Dkt. Nchimbi: Rais Samia anaungwa Mkono na wana CCM wote

Dr Nchimbi KM wa CCM akiongea kwenye kikao cha makatibu wakuu wa vyama rafiki wa CCM amesema namnukuu "WATANZANIA WOTE WANAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA NA WANAJIVUNIA UWEZO WAKE WA KUONGOZA NCHI", mwisho wa kunukuu.
Kauli ya Kichawa kama hii hata KUPE Lucas Mwashambwa hawezi kuitoa maana anamwogopa Mungu. Ni Mtu asiyeamini uwepo wa Mungu ndiye anayeweza kutoa kauli ya uongo na kizandiki kama hii tena akijua yeye ni kiongozi wa ngazi ya kitaifa kichama na anaongea mbele ya viongozi toka nje ya Nchi. Kwamba Leo ukiitishwa Uchaguzi wakawekwa Watanzania mil.2 tu Samia atapata Kura mil.2?
Hivi hii Tabia ya kuwaona Watanzania wote ni wajinga nyie Wenye platform za kuongea ndio Wenye akili mmeitoa wapi? Yaani KM unawapiga propaganda hata wageni toka nje ya Nchi? Itasaidia nini wakifika Namibia au Msumbiji?
Hivi ungesema Watanzania WENGI wanamuunga mkono japo nalo halina uhakika ungepungukiwa nini zaidi ya kuchuma dhambi Kwa kusema uongo mchana kweupe?
20240320_135429.jpg
 
Hapa katibu kateleza nae ni binadamu raha ya kukalia kiti cha chama kubwa kila usemalo ni habari!
 
😂😂😂

Hii kali sana

Watanzania Wote maana yake na Mdude Nyagali yumo, Tundu Lisu yumo, Mwabukusi yumo dadeki 😂😂😂
 
Anaungwa mkono na Watanzania wote?

Huu ni mwanzo wa kuiba kura tayari!

Kauli hii inabidi ipingwe haraka sana na aombwa KM wa CCM akaifafanue vizuri mahakamani
 
#HABARI: Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, amesema kuwa Watanzania wote kwa ujumla wao wanajivunia uwezo mkubwa wa kiuongozi, anaouonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan ndani ya miaka 3 ya uongozi wake, ukijidhihirisha kwa namna anavyoiongoza nchi, kwa ajili ya maendeleo ya watu, ustawi wa jamii na kuimarisha utaifa nchini.

Akizungumza mbele ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 11 wa Makatibu Wakuu wa Vyama Rafiki vya Ukombozi wa Kusini, unaoendelea katika siku yake ya pili, kwenye Mji wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe, Jumanne, Machi 19, 2024, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Nchimbi, amesema Chama Cha Mapinduzi pia kinajivunia uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa jinsi anavyoendelea kuiongoza Serikali katika kutafsiri kwa vitendo utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 – 2025, akisisitiza kuwa CCM na wanaCCM wanamuunga mkono bega kwa bega.

“Kabla sijaanza kuwasilisha hapa…kwa ruhusa yako Mwenyekiti wa Kikao, imekuwa kama bahati nzuri zilizogongana leo…naomba niwataarifu Wajumbe wa Mkutano wa Kumi na Moja wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Ukombozi wa Kusini mwa Afrika kwamba leo ni maadhimisho ya mwaka wa tatu tangu Mhe. Samia Suluhu Hassan aliposhika Madaraka ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania miaka mitatu iliyopita.

“Kwa kweli ninajivunia sana Rais Samia Suluhu Hassan, si kwa sababu tu mimi ni mpigania haki za wanawake, bali kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa uongozi mzuri anavyoendelea kuiongoza nchi yetu ya Tanzania.

Kutokana na hilo, Chama Cha Mapinduzi kinajivunia sana uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, na Watanzania kwa ujumla wetu tunajivunia sana kuongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwezo wake mkubwa ambao ameuonesha ndani yah ii miaka mitatu,” amesema Katibu Mkuu Balozi Dk. Nchimbi.

Dk. Nchimbi pia alitumia nafasi hiyo kuwahakikishia wajumbe kuwa kutokana na kuwa mwanamajumui wa kweli wa Afrika, Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ana dhamira ya dhati kuimarisha na kuboresha uhusiano wa nchi na vyama rafiki katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika na kwamba anafuatilia mkutano huo wa 11 wa Makatibu Wakuu wa vyama hivyo kwa ukaribu, huku pia akiwaomba wajumbe kuungana nae kumtakia kila la heri Mhe. Samia na kumuunga mkono, ombi ambalo lilipokelewa na kukubaliwa na wajumbe.

Ukiwa kiongozi wa CCM, usiposema uongo tena hadharani una hatari ya kunyang'anywa kadi ya uanachama
 
Halafu Katibu Mkuu amevaa kofia zilizopigwa marufuku na jeshi
 
Imfikie misambwanda
 
Ndani ya CCM demokrasia ni finyu sana, hivi unawezaje kujitokeza kumpinga Rais wa nchi ambaye ndiye mgombea pekee ndani ya chama chako?. Je utakuwa unajipenda ewe mwana CCM kweli.
 
Back
Top Bottom