TANZIA Dkt. Shogo Mlozi, Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki afariki dunia

Haya maelezo yako hakuna sehemu yameonyesha elimu haina maana.

Ukipata yanayoelezea upuuzi wa elimu ukaungana na ngumbaru wenzako niite.
Wapi nimesema Elimu haina maana kwenye maelezo yangu.
Kila kitu kina umuhimu wake.
Ila kipaji kina lipa zaidi ya elimu ndugu kwa sababu under Ceteris paribus, kila mtu anaweza kusoma kupata elimu ila kila mtu hawezi kuwa na kipaji fulani
 
Na majina ya wazazi wao yamewabeba. Ni wangapi wana masters na hizo PhD wako mtaani wanafanya Yao kimya kimya hawaonekani kwenye hizo nafasi??
Tanzania upendeleo una nafasi kubwa sana kuliko kile unchojua
Yeye ana impact Kwa jamii Hadi alikuwa na foundation ya kusaidia watu hadharani hao wanaofanya mambo Yao kimya kimya wanafanya Nini uchawi kukaba watu usiku au ?
 
Wapi nimesema Elimu haina maana kwenye maelezo yangu.
Kila kitu kina umuhimu wake.
Ila kipaji kina lipa zaidi ya elimu ndugu kwa sababu under Ceteris paribus, kila mtu anaweza kusoma kupata elimu ila kila mtu hawezi kuwa na kipaji fulani
Anzia kwenye comment yangu nimewaita wanaodai elimu haina maana waje wajionee.

Wanionyeshe familia ambayo baba ni msanii kafanikiwa, mama ni muigizaji kafanikiwa, mtoto mmoja yuko bongo fleva na mwingine yuko timu ya ligi kuu kama hii familia ilivyofanikiwa kwa elimu tu.
 
Alipataje huo ukuu wa Chuo?
.
1. Nafasi ilitangazwa wazi? Kwenye magazetti? Lipi? La lini?

2. Wali-apply wangapi? Shortlisted? Invited for interview? Interview scores? Panelists walikua wakina nani?

3. Nani alishinda interview? Scores zao?
Naomba tutumie u Afrika wetu na Utanzania wetu kutomsema vibaya marehemu.

Please let her rest in peace.
P
 
Dah wew jamaa mbishi sana huyu binti marehemu huwezi kusema katoka kwenye familia ya wasomi saanaa.
Baba yake kweli msomi kwelikweli Professor huyu mtoto hadi anazaliwa mama yake Queen Mlozi alikuwa ni mwalimu wa primary.
Huyu mama yake marehemu degree yake kaipata kupitia mature age entry na aliweza kufaulu kupitia kujuana kati ya Mume wake akiwa professor sua na wakufunzi wa mzumbe aliposomea degree huyo mama yake marehemu.
Huyu mama zen akafluck fluck huko ccm akahonga na kupewa u dc baadae akawa katibu mkuu uwt.
Suala la kufanikiwa mtu kimaisha na masuala ya elimu are not directly proportion.
Kuna watu kibao nawajua mimi wazazi wao hawana elimu yeyote ila wamefanikiwa kupita watu wengi wenye elimu zao na Kuna watu wazazi wao ni wasomi na elimu zao kubwa ila hawana lolote la kujivunia.
Kwa hiyo ndugu kwa karne hii kufanikiwa ki maisha hakutegemei sana elimu ya darasani.
Mimi hapa mwenyewe nina degree 3 bachelor 1 na masters 2 tofauti ila kimafanikio ya kimaisha nakiri Dimondplatnumz aliyefeli form 4 wakati mimi nina division 1 amenizidi kimafanikio ya kimaisha huyo dimond
 
Pole paskali kwa kuondokewa na mdau wako.

Poleni ndugu ,jamaa na marafiki..

M.A.P Dr Shogo.
 
Yeye ana impact Kwa jamii Hadi alikuwa na foundation ya kusaidia watu hadharani hao wanaofanya mambo Yao kimya kimya wanafanya Nini uchawi kukaba watu usiku au ?
Bila kujua ushike wapi hiyo NGO Itafika wapi?? As if huelewi mifumo ya nchi hii. Wengi waliokuwa wanasapot hyo NGO yake wengi ni wabunge... Nenda instagram uangalie alafu urudi uandike tena.
Technical know who badala ya know how Ina matter sana nchi hii.
Marehemu hasemwi ngoja tumuache akapambane na alichochagua
 
R.I.P
Duniani tunapita tu kila mmoja ataondoka kwa wakati wake haijalishi ni tajiri au masikini 👁
R.I.P Dr
Poleni sana wafiwa Mungu awape subira na nguvu 🙏🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…