Dkt. Slaa adaiwa kubadilishiwa mashtaka kutoka ya uchochezi na kuwa ya uhaini

Dkt. Slaa adaiwa kubadilishiwa mashtaka kutoka ya uchochezi na kuwa ya uhaini

Mfalme Nebkadneza aliambiwa na Danieli aache matendo yake dhidi ya Wana wa Israeli la sivyo Atabadilika kuwa Hayawani.

Nebkadneza alikuwa na jeshi zuri lenye nguvu likiongozwa na Jemedali Mwanaye anaitwa Neboporasa.

Baadae pamoja na jopo lake la waganga, wasihiri na wenye hekima ufalme ukaanguka, mfalme akajikuta yuko nyikani anakula nyasi kama wanyama wa mwituni.

Hapa ardhi ya Nyerere kuna mtu aliambiwa atubu akawa amedharau pia.
UONGO
 
Wakati wa Mwendazake, watu walipiga kelele Mungu akajibu kwa namna yake. Umepewa nafasi na Mungu huyo, huyo, sasa unafanya kinyume . Haya endelea tuone na wewe utafika wapi unless wewe ni bora sana .
Kwa upumbavu na ujinga wako wewe unaamini kifo ni adhabu au ni hukumu ya watu waovu.una fikra mbirikimo na akili zenye matege.
 
Ameandika kwenye account yake ya mtandao wa twitter:

Usiku huu, Dkt. Wilbroad Peter Slaa, mashtaka yake yamebadilishwa kutoka katika matumizi ya lugha ya uchochezi sasa amepewa mashtaka ya UHAINI. Dkt. Wilbroad Slaa yupo kituo cha polisi Oysterbay. Taarifa hii ni kutoka kwa wakili wake, Adv. Dickson Matata. Anakuwa mtu wa tatu.
Wahaini ni serkali, wabunge na Polisi.
 
Habari kama hizi awamu iliyopita zilikuwa zinatafsiriwa hapa JF kwa ajili ya "English audience".

Nafikiri kwa sasa kuna option ya translation kwenye app ya JF au mkalimani amestaafu.

BTW:Uhaini hauna plea bargaining!
 
Ameandika kwenye account yake ya mtandao wa twitter:

Usiku huu, Dkt. Wilbroad Peter Slaa, mashtaka yake yamebadilishwa kutoka katika matumizi ya lugha ya uchochezi sasa amepewa mashtaka ya UHAINI. Dkt. Wilbroad Slaa yupo kituo cha polisi Oysterbay. Taarifa hii ni kutoka kwa wakili wake, Adv. Dickson Matata. Anakuwa mtu wa tatu.
Safi sana,huyu alikuwa Balozi wa Nchi Sasa anakiuka na kusaliti Nchi na kiapo chake.

Ashughulikiwe na wengine wa dizaini hii.
 
Ameandika kwenye account yake ya mtandao wa twitter:

Usiku huu, Dkt. Wilbroad Peter Slaa, mashtaka yake yamebadilishwa kutoka katika matumizi ya lugha ya uchochezi sasa amepewa mashtaka ya UHAINI. Dkt. Wilbroad Slaa yupo kituo cha polisi Oysterbay. Taarifa hii ni kutoka kwa wakili wake, Adv. Dickson Matata. Anakuwa mtu wa tatu.
na simu anayo anachati tu
 
Kumtuhumu Mtu kuwa ni Mwizi ni lazima utusaidie na Ushahidi wa Wizi wake maana kosa la Wizi ni Jinai. Kumtuhumu Uongo Rais wa nchi ni Kujidhalilisha Mwenyewe kwenye uso wa Dunia.
Wanasiasa badala ya kutumia Nafasi Vizuri kuviuza vyama vyenu mnaanza kutukana na Kutishia Viongozi sidhani kama ndilo lengo la Demokrasia eti kudhalilishana badala ya kuuza Sera zako.

Mkuu huu ni uhaini?
 
Mama hajui kuwa hiyo yote ni movement ya kumng'oa yeye.
Atafululizishiwa matukio halafu si unajua mambo ya overweight, busy, uchovu na stress? MPANGO ni Mkakati wa kumalizia ndiyo maana akapangwa pale.
Mimi naamini kwa Chato kabisa haya yanayoendelea siyo maagizo ya Samia.

Mama anayo nafasi ya kusimama kama Rais na kukomesha huu uhaini anaofanyiwa ndani ya mfumo wake.

Ni hakika jamaa wamedhamiria 2025 mgombea Urais asiye mama, hizi medani za kivita za kumdhoofisha na kumchonganisha umma ili anuke ubaya na wanaelekea kufanikiwa.

Usalama wa Samia ni kuamka usingizini sasa na kutoka maagizo kama amiri Jeshi mkuu.

Haiwezekani Kamwe mtu anayejitahidi kurekebisha mifumo ya haki eti hiyo huyo ndio awe mratibu wa hiki kinachoendelea, hili si kweli hata kidogo namuonea huruma sana huyu mama.

Kama angalikuwa ni mama yangu ningemshauri aongoze kipindi kimoja akae pembeni watamuuwa.

Maadui wa mama na Wahaini halisi siyo upinzani Bali wapo ndani ya Ccm na kwenye mifumo, mnapowaona kina Kassimu wapo kimyaa kama hawapo jiongezeni akili.
 
Usalama wa Samia ni kuamka usingizini sasa na kutoka maagizo kama amiri Jeshi mkuu.

Haiwezekani Kamwe mtu anayejitahidi kurekebisha mifumo ya haki eti hiyo huyo ndio awe mratibu wa hiki kinachoendelea, hili si kweli hata kidogo namuonea huruma sana huyu mama.
Hata mimi nimelishtukia sana hili.

Na kuna mawakala wa uovu wamevamia jukwaa humu wako kama nyoka. Yaani maneno yao ukiyasikia kwanza hawakuwepo kipindi chote cha mjadala wameibuka na ID mpya au ID zilizokuwa domant tangu juzi kutangazwa Uhaini hewa.
 
Mateso wanayopewa hawa wazalendo na serikali ya ccm ni ya muda mfupi sana.
Mwenyezi Mungu hachezewi na kukandamiza wengine kutokana na ukweli wao ni DHAMBI kubwa sana.
Watambue kuwa kama ni UHAINI walioingia mkataba wa DPW ndio WAHAINI.
 
Kwa kuwa nia ilikuwa amani, umoja na mshikamano kama unavyosema, haya yanayofanyika yanatupelekea kwenye nia hiyo au hizo nia hazina umuhimu kuzidi staha Kwa wakubwa?
Violation cum retaliation
 
Mateso wanayopewa hawa wazalendo na serikali ya ccm ni ya muda mfupi sana.
Mwenyezi Mungu hachezewi na kukandamiza wengine kutokana na ukweli wao ni DHAMBI kubwa sana.
Watambue kuwa kama ni UHAINI walioingia mkataba wa DPW ndio WAHAINI.
Ameeni ameen. Mungu wetu wa Ibrahim Isaka na Yakobo atatwnda miujiza hajawahi kushindwa.
 
Kumtuhumu Mtu kuwa ni Mwizi ni lazima utusaidie na Ushahidi wa Wizi wake maana kosa la Wizi ni Jinai. Kumtuhumu Uongo Rais wa nchi ni Kujidhalilisha Mwenyewe kwenye uso wa Dunia.
Wanasiasa badala ya kutumia Nafasi Vizuri kuviuza vyama vyenu mnaanza kutukana na Kutishia Viongozi sidhani kama ndilo lengo la Demokrasia eti kudhalilishana badala ya kuuza Sera zako.
Mkataba wa DP World na Sakata la wamasai Ngorongoro vinadhihirisha wizi wa Samiah.
 
Back
Top Bottom