Dkt. Philip Mpango: Narudi kuchapa kazi, Mungu amenivusha. Leo siku ya 3 sijatumia mtungi wa Oxygen

Dkt. Philip Mpango: Narudi kuchapa kazi, Mungu amenivusha. Leo siku ya 3 sijatumia mtungi wa Oxygen

Mwambie barakoa ni muhimu asije akatuletea balaa jingine!

Hatari sana, hivi Kwa Maelekezo ya Wizara ya Afya, huyu bwana alikuwa sahihi kuongea vile na kikohozi bila barakoa? Pembeni akiwa na wape jamaa wawili nao bila barakoa za kutengenezwa MSD?
 
Amezungumza na waandishi wa habari akiwa hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma leo tarehe 23 Febr 2021, live kupitia TBC.

Amesema alikuja hapo hospitalini akiwa na mtungi wa Oxygen. Amekuwapo kwa zaidi ya wiki mbili. Na leo ni siku ya 3 hajagusa mtungi wa Oxygen, anapumua mwenyewe.

Tunafurahi sana kuona amepona.

Binafsi nafurahi zaidi kwa ushuhuda wake wa kwamba amepona kwa tiba rasmi za hospitali, na si kwa mambo ya kujifukiza na kupiga nyungu. Huu ni ushuhuda kwamba hizi ndizo huduma tunazopaswa kuzieneza kwa wote na kuhimiza wananchi wazitumie, na siyo kutupoteza kwa mambo ya nyungu.

Amesifu excellent professionalism ya madaktari wetu. Naomba ujumbe huu uwafikie wale wanasiasa wote wanaobeza madaktari wetu na kuwadhalilisha, na ujumbe uwafikie pia wale wanaohimiza uganga wa jadi. Mheshimiwa amekiri kuwa hii sekta inastahili kupewa kipaumbele zaidi.
Uchambuzi murua
 
Jamani dakika 20 tu zimepita nimepata taarifa za msiba. Na umri ni 35. Aliumwa na akapata nafuu lkn ghafla hali ilibadilika na ameaga dunia leo. COVID-19 variant ni unpredictable na inachukua aspect tofauti kwa kila anayeipata. Watoto tu ndio inafahamika symptoms sio severe lakini very good carriers of the C-19.
Pole sana bibie, mimi mepoteza ndugu last two weeks
 
Bado unaumwa DR.. tusidanganyane !! usifanye mchezo na Covido - bado game hujalimaliza rudi kitandani fasta upate 0xgn watanzania wanakuhitaji.
 
Hatari sana, hivi Kwa Maelekezo ya Wizara ya Afya, huyu bwana alikuwa sahihi kuongea vile na kikohozi bila barakoa? Pembeni akiwa na wape jamaa wawili nao bila barakoa za kutengenezwa MSD?
Ajabu na hao wawili mmoja ni mkurugenzi wa hiyo hospitali ya Benjamin Mkapa?
 
Nadhan sasa dokta atakuwa amepata fundisho, kutovaa barakoa kwake lilikuwa ni kosa kubwa sana kwake, siku nyingine asikubali kudanganywa......
 
Ukweli, alikuwa anaumwa na wengine wamekufa - ni mpango wa mwenyezi Mungu tu; si kwamba yeye aliomba sana kuliko wengine au alipata huduma za ziada kuliko wengine!
Hivi gharama ya kulazwa wiki 2 ni sh ngapi? na bado unatoka ukiwa dhaifu! Chanjo je ni bei gani? maana wahenga walisema kinga ni bora kuliko tiba
 
Back
Top Bottom