Dkt. Slaa adaiwa kubadilishiwa mashtaka kutoka ya uchochezi na kuwa ya uhaini

Dkt. Slaa adaiwa kubadilishiwa mashtaka kutoka ya uchochezi na kuwa ya uhaini

Pia alisema kupigwa risasi kwa Tundu Lissu ni jambo la kawaida sasa wacha anyee debe aache siasa za ukigeugeu.
Siasa za kigeugeu ni kutuaminisha mtu fisadi kwa miaka 8 na kwamba apigwe mawe halafu siku moja tu mkasema mwenye ushahidi aupeleke mahakamani wakati miaka yote 8 mkisema nyie mnao.

By the way, kumbe hii yote ni siasa tu? Mimi nilidhani mnaungana na kila anayepinga vipengele vibovu vya mkataba. Kumbe mnaunga mkono kasema nani na wala si hoja...

Safari ya Mtanzania bado ndefu
 
Huyu atatoka baada ya miaka 8 gerezani tupo hapa. Uhaini siyo kesi ndogo ni kujaribu kumpindua rais aliyepo madarakani.
 
Kwani lazima aende CDM au ACT tu....
Slaa tayari ni brand inayojitemea na hata akiungana na Umoja Party bado itapeta tu.
Siasa za nchi zinaangalia brand ya mwanasiasa zaidi na sio hawa wanaotembea wakigombana na Magufuli mpaka leo.
Na hilo linawakosti bila kujua
 
Au nawe ulikuwa unaona Tundu Lissu kupigwa mvua ya risasi ni jambo la kawaida
Kama kwa sasa kwako hiyo ni topic muhimu kuliko kilichowaweka ndani mdude, slaa, na mwambukusi basi endelea kujadili hilo.
 
Hatimaye dr.slaa ameswekwa lupango kutokana na harakat zake za kisiasa

Dr. alishafanya majaribio kadhaa ili kujibrand lkn naamin hili litampaisha zaid na litamwezesha awe kinara ktk vichwa vya habar na hiyo itamfanya aonekane shujaa mpaka pale kesi itakapotamatika

Swali linalotesa watu wengi ni je akimaliza kesi yake ambayo bila shaka itafutwa kabla ya kufika kwenye hukumu atajiunga na chama gan???

Baadh ya wajuz wa mambo wa hapa karume mchikichin wanaamin hatojiunga na cdm ila kuna uwezekano mkubwa akajiunga na act ili kuendelea kuidumaza cdm

Na kwa mujibu wa wajuz wa mambo wanaamin haya yote yanaratibiwa na wananzengo ili uratibu wao wa 25 uende km wanavyotaka

Wajuz wa mambo walimalizia kwa kusema kuwa di pi[emoji289] huo ni mtego uliowekwa na wananzengo na kwa bakhti mbaya bibie na timu yake waliuingia mazima
Huyu ndiye Fitna namba moja hapa Tanzania. Na hii ni tabia aliyozaliwa nayo ndiyo maana alishindwa kazi ya kanisa.
 
Kama kwa sasa kwako hiyo ni topic muhimu kuliko kilichowaweka ndani mdude, slaa, na mwambukusi basi endelea kujadili hilo.
Sijamuongelea Mdude wala Mwambukusi nimekiongelea hichi kigagula kilichomtosa shujaa wangu Tundu Lissu alipokuwa katika hali ngumu
 
Tamthiliya za dipi weldi zimeingia ukurasa mpya nao ni kesi baada ya kesi...
 
Hatimaye dr.slaa ameswekwa lupango kutokana na harakat zake za kisiasa

Dr. alishafanya majaribio kadhaa ili kujibrand lkn naamin hili litampaisha zaid na litamwezesha awe kinara ktk vichwa vya habar na hiyo itamfanya aonekane shujaa mpaka pale kesi itakapotamatika

Swali linalotesa watu wengi ni je akimaliza kesi yake ambayo bila shaka itafutwa kabla ya kufika kwenye hukumu atajiunga na chama gan???

Baadh ya wajuz wa mambo wa hapa karume mchikichin wanaamin hatojiunga na cdm ila kuna uwezekano mkubwa akajiunga na act ili kuendelea kuidumaza cdm

Na kwa mujibu wa wajuz wa mambo wanaamin haya yote yanaratibiwa na wananzengo ili uratibu wao wa 25 uende km wanavyotaka

Wajuz wa mambo walimalizia kwa kusema kuwa di pi[emoji289] huo ni mtego uliowekwa na wananzengo na kwa bakhti mbaya bibie na timu yake waliuingia mazima
Bandari zetu zirudi kwanza kisha mengine yatafuata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Balozi Mteule na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Wilbroad Slaa amesema tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na watu ‘wasiojulikana’ ni jambo la kawaida na ameitaka jamii kuliacha Jeshi la Polisi kukamilisha upelelezi na kutoa majibu.

Dkt. Slaa ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa na kituo cha runinga cha Clouds juu ya hali ya kisiasa ya Tanzania na mustakabali wa maisha yake baada ya kuondoka CHADEMA, amesema hafurahishwi na baadhi ya watu kuwataja hadharani watuhumiwa wa tukio hilo kwasababu linaharibu uchunguzi wa polisi.

“Mimi kinachoniudhi ni hii watu kusema hadharani kwamba kuna hiki na hiki tunasuspect (tunahisi) waliofanya ni fulani. Sheria inasema ukihisi nenda polisi katoe taarifa sio unaenda kwenye vyombo vya habari”, amesema Dkt. Slaa.

Amesema hawezi kuzungumzia kwa undani suala la Lissu kupigwa risasi, ikizingatiwa kuwa watu wengi wamepigwa risasi nchini na kazi ya kuwabaini wahalifu waliomshambulia ni ya polisi sio viongozi wa siasa au wananchi.

“Lakini kama binadamu hakuna anayependa binadamu yeyote aumizwe lakini matukio haya ya kuumizwa yametokea nchi hii kwa watu wengi sana. Na mimi sio chombo cha dola kujua kwamba unanyoosha kidole kwa kitu ambacho hatukiamini; mimi ni msomi”, amesema Dkt. Slaa na kuongeza kuwa,

“Ukitoa taarifa za upelelezi unaharibu upelelezi. Mimi niko Canada mauaji yapo kila siku na watu wanapotea, wanapigwa risasi wakiulizwa polisi wanakwambia suala hilo liko kwenye upelelezi tukifikia hatua nzuri tutatoa taarifa”.
 
Ujanja wenu ni humu humu mitandaoni, huko mitaani ni waoga kama mbwa koko tui.
Endelea sasa kufikiri hivyo hivyo, huku ukisubiri kiyama kije kukuzoa wewe na takataka nyingine zinazokuleta humu JF.

Hamna pa kutokea tena, mmekwishajiweka kitanzi wenyewe.

Hopeless Kabisa.
 
Sisi wafuasi wa Magufuli tuko na porp corn zetu tu hapa tunacheck hii movie. Maana tuliambiwa boss wetu ndio alikua Rais muovu kuliko wote duniani na huyu aliyeingia ni Chaguo la Mungu.
Zamu ya chiba now
 
Huyu mama kachukia sana. ana dili nyingi na waarabu , sasa hii moja imevuja na watu wameishikia bango, ile ya ngorongoro watu walipiga kimnya.

Pia kapoteza mvuto kwa kasi ya 5G.. Hapo anafikiri dili zilizobaki na waarabu zitakuweje? Mwisho wa siku anatoa maamuzi mabovu sababu ya Hasila zake...SIKU YA KUFA NYANI ....
Umeona mbali! Ukitaka vita na nyoka mshike mkia wake.
 
Hayo makosa, yanaitwa fabricated, wahuni wanayafanya kwa malengo maalum, hapo wanajua kabisa hawana ushahidi wa kuthibitisha madai yao, watakachofanya ni kuwapeleka watuhumiwa mahakamani, then kila siku iwe ile habari yao ya bado uchunguzi unaendelea...

Watuhumiwa wanarudishwa rumande, wakipelekwa mahakamani tena tarehe nyingine, itakuwa hivyo hivyo uchunguzi unaendelea, wanafanya hivyo kwasababu wanajua hilo kosa halina dhamana, ndio maana wakabadilisha kutoka uchochezi, na kupeleka kwenye uhaini.
Yeah Lengo ni kuwapotezea muda tu ili baadae wakitoka watakuta mambo yote yameshaisha.
 
Endelea sasa kufikiri hivyo hivyo, huku ukisubiri kiyama kije kukuzoa wewe na takataka nyingine zinazokuleta humu JF.

Hamna pa kutokea tena, mmekwishajiweka kitanzi wenyewe.

Hopeless Kabisa.
Huko nje wanaotamba ni polisi na landrover lao, hakuna shujaa wa nyuma wa keyboard wa aina ya Kalamu hata mmoja, mara ya mwisho walimsakizia binti mmoja mdogo akakamatwa na sijui kesi yake iliishaje.

Kina Kalamu ujanja wao ni kwenye podcast tu, huko ataita wanasheria kutoka Kenya na ataita wabunge wepesi kama yule dada Catherine wa Arusha mjini ili ajenge hoja nyepesi ya kumkataa mwekezaji DPW.

Ujinga na uswahili ndio silaha ya wanaharakati wengi tulionao. Bandari ya Antwerp inaendeshwa na DP World.

Bandari ya London na Southampton zinaendeshwa na hao waarabu. Halafu mpuuzi mmoja anakwambia mwarabu anataka kuichukua Tanzania kupitia bandari yetu!. Kwanini asiinunue Belgium na UK aje kuinunua Tanzania yetu?. Tujiongeze vichwani ili hawa mawakala wa wapigaji kina Kalamu wakose kabisa hoja.
 
Back
Top Bottom