Pre GE2025 Dkt. Nchimbi: Maendeleo aliyoleta Rais Samia kwa miaka 3 Madarakani ni kama miujiza

Pre GE2025 Dkt. Nchimbi: Maendeleo aliyoleta Rais Samia kwa miaka 3 Madarakani ni kama miujiza

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu mfumo dume umechangia,walio wengi walidhani Mama Samia ni mtu wa kuendesha tu,hana lolote.Lakini pale alipoanza kuonyesha makali ya kistaarabu katika kubuni na kusimamia mfuko wa COVID,wenye riba karibu sifuri,ndio tukasikia mambo ya nchi imeuzwa wakati huko nyuma kimya kimya tulikuwa tukikopa kwa riba kubwa hata 15% kwa benki za Shailoki"Kausha Damu"tena grace period ya muda mfupi,sababu ya kutozingatia kanuni za Benki hizo za Maendeleo zenye riba nafuu.Miradi ya Mjomba Magu karibu yote ipo hatua nzuri na nyingine imekamilika.
Mama ni msikivu,hana majivuno,na nchi inasonga mbele.
Kilichobaki deni kwa Mama yetu ni katiba mpya ili asije tena mtu wa kutugeuza watumwa ndani ya nchi yetu.
🆒📝🤝🙏🎁
 
Nchimbi awaite Waandishi wa Habari wa CNN MSNBC Al Jazeera TV 5 BBC n.k n.k awaeleze haya wayabandike huko kwao.

Hizi ni Ngonjera za Kinafiki.

LUHANGA MPINA ajibiwe hoja zake.
Keyboard drop
 
Hayo yameelezwa na KM wa CCM Dkt.John Nchimbi wakati wa ziara yake ya Mikoa 6 akiwa Njombe.

DK Nchimbi ameonekana kushangazwa na kufurahishwa na Wingi wa miradi na maendeleo yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika akisema ni kama miujiza maana kilichotakiwa kufanyika Kwa muda mrefu kimewezekana ndani ya mda mchache kabisa.

Kwa wasio fahamu,haters na wabishi hii hapa ni summary tuu ya kilichofanywa na Samia.👇👇

-Mapato ya TRA kuongezeka kutoka wastani wa 1.5T Hadi 2.2T(ongezeko bil.700 )

-Makusanyo ya Halmashauri kuongeza kutoka Bil.800 Hadi Trilioni 1.2(Ongezeko Bil.400)

-Ongezeko la Mapato ya Utalii Hadi 3.5T(Watalii 1.9m) kutoka 3T(Watalii 1.5mln).

-Ujenzi wa Bandari Ziwa Nyasa(MbambaBay),Ziwa Tanganyika(Kigoma),Ziwa Victoria (Mwanza,Bukoba,Chato) na Bhari ya Hindi(Dar,Tanga,Kilwa na Mtwara).

-Ujenzi wa viwanja wa ndege 15 Unaendelea Tanzania nzima eg Sumbawanga,Tabora,Shinyanga,Kigoma,Ruaha NP,Nyerere NP,Moshi,Iringa nk huku akikamilosja viwanja vya Songwe, Songea,Iringa na Katavi.

-Ujenzi wa Hospital za Wilaya mpya 129 ,Mikoa 7 na Rufaa za Kanda 3(Mtwara,Kigoma na Ukerewe).

-Ujenzi wa Vituo vya Afya vipya 402 kwenye kata za kimkakati hapo tozo za miamala (234).

-Ununuzi wa vifaa tiba ambavyo havikuwahi kuwepo Kwenye hospital za Tanzania mfano Ultra Sound 192 ,Digital X-rays 147,CT Scan 32,MRI machines 7.

-Ujenzi wa majengo ya Wagonjwa Mahututi(ICU) 28 na Dharula 127,

-Upanuzi na Ujenzi wa Vyuo Vikuu vipya na kampasi za Vyuo kwenye Mikoa 14 ambayo swali haikuwa na Vyuo Vikuu au kampasi eg Kigoma,Simiyu,Njombe,Ruvuma, Rukwa,Katavi,Shinyanga,Lindi,Mtwara nk.

-Kaongeza Bajeti Kila Wizara ila Kwa upekee ni Wizara ya Kilimo(Umwagiliaji )kutoka Bil.270 Hadi Bilioni 950.Skimu Mpya za uwamwagiliaji hectare 95,000 zimejengwa na kufufuliwa,kafungua ofisi za Kilimo Kila Wilaya na kaajiri Wataalamu na kawapa vitendea kazi.

-Kaondoa shida ya vitambulisho NIDA,zaidi ya vitambulisho 12,000,000 vimegawiwa.

-Ujenzi wa minara mipya 1,200 ambapo Kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali minara 728 inaendelea na Ujenzi Kwa Bilioni 126.(Kijijini kama mjini)

-Amefikisha maji ya Bomba Kwa zaidi ya Vijiji 11,000.(Kampeni ya kumtua Mama ndio kichwani).

-Amefikisha umeme Kila Kijiji,kazi inaendelea kwenye vitongoji na migodi ya umeme.

-Amewasha Umeme gridi ya Taifa Mikoa Kigoma,Katavi na kazi zinaendelea Rukwa ,Lindi, Mtwara.

-Kazi zinaendelea ujenzi wa Vyanzo vipya vya Umeme eg Mto Malagalasi,Kakono,Umeme Jua Kishapu,Joto Ardhi Mbeya nk

-Amejenga zaidi ya Shule Mpya za Sekondari 3,200 ,shule za msingi zaidi ya 300 na madarasa 24,000 ,mabweni 137 nk

-Kupitia TanRoads amekamilisha zaidi ya km 1,000 za lami na zingine zaidi ya 3,700 zinaendelea na Ujenzi.

-Kupitia Tarura amejenga zaidi ya km 800 za lami na zingine zaidi ya 500 zinaendelea na Ujenzi (Hapa amefungua maelfu ya Vijijini Kwa Barabara Mpya za changarawe na madaraja). Bajeti ya Tarura aliongeza kutoka bil.270 Hadi Bil.800.

-Sekta ya mifugo amegawa Boti za Kisiasa zaidi ya 200 na viximba zaidi ya 1300 Kwa Vijana.

-Sekta ya Elimu kaongeza mikopo Kwa wanafunzi ambapo Sasa Diploma Hadi Chuo Kikuu wanapata,chekechea Hadi form six Elimu Bure(kafuta ada ya form Six),Kafuta Mapenato na mambo ya hivyo ya Bodi ya Mikopo.

-Katoa Ajira zaidi ya 55,000 kada zote huku Elimu na Afya wakipewa kipaombele.

-Anajenga na kukamilisha zaidi ya miradi ya maji 3,700 mikubwa Kwa midogo mfano mradi wa Miji 28,bwawa la kidunda na kukwamua miradi iliyokwamba kama same-mwanga,Tarime-Kiabakari nk.

-Kwenge sekta ya biashara baada ya maboresho maelfu ya miradi imemenika Kila sekta baada ya Wafanyabiashara kurejesha Imani Kwa Serikali Kupitia sera ya Diplomasia ya Uchumi na kuifungua Nchi.Hakuna ziara ambayo mama alifanya Nje ya Nchi hajakutana na Wafanyabiashara wa Kimataifa.

-Sekta ya michezo na Burudani.Huko Kila mtu anajua kwamba Mama alikatabati viwanja,akaleta ufunguzi wa AFL na sasa ameileta Afcon 27 na uwanja Mpya inajengwa Arusha.Likewise kuwapa mikopo Wasanii.

Kiufupi ni vigumu kuelezea vyote,pamoja na Changamoto ila Mama kaupiga mwingi ,Anatosha na Chenji inabakia.

View: https://www.instagram.com/p/C59CY7uMJC5/?igsh=MTNiYnozM2hubjMwZQ==
My Take
Yote hayo kafanya na anaendelea kufanya lakini hajawahi acha mradi hata 1 aliourithi kutoka Kwa Mwendazake kama Bwawa la JNHPP,Daraja la JPM,EACOP,SGR,Ndege Mpya,Ujenzi wa Mji wa Serikali na hajatoa visingizio.

View: https://twitter.com/MfanyakaziNews/status/1781317600514809949?t=yhy9JBufLMEhmo34FTghDg&s=19

Hebu acheni kutufanya wapumbavu kiasi hicho.Ni kipi tunachoweza kujivunia kuwa ni maendeleo kitaifa,angalau kiwe ni alama ya utawala huu?Sanasana ni hali ya wananchi kurudishwa nyuma miaka 10+.
 
Kwahio kinachofanyika sasa ni Miujiza na wakiomba waendelee kuwepo ni muendelezo wa hii hii Miujiza ? (More of the Same) ?

Nadhani Kitaa ukiwaambia hivi watakwambia Ugumu wa Maisha umeongezeka Leo ni Mbaya afadhari ya Jana sasa kama watumishi wetu wanaona kwamba leo ni nzuri (miujiza) nachelea kusema either they are out of touch au wanaridhika na mediocrity...
Ule utawala wa maisha bora kwa kila mtanzania ulisababisha baadhi ya watu kuwaza na kusema ''bora kuzaliwa/angezaliwa mbwa/paka ulaya kuliko hali ya maisha anayoishi Tanzania akiwa binadamu ,ni rahisi kuona/kuhisi ni mawazo ya kijinga, lakini ilidhihirisha hali ngumu anayo/wanayo ipitia.Lakini kwa hali iliyopo sasa hivi,ni bora ya utawala ule.
 
Ule utawala wa maisha bora kwa kila mtanzania ulisababisha baadhi ya watu kuwaza na kusema ''bora kuzaliwa/angezaliwa mbwa/paka ulaya kuliko hali ya maisha anayoishi Tanzania akiwa binadamu ,ni rahisi kuona/kuhisi ni mawazo ya kijinga, lakini ilidhihirisha hali ngumu anayo/wanayo ipitia.Lakini kwa hali iliyopo sasa hivi,ni bora ya utawala ule.
Ukishakuwa na perception ya kwamba unatawaliwa / utawala ni sawa na sio kwamba hawa ni watumishi wetu tunaowalipa na tumewapa vyeo kama dhamana utaendelea kuona kila kinachofanyika ni Hisani na sio wajibu..., hence hata ukipewa pungufu utashukuru na sio kuhoji kwanini hakiendani na malipo unayowapa...
 
Ukishakuwa na perception ya kwamba unatawaliwa / utawala ni sawa na sio kwamba hawa ni watumishi wetu tunaowalipa na tumewapa vyeo kama dhamana utaendelea kuona kinachofanyika ni Hisani na sio wajibu..., hence hata ukipewa pungufu utashukuru na sio kuhoji kwanini hakiendani na malipo unayowapa...
Ni kweli kuwa hawa n[viongozi]ni watumishi wetu kama ambavyo JPM alivyokuwa akiwasisitiza wasaidizi wake kuwa wananchi [walipa kodi]ndio waajiri wao...Ni kwanini hatuna nguvu/uwezo wa pamoja wa kuwawajibisha wanapo kosea,kama ilivyo kwa baadhi ya mataifa mengine ?Hapo ndipo tatizo lilipo,katiba na sheria zetu zimekuwa kinga yao na kuwafanya waitupilie mbali hiyo dhana ya kuwa wananchi ndiyo waajiri wao,matokeo yake wanageuka kuwa miungu watu/
 
Hebu acheni kutufanya wapumbavu kiasi hicho.Ni kipi tunachoweza kujivunia kuwa ni maendeleo kitaifa,angalau kiwe ni alama ya utawala huu?Sanasana ni hali ya wananchi kurudishwa nyuma miaka 10+.
Usiwe unauliza swali la kipumbavu na kipunguani,hayo niliyoeleza hapo Juu yamefanyika Burundi na hivyo Warundi ndio wanatakiwa kujivunia? Kwa akili zako wewe kitu Cha kujivunia na alama kintakiwa kuwaje? Acha upunguani basi.

Wananchi wa Kalambo walioachiwa alama hii ya daraja watamkumbuka Mama Yako? Unataka nikutajie vitu specific si nitajaza servers?
IMG_20240405_151325_240.jpg
IMG_20240405_152827_424.jpg
IMG_20240405_151434_358.jpg
IMG_20240405_153136_349.jpg
IMG_20240405_154555_271.jpg
IMG_20240405_154818_848.jpg
IMG_20240405_154559_152.jpg

My Take: Majitu majinga yaliyojaa chuki za kipumbavu kama wewe ni hatari sana Kwa Taifa.

Kusoma hujui na picha huoni? Waliosema Nabii hakunaliki kwao hawakuwa wajinga.

View: https://twitter.com/ccm_tanzania/status/1781731724684042444?t=LwQSgtN4xldHxRV4qnXsbA&s=19

Mwisho jitu halijui chochote Cha maana kinafanyika hata hapo ulipo aidha Kwa sababu huna pesa za kusafiri,mbaya zaidi hujui hata upate vipi sources za taarifa kujua nini kinafanyika hapo hapo mkoani kwako au kwingineko ila unaropoka tuu kama punguani.
 
Ajira kiasi gani?
Mfumuko wa bei?
Kikokotoo?
Biashara ngapi zimeanzishwa?
Biashara ngapi zimefungwa?
Bima ya afya?
GDP per capita?
Viwanda?
Nauli za ndege?
Ajali za barabarani zimepungua kwa kiasi gani?
Katiba mpya?
Wakikujibu nitagi.

Hata wakikutukana tu
 
Nchimbi awaite Waandishi wa Habari wa CNN MSNBC Al Jazeera TV 5 BBC n.k n.k awaeleze haya wayabandike huko kwao.

Hizi ni Ngonjera za Kinafiki.

LUHANGA MPINA ajibiwe hoja zake.
Keyboard drop
Punguani wenzenu ndio watawajibu
 
Ajira kiasi gani?
Mfumuko wa bei?
Kikokotoo?
Biashara ngapi zimeanzishwa?
Biashara ngapi zimefungwa?
Bima ya afya?
GDP per capita?
Viwanda?
Nauli za ndege?
Ajali za barabarani zimepungua kwa kiasi gani?
Katiba mpya?
Kwahiyo katiba mpya ni maendeleo? BAVICHA mna vituko
 
Hata deni la Taifa nalo ni muujiza ndugu Katibu Mkuu.

Hakuna Rais akiyethubutu kukopa namna hii tangu Uhuru 1961.
 
Back
Top Bottom