TANZIA Dkt. Peter Mamiro afariki dunia zikiwa zimepita siku mbili tokea mkewe(Prof. Delphina Mamiro) afariki dunia

TANZIA Dkt. Peter Mamiro afariki dunia zikiwa zimepita siku mbili tokea mkewe(Prof. Delphina Mamiro) afariki dunia

Mh Kikwete hakukosea aliposemaga "Akili za kuambiwa changanya na zako". Usisubiri serikali ikuaminishe kuwa ugonjwa upo au haupo. Jilinde jikinge na uwakinge na wenzako. Vaa barakoa (after all unajikinga na vumbi, TB pia; Nawa mikono kwa sabuni, si ni usafi tulifundishwaga toka shuleni?; paka sanitizers kwa usalama tu)
 
pole kwa familia.au ndo hiz chanjo wanazokimbilia!!hiz chanjo badala ya kuleta faraja,Sasa zimegeuka msiba.
Wa Brazil ilibidi waombe poo. Ni baada ya kuibeza Corona.

Hata kama tukiionea aibu kuitamka jina. Corona ipo na inaua kinyama .
 
Muda wowote kuanzia kesho tutalajie kusikia mzeebaba akifanyia kazi kutoke kijijini Chato maana hii variant ya Africa kusini haina utani kabisa
Hii new strain from South Africa c mchezo, ndio inayotutafuna sasa.
 
Tatizo humu hatujuani. Nilitaka nikutukane bonge la tusi lakini nikaogopa isije ikawa namtukana jiwe nikajikuta natafutwa kwa gharama yoyote. Ila mkuu sio poa, unataka kutuambia chanzo ya covid 19 inaua?
Watu wnafanya masihara ila mkuu we poteza
Tu anaye bisha acha abishe

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Kama hatua hazichukuliwi maana yake virus vinakuwa free tu na bila kujulikana. hapo ndipo strains hatari zinaweza kutokea. Dunia itatutenga. Maana haiwezekani wazalishe chanjo kwa kazi halafu huku tutoe strain mpya isiyosikia chanjo. Mtu wa hivyo hata kichapo anaweza pewa.
 
hizi habari mnazipenda kuziweka jf sijui mna tatizo gani siku hizi
 
watu wanakohoa sana...mafua ndio usiseme huu ugonjwa unazurura tu mtaani,mahospitali ndio usiseme.
poleni sana wafiwa kwa kuondokewa na wapendwa kwa muda mfupi mola awape nguvu na subira.
 
Naona huyu wa SA wala haanzi na dalili za mafua na homa tena.

Tunakoelekea kila familia itajikuta ina mtu wa karibu inayemfahamu ambaye amefariki kwa "pneumonia" na hapo ndipo watu watarudi kwenye uhalisia wa kuchukua precautions bila kusubiri mtu.

Chukueni precautions mazee!
 
Habari mbaya ya kusikitisha ni kuwa Dkt. Peter Mamiro amefariki dunia usiku wa kuamkia leo mkoani Morogoro ikiwa zimepita siku mbili tokea mkewe, Profesa Delphina Mamiro afariki dunia. Dkt. Peter Mamiro na Profesa Delphina Mamiro walikuwa wanafundisha Chuo cha Kilimo Sokoine - SUA.

Habari za kuaminika kutoka kwa ndugu wa karibu zinasema kwamba siku chache zilizopita, Dkt. Peter na Profesa Delphina walitoka Kilimanjaro kuwazika wazazi wawili (Mchungaji Kessy na mkewe) wa Profesa Delphina ambao nao vifo vyao vilifuatana.

Inadaiwa baada ya kurudi Morogoro hali ikuwa mbaya mpaka umauti unawakuta.

Mwenyezi Mungu aipe nguvu na faraja familia hii inayopitia majaribu haya yote.

Pia soma TANZIA - Profesa Delphina Mamiro wa Chuo Kikuu cha Kilimo(SUA) afariki dunia

"Mabeberu wanatuonea wivu sisi ni matajiri. Sasa wameanza kuturoga, mnaona?" alimaka yule mfalme maarufu wa ma-Zinjanthropus.

Sisi na tuseme "BWANA aliyetoa tangu awali ndiye anayetwaa sasa. Jina lake libarikiwe. AMEN"
 
Aiseee. Mungu atulinde jamani. Hali imekuwa tete sana jamani. Bila shaka yule saizi yupo happy anashushia na kapepsi barid akiona wananchi wake tunateseka[emoji25][emoji25][emoji25]
SASA MNATAKA NINI KIFANYIKE?? TUSIBAKI TUNA TOA LAWAMA ZISIZO KUWA NA MASHIKO. KILA MARA TUMESHATAHADHALISHWA TUCHUKUE TAHADHARI KWA MAAMBUKIZI KWA KUWA TZ SIYO KISIWA. AU UNATAKA SERIKALI ISEME KUANZIA LEO KILA RAIA ABAKI KWAKE TUTAWALETEA MKATE WA KILA SIKU KWENYE MLANGO?? SEMA UNA TAKA NINI KIFANYIKE??? NYUMBU WEWE.
 
Back
Top Bottom