Dkt. Nchimbi: Rais Samia anaungwa Mkono na wana CCM wote

Dr Nchimbi KM wa CCM akiongea kwenye kikao cha makatibu wakuu wa vyama rafiki wa CCM amesema namnukuu "WATANZANIA WOTE WANAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA NA WANAJIVUNIA UWEZO WAKE WA KUONGOZA NCHI", mwisho wa kunukuu.
Kauli ya Kichawa kama hii hata KUPE Lucas Mwashambwa hawezi kuitoa maana anamwogopa Mungu. Ni Mtu asiyeamini uwepo wa Mungu ndiye anayeweza kutoa kauli ya uongo na kizandiki kama hii tena akijua yeye ni kiongozi wa ngazi ya kitaifa kichama na anaongea mbele ya viongozi toka nje ya Nchi. Kwamba Leo ukiitishwa Uchaguzi wakawekwa Watanzania mil.2 tu Samia atapata Kura mil.2?
Hivi hii Tabia ya kuwaona Watanzania wote ni wajinga nyie Wenye platform za kuongea ndio Wenye akili mmeitoa wapi? Yaani KM unawapiga propaganda hata wageni toka nje ya Nchi? Itasaidia nini wakifika Namibia au Msumbiji?
Hivi ungesema Watanzania WENGI wanamuunga mkono japo nalo halina uhakika ungepungukiwa nini zaidi ya kuchuma dhambi Kwa kusema uongo mchana kweupe?
 
Hapa katibu kateleza nae ni binadamu raha ya kukalia kiti cha chama kubwa kila usemalo ni habari!
 
😂😂😂

Hii kali sana

Watanzania Wote maana yake na Mdude Nyagali yumo, Tundu Lisu yumo, Mwabukusi yumo dadeki 😂😂😂
 
Anaungwa mkono na Watanzania wote?

Huu ni mwanzo wa kuiba kura tayari!

Kauli hii inabidi ipingwe haraka sana na aombwa KM wa CCM akaifafanue vizuri mahakamani
 
Ukiwa kiongozi wa CCM, usiposema uongo tena hadharani una hatari ya kunyang'anywa kadi ya uanachama
 
Halafu Katibu Mkuu amevaa kofia zilizopigwa marufuku na jeshi
 
Imfikie misambwanda
 
 
Ndani ya CCM demokrasia ni finyu sana, hivi unawezaje kujitokeza kumpinga Rais wa nchi ambaye ndiye mgombea pekee ndani ya chama chako?. Je utakuwa unajipenda ewe mwana CCM kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…