe kwenye uchaguzi.

Naona Uchawa umezidi kuliko uhalisia.
 
Do you expect Samia atamaliza shida za Watanzania Kwa miaka 3,5 au 10? Yeye anafanya pale atakapoweza na Kwa mujibu wa makubaliano ya kwenye Ilani.
Kosa kubwa la kwanza ni kutaka Samia amalize au kuita Miradi ya Samia au Magufuli (Hakuna Miradi ya Mtu)... Inabidi kila anayekuja pale kuwepo na Miradi / Long term plans ambapo wadau wamepanga nini kifanyika kama Taifa no matter ni Chama gani au nani anachukua nchi....; Hatuwezi kuendelea kufuata matakwa / maono ya kila mtu anapokuja kwa miaka mitano (tutaendelea kufanya vitu vidogo vidogo ili mtu aonekane amefanya)
Anatengeneza au anaharibu ? Hakuna mtu wa kumfanyia mtu kitu bali kama Taifa hawa watunga sera wakihakikisha kwa nchi kama Tanzania yenye vyanzo vingi vya resources kila mwenye nguvu na uwezo anapata ajira yenye ujira kila mtu atajifanyia ya kwake na mambo yatakwenda.... Na hayo yote hayawezi kufanyika kwa yafuatayo:-
  • Nishati isiyo na uhakika na ya gharama (afadhali predecessor wake alishusha gharama ya kuunganisha watu na alitaka Bwawa limalizike haraka ili bei ishuke) awamu hii wamesema wala Bei haitashuka.
  • Unaongelea Bima, Bima lazima iwe bora na affordable sasa hivi kuna sarakasi sio tu kwamba sio affordable bali kuna huduma nyingi zimenyofolewa...
  • Kipindi cha sayansi na teknolojia kuna wale wachache wanajitahidi kupata elimu kwa kujifunza kwenye mitandao au wengine kutengeneza kazi kwenye mitandao (TCRA na Serikali kwa ujumla na Bei zao elekezi imefanya Bundle halishikiki)
  • Tunapoelekea nguvu kazi inazidi kutokuhitajika automation ndio imeshika hatamu...; yet tunaleta so called wawekezaji ili tugawane nao mapato badala kwenye sekta nyingine kubwa (mfano bandari) tungeweza kubaki na 100 percent ili kusaidia kupunguza makali ya wakosa ajira
  • Kukiwa na uhakika wa Transport watu kutoka makwao mpaka kwenye kuzalisha utawapunguzia watu mzigo mkubwa na kuwahi makazini (lakini zaidi ya kuleta ndoto za kuleta trams za umeme) kitakachotokea hata Train wanazomalizia gharama yake haina tofauti na usafiri uliopo sasa...
In short zaidi ya Awamu hii MIRADI kugeuka ndio MIRADI (wachache kunufaika na miradi ya kwenye makaratasi) hatuna any long term plans
 
Akisema muujiza anaelewa maana ya muujiza? Anazungumzia muujiza chanya au muujiza hasi?
No ajira,barabara mbovu, NHIF ni janga,ripoti ya CAG ni msiba kila kona, maisha yamepanda bei. Kama anazungumzia muujiza atakua amejitazama yeyetu kwamba huko alikokua na hapo alipo leo ndio muujiza
 
Miradi ya Magufuli ipo na miradi ya Samia ipo,huu ndio utaratibu ulioanzishwa na awamu ya 5 na unaendelea.

Gharama ya kuunganisha umeme ilishuka kutoka ngapi kwenda ngapi? Hakuna kushusha bei tofauti na zilizopo Kwa Sasa labda kwenye viwanda na Biashara kubwa.

Bima ipi sio affordable? Huduma zipi zimengifolewa maana Mimi Nina bima.Pili Bima ya Afya Kwa wote itakuwa more than affordable na Kuna watu zaidi ya mil.25 watapewa Bima Bure maana hawana uwezo wa kuchangia.

Awamu ya 6 ndio imewapa Vijana uhuru wa kutengeneza maudhui kwenye social platform tofauti na ukandamizaji wa awamu ya 5.Sekta ya mawasiliano ni Kati ya sekta zinazoongoza Kwa Ukuaji Kwa Sasa.

Sasa kama nyie wazawa ni incompetent na mnaendekeza Rushwa na Ufisadi ni Bora kubinafsisha Kwa wenye uwezo wale wa ndani au wa Nje.Kugawana Mapato sio tatizo.

Sayansi inazingatiwa sana kuanzia shule Hadi vyuoni mambo ni safi kabisa.
 
Wewe ni kakenge kweli kweli .

Nyambafu.
 
Miradi ya Magufuli ipo na miradi ya Samia ipo,huu ndio utaratibu ulioanzishwa na awamu ya 5 na unaendelea.
Kwahio sababu walifanya upuuzi awamu ya tano ambao ndio hawahawa wapo awamu ya 6 upuuzi huu uendelee ?
Gharama ya kuunganisha umeme ilishuka kutoka ngapi kwenda ngapi? Hakuna kushusha bei tofauti na zilizopo Kwa Sasa labda kwenye viwanda na Biashara kubwa.
Kwamba kuunganishwa kwa Tshs 27,000 haikuwahi kushuswa Samia akaja kurudisha kwenye malaki tena (au nilikuwa naota na haikutokea)?
Bima ipi sio affordable? Huduma zipi zimengifolewa maana Mimi Nina bima.Pili Bima ya Afya Kwa wote itakuwa more than affordable na Kuna watu zaidi ya mil.25 watapewa Bima Bure maana hawana uwezo wa kuchangia.
Kwamba hii Bima ni Fit for purpose ? Na ingekuwa Fit for purpose watu wangekuja na ideas za kuanza kuwakata watu kwenye Line zao za Simu ? Kwamba huduma zote zinapatikana kwenye Hio so called Bima Affordable au kuna Dawa zimepunguzwa ?
Awamu ya 6 ndio imewapa Vijana uhuru wa kutengeneza maudhui kwenye social platform tofauti na ukandamizaji wa awamu ya 5.Sekta ya mawasiliano ni Kati ya sekta zinazoongoza Kwa Ukuaji Kwa Sasa.
Wewe unaongelea uhuru jambo ambalo wala hauhitaji kupewa ni haki yako mimi naongelea Bei za bundle kuongezeka maradufu sababu ya upuuzi wa TCRA kuweka bei elekezi..., Naongelea hawa watunga sera wasio na mawazo mbadala wanaotoa suggestions na watu waanze kulipia mpaka whatsApp calls utadhani hawalipii kwenye kununua bundle
Sasa kama nyie wazawa ni incompetent na mnaendekeza Rushwa na Ufisadi ni Bora kubinafsisha Kwa wenye uwezo wale wa ndani au wa Nje.Kugawana Mapato sio tatizo.

Sayansi inazingatiwa sana kuanzia shule Hadi vyuoni mambo ni safi kabisa.
Kwahio incompetence ya hiki kizazi ndio iwe hukumu kwa vizazi vijavyo ? Kama sisi ni incompetent ndio watu wafanye maamuzi ya ku-cost vizazi ? Kwamba ni incompetent hata wa kuleta wataalamu wafanye tuwalipe na sisi kubakia na asilimia 100%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…