Dkt. Slaa adaiwa kubadilishiwa mashtaka kutoka ya uchochezi na kuwa ya uhaini

Dkt. Slaa adaiwa kubadilishiwa mashtaka kutoka ya uchochezi na kuwa ya uhaini

Hawa kunguni wanajiona miungu mtu wakikosolewa wanakuuzia kesi ya uhaini, zero respect kwa huyu mama sasa
Kwani unafahamu kwanza uhaini ni nini? Kwa nini unadhani Dr Slaa hajafanya uhaini? Nakuletea bandiko hapa
 
Attachments

  • 20230814_062711.png
    20230814_062711.png
    19.4 KB · Views: 3
Ameandika kwenye account yake ya mtandao wa twitter:

Usiku huu, Dkt. Wilbroad Peter Slaa, mashtaka yake yamebadilishwa kutoka katika matumizi ya lugha ya uchochezi sasa amepewa mashtaka ya UHAINI. Dkt. Wilbroad Slaa yupo kituo cha polisi Oysterbay. Taarifa hii ni kutoka kwa wakili wake, Adv. Dickson Matata. Anakuwa mtu wa tatu.
Sijapenda ila wanastahili. Mama alisema wazi yuko tayari kukosolewa na kushauriwa ili kujenga Taifa lenye amani, umoja na mshikamano. Hata hivyo ukosoaji huo ufanyike kwa maana ya kukosoa sio kutukana wala kukosoa au kutishia watu. Bahati mbaya kuna watu hawajapenda hali hiyo. Wacha dola ifanye kazi yake.
 
Kipenzi chenu kimetoa bandari zetu zote milele kwa wajomba zake, halafu kwa mawazo yako ya kitumwa bado unamuita kipenzi? huoni kama anawapenda waarabu zaidi ya anavyokupenda wewe?

Mjinga.
Wewe ni kati ya wapotoshaji wakuu. Ni lini bandari zimetolewa milele? Mbona wajomba wa Samia wako Oman na siyo Dubai? Huu upotoshaji ndiyo unawa cost viherehere wenzio.

Na ungekuwa unatumia verified ID na wewe ungeunganishwa na akina Slaa
 
Wakati wa Mwendazake, watu walipiga kelele Mungu akajibu kwa namna yake. Umepewa nafasi na Mungu huyo, huyo, sasa unafanya kinyume . Haya endelea tuone na wewe utafika wapi unless wewe ni bora sana .
Anakuaje kizuizini na kuwa na mawasiliano?
Hilo ni kosa kubwa wanafanya hao askari

Wamuhifadhie tu hayo mawasiliano yake mpaka atakapokuwa huru tena
 
Ameandika kwenye account yake ya mtandao wa twitter:

Usiku huu, Dkt. Wilbroad Peter Slaa, mashtaka yake yamebadilishwa kutoka katika matumizi ya lugha ya uchochezi sasa amepewa mashtaka ya UHAINI. Dkt. Wilbroad Slaa yupo kituo cha polisi Oysterbay. Taarifa hii ni kutoka kwa wakili wake, Adv. Dickson Matata. Anakuwa mtu wa tatu.
Ina maana ameshasomew shitaka lake kabla ya kwenda mahakamani?
 
Huyu mama kachukia sana. ana dili za wizi nyingi na waarabu , sasa hii moja imevuja na watu wameishikia bango, ile ya ngorongoro watu walipiga kimnya...pia kapoteza mvuto kwa kasi ya 5G.. Hapo anafikiri dili za wizi zilizobaki na waarabu zitakuweje? Mwisho wa siku anatoa maamuzi mabovu sababu ya Hasila zake...SIKU YA KUFA NYANI ....
Wanaokwenda kufaidika na DP World pale TPA ni wafanya biashara wengi wanaoingiza pesa nyingi kwenye mzunguko wa mtaani, ni rahisi sana kwa haya maneno ya mkuu kitansa kutokuwa na ushawishi wowote miaka miwili ijayo wakati wa uchaguzi mkuu.
 
Ameandika kwenye account yake ya mtandao wa twitter:

Usiku huu, Dkt. Wilbroad Peter Slaa, mashtaka yake yamebadilishwa kutoka katika matumizi ya lugha ya uchochezi sasa amepewa mashtaka ya UHAINI. Dkt. Wilbroad Slaa yupo kituo cha polisi Oysterbay. Taarifa hii ni kutoka kwa wakili wake, Adv. Dickson Matata. Anakuwa mtu wa tatu.
Huyu wakili namkumbuka kwenye kesi ya mbowe akiwa na akina kibatala

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Ameandika kwenye account yake ya mtandao wa twitter:

Usiku huu, Dkt. Wilbroad Peter Slaa, mashtaka yake yamebadilishwa kutoka katika matumizi ya lugha ya uchochezi sasa amepewa mashtaka ya UHAINI. Dkt. Wilbroad Slaa yupo kituo cha polisi Oysterbay. Taarifa hii ni kutoka kwa wakili wake, Adv. Dickson Matata. Anakuwa mtu wa tatu.
Safi sn tunaenda pazuri huyu dikteta anadhani nchi ni mali ake binafsi
 
Mama hajui kuwa hiyo yote ni movement ya kumng'oa yeye.
Atafululizishiwa matukio halafu si unajua mambo ya overweight, busy, uchovu na stress? MPANGO ni Mkakati wa kumalizia ndiyo maana akapangwa pale.
Mpaka mimi chawa nimetema damu niliyonyonya usiku kucha hahahahah, hilo jambo sijui kwa nini Mama yaani hakuliona tangu asubuhi, sijui kwa nini hana macho, walianza toka walivyotaka kumgombanisha na msukuma wa watu anayependa wanawake wenye rangi za kiarabu, yaani kwake kumuona tu Samia ilikuwa burudani tosha, alimpenda kama dada yake, wajuvi wakaingia kazini wakahakisha wanamfitinisha na hatimaya k-vant na spirit zikahusika hahaha akiingia nyumbani hahaha U makamu mwisho getini ohhhh msukuma akachoka kabisa, basi wakamtengeneza akawa mnyetishaji kigogo14 raha tupu,

ngoma hatimaye wakaudondosha mbuyu wakamtengenezea mazingira kuwa walimuokoa na wafuasi wa msukumawabaya na msukuma alikuwa mbaya si umeona hahahaha basi wakajua atawaachia wapi urais mtamu, dogo faster dubai hahaha dili dili sasa wanaona ohhh kazidi atafutiwe angle, sasa sijui nani atakuwa mshindi, ila Mama alikosea sana kujihusisha na kumdhihaki Dkt Magufuli, ina mgarimu sana maana ndiyi serikali pekee aliyopaswa kujivunia
 
Kumtuhumu Mtu kuwa ni Mwizi ni lazima utusaidie na Ushahidi wa Wizi wake maana kosa la Wizi ni Jinai. Kumtuhumu Uongo Rais wa nchi ni Kujidhalilisha Mwenyewe kwenye uso wa Dunia.
Wanasiasa badala ya kutumia Nafasi Vizuri kuviuza vyama vyenu mnaanza kutukana na Kutishia Viongozi sidhani kama ndilo lengo la Demokrasia eti kudhalilishana badala ya kuuza Sera zako.
Kwani hujawahi kusikia Rais ameiba mali ya nchi yake?
 
Sijapenda ila wanastahili. Mama alisema wazi yuko tayari kukosolewa na kushauriwa ili kujenga Taifa lenye amani, umoja na mshikamano. Hata hivyo ukosoaji huo ufanyike kwa maana ya kukosoa sio kutukana wala kukosoa au kutishia watu. Bahati mbaya kuna watu hawajapenda hali hiyo. Wacha dola ifanye kazi yake.
Kwa kuwa nia ilikuwa amani, umoja na mshikamano kama unavyosema, haya yanayofanyika yanatupelekea kwenye nia hiyo au hizo nia hazina umuhimu kuzidi staha Kwa wakubwa?
 
Back
Top Bottom