Dkt. Ndumbaro sababu hizi hazitoshi kuhamisha FITI-Moshi

ndio wale wale walifuta michezo shuleni alafu baadae wakaja kuzomewa.
Walifuta
  1. Michezo
  2. Masomo ya ufundi Iyunga, Ifunda nk
  3. Masomo ya biashara
  4. Masomo ya kilimo
  5. Masomo sanaa
Njama chafu ilikuwa ni kuajiri watu wenye fani hizo kutoka nchi jirani alikotoka Waziri wa Elimu wa wakati huo
 
Wapi. Zama zimechenji mzee zama za kurundika taasisi za umma Moshi zimeisha. Sasa ni zama za even development. Njombe inaongoza kwa mistu East Africa lakini wajanja wakapeleka chuo kwao.
Hicho chuo umeambiwa kimeanzishwa mwaka 1975 kwahiyo lazima kuna vigezo vilitumika tofauti na hapo ni hisia zako.na sasa kama wewe unaona njombe kuna msitu mkubwa anzisheni cha kwenu uko njombe sio kuhamisha kilichoko.Hoja yako haina maana zaidi ya ubadhirifu wa fedha.
 
Sioni jambo baya. Majengo ya hicho chuo bado yatabaki na pengine kugeuzwa kuwa chuo chenye manufaa zaidi.
Mkoa wa Iringa na Njombe ni sehemu hot sana kwa mambo yq misitu. Si mbaya uamuzi huo.
 
Kuna mikoa haina taasisi ya umma hata mmoja. Sasa mikoa iliyorundikiwa taasisi itulie kwanza.
Hiyo siyo sababu ya kuhamisha. Wajenge hizo taasisi na huko ambako hakuna. Watu si wanaongezeka.
 
Aisee kudumu kwake basi ni ngekewa na huo umafya wake una msaidia hafu ana kakimbele front flani hivi loh.
Nakumbuka send off ya Binti yake ili rushwa tbc Yani alikuwa hatulii kama mama wa Bibi harusi full kuhangaika humo ukumbini.
 
Kwa hiyo unaona sawa mikoa mingine kutokua na taasisi za umma. Chuo Cha Wanyamapori Ushirika, FITI na makumi zaidi Moshi. Mikoa mingine inachekwa tu.
Wewe hujielewi kwahyo kukitoa Moshi ndo kutafanya huko kwingine kupige hatua, acha wivu wa kijinga badala muongeze vyuo viwe vingi zaidi kikanda nyie mnawaza kupunguza maendeleo mazuri yanatakiwa yawe kote sio kunyang'anya hichi peleka kule
 
Wapi. Zama zimechenji mzee zama za kurundika taasisi za umma Moshi zimeisha. Sasa ni zama za even development. Njombe inaongoza kwa mistu East Africa lakini wajanja wakapeleka chuo kwao.
Dah wewe una akili za kijiwe jiwe hivi loh
 
Wewe hujielewi kwahyo kukitoa Moshi ndo kutafanya huko kwingine kupige hatua, acha wivu wa kijinga badala muongeze vyuo viwe vingi zaidi kikanda nyie mnawaza kupunguza maendeleo mazuri yanatakiwa yawe kote sio kunyang'anya hichi peleka kule
Tulia wewe. Serikali imeona hakuna hitaji la kupanua chuo husika kwa Sasa bali kurelocate period.
 
Kwahiyo na vyuo vya wanyamapori kama pasiansi na mweka vilivyoko chini ya hiyo wizara vihamie serengeti.Punguza uzwazwa.Msitu unaweza kuanzishwa popote penye ardhi.
Hicho kimkoa hakuna ardhi,vyuo viende kwenye utalii
 
Kabisa, unajua sometimes unawaza yani hata Rais Samia akifukuza hawa mawaziri atafukuza wangapi?
Unajua mtu sijui anawaza wapi?
Its like useme Dar kuna viwanja vingi vya mpira kwahiyo kile cha Karume pale ilala kifungwe kihamishiwe Dodoma, what a nonsense?
 
Nchi hii bado ujinga wa jp unawasumbua. Ila basi chuo cha Moshi kibadilishwe makusudi yake iwe bora zaidi kwa manufaa makubwa zaidi ya wananchi kuna watu wana upeo mdogo badala ya kuboresha chuo wanakihamisha!
Hicho chuo moshi kimejengwa kwa msaada wa SIDA/DANIDa, wa Denmark, kina wazungu wameweka mashine na mitambo toka 1975 na inafanya kazi mpaka leo, anakuja mtu na tope kichwani eti tuhamishe, na kipo pembezoni mwa reli ya Moshi -Dar kwaajili ya kusafirisha magogo na mazao mengine, sasa sijui huyu Ndumbaro anawaza kitu gani, kwakweli .
 
Mkuu PTER , kwa kweli kuna mengi sana ya kushangaa,lakini kwa kweli tumechoka kushangaa.
Yaani hayo mambo hapo juu uliyoyaorodhesha,yangesemwa na mbunge msukuma,kibajaji au vijana wa Lumumba (hawa hutolewa ubongo kabla ya kupewa kadi),tusingeshangaaa.
 
Ni wapuuzi wachache wanaofikiri kama mwendazake kwamba Moshi imeendelea sana na haihitaji maendeleo tena!
 
Huyo ndio aliyeua elimu bongo Wala tusitafute mchawi
Mchawi wa elimu bongo sio Mungai pekee.
Mchawi aliyeua elimu ya Tanzania ni CCM.
Kama ilivyo kwa mtaji wa masikini kuwa nguvu zake mwenyewe,ndivyo ilivyo kwa mtaji wa CCM kuendela kuwepo madarakani ni elimu duni wanayopata watoto wa Kitanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…