Dkt. Slaa Afuatiliwa na watu wasiojulikana kutoka Iringa hadi Dar Es Salaam

Nasikitika ujinga kama huu kuandikwa kwenye mtandao wa kijamii unao ongoza hapa Tanzania! Propaganda za kijinga kama hizi zina shusha hadhi ya JF
 
Naona kwa sababu Dk Slaa aliwachana sana TISS Pamoja na ikulu kwa ujumla, pale kwenye mkutano mkubwa wa hadhara Mbeya.
Mkuu, TISS na vyombo vya dola hawafanyi michezo ya kitoto hivyo. Wamfuatilie kwa malengo gani. Kama lengo ni kutaka kumdhuru, iweje wasitekeleze mpango huo kwenye zile anga za kutoka iringa hadi morogoro kwenye milima ya uluguru na kule kitonga. Acheni propaganda za kipumbavu.
 
Nasikitika ujinga kama huu kuandikwa kwenye mtandao wa kijamii unao ongoza hapa Tanzania! Propaganda za kijinga kama hizi zina shusha hadhi ya JF
Mkuu, kitendo cha uzi kama huu kuwekwa hapa ni dhahiri kuwa kuna malengo maalum. Si unajua hawa jamaa walivyokamatika sasa.
 
Atongwele,

tafadhali usilete upotoshaji hapa.Hapa tunaongelea uhai wa watu.Utani huu haustahili sehemu hii peleka sehemu husika
 
Last edited by a moderator:
Ndiyo gari hilo hilo waliloamuwa kulipiga picha?
 
Atongwele,

tafadhali usilete upotoshaji hapa.Hapa tunaongelea uhai wa watu.Utani huu haustahili sehemu hii peleka sehemu husika
Confederate Spy:
Tafadhali usiwe mjinga hadi ukaaminisha watu kuwa una amini propaganda rahisi kama hizi!
 
Last edited by a moderator:

Verified ID?Ni mambo mangapi yameletwa hapa kwa ID hizi hizi kuanzia EPA hadi RICHMOND na kuwa chanzo kikuu cha habari.Masharti na kanuni za JF zimezingatiwa.Tafadhali usituondoe kwenye mijadala
 
Mkuu, kitendo cha uzi kama huu kuwekwa hapa ni dhahiri kuwa kuna malengo maalum. Si unajua hawa jamaa walivyokamatika sasa.

Great Minds discuss Ideas,medium minds discuss events,small minds discuss people!
 
Funny how people who just joined the forum (Jan - April 2013) seems to have similar arguments. Scripted ..??
Why on earth this is said to be spinning..?? Ask Mwakyembe what happened to him that year, or even ask that police constable who saw the accident and the vehicle involved, and why he was transferred immediately. Yeah, it is Nyombi, now in DCI's office.
C'mon u a...s h...les

 
TISS kufuatilia watu ni michezo ya kitoto?

Unafahamu maana ya intimidation?

Unauliza afauatiliwe kwa malengo gani,halafu hapo hapo unasema eti "kama lengo ni kumdhuru iweje wasitekeleze kwenye milima ya Kitonga",kama hufahamu lengo lao,haina maana kuwa hawakumfuatilia...
 
Verified ID?Ni mambo mangapi yameletwa hapa kwa ID hizi hizi kuanzia EPA hadi RICHMOND na kuwa chanzo kikuu cha habari.Masharti na kanuni za JF zimezingatiwa.Tafadhali usituondoe kwenye mijadala

Kuondolewa kwenye mjadala maana yake nini?

Dr. Slaa anapenda sana kujibu habari za udaku hapa JF. Kwanini asije kuthibitisha hii habari in person?

Story za kutekwa siku hizi zimekuwa deal la kupata umaarufu!!!
 
Hapo watu walikuwa wanasubiri simu ya kupewa go ahead baaasi mambo yamalizwe du mwaka huu tutang'olewa kucha mpaka ukombozi utapokuja tutakuwa tumekwisha...any way hata musa hakufika nchi ya ahadi.....
 
CDM mnafanya mambo ya hatari na kujiweka hatarini na kuwaweka viongozi hatarini. Mmegundua kuwa kuna gari linawafuata halafu mnafanya nini?

a. Mnategeana na gari (mnalipita linawapita) wenyewe mnasema "Walichukulia kama vile ni mchezo wa kawaida hadi walipofika Morogoro na kushtuka zaidi na kuanza kuchukua tahadhari kwa kunakili namba ya gari hilo" Really? Mchezo wa kawaida barabarani? grrrrrrrrr!!!!!!

b. Mnachukua namba ya gari ambalo limekuja nyuma yenu (kwanza gari hadi linaingia nyuma ya gari ya Katibu Mkuu ni kashfa ndan yake..)!

c. Mkaenda na hilo gari halafu "Walipofika kibaha ilibidi watoe taarifa kwa askari wa usalama barabarani."

Yaani, mna usahaulifu hivyo? Hawa hawa Polisi waliomkamata Mbunge Lema jana usiku; hawa hawa waliowapiga virugungu, hawa hawa... mnawapelekea haya haya mkitumaini kuwa wataikamata ile gari? Halafu wakikuta ni watumishi wenzao wa serikali (TISS au secret branch) mnatarajia watawafanya nini?


Ndugu zangu, mnatutisha... Yaani, mikakati yenu yote ya counter-intelligence mlichofanya ni hicho? haya bana...
 
Hiyo gari naifahamu, ni ya manyigu. Ila inawezekana haikuwa na nia mbaya. Inawezekana ilikuwa na assignment ya kuhakikisha dr slaa anafika safari yake salama. Nadhani ingekuwa jambo la busara kufanya uchunguzi kujua nia ilikuwa ni nini kabla ya ku judge.
 
Pole sana Kiongozi wangu (Dr.Slaa) pamoja na Maofisa wa chama mliokuwa nao ktk safari hiyo.Ni wazi na ni Dhahiri kuwa Serikali Dhaifu na Dhalimu ya CCM imeshakabwa pabaya na viongozi wote wa CCM wameshakabwa koo hawapumui badala yake kila kukicha TISS imebaki kuwa chombo maalumu cha kupanga mikakati maalumu kwa watu maalumu kwa kuagizwa na Watu maalumu(Magambazi).Nawaasa tu Magamba kwa kushirikiana na maofisa wake qakubali yaishe kwani wao ndo walijisahau na kuwageuza wananchi kuwa shamba la bibi kwa kushindwa kutekeleza Ilana na ahadi za ccm badala ya kuulizana wenyewe ni wapi wameshindwa sasa wanafikiri njia sahihi ni kudhuru viongozi na wanaharakati wa CDM.Dola wajue kuwa wanachokifanya wakilenga kuihujumu CDM ni sawa na mtu anayezuia Mafuriko kwa kutumia matope au Nyavu.Vile vile ni sawa anayezipa shimo la panya kwa kutumia mkate akiamini panya atashindwa kuingia.Watanzania wenzangu pamoja na Vikwazo hivi hakika TUTASHINDA.CDM KUKUBARIKA KWA WANANCHI NI MPANGO WA MUNGU NA MABADILIKO TUNAYOYATALAJIA NI MPANGO WA MUNGU WA MUNGU HAKUNA WA KUZUIA MPANGO WA MUNGU HATA ATUMIE RISASI WALA MABAVU.MUNGU IBARIKI CDM NA WATANZANIA WANAOSUBIRIA MABADILIKO.''VOTE FOR T2015CDM'' AMEN. COPY KWA Sumu,Wingu,Bungeni,My web na ZeMarcopolo.
 
Hawa ndio wanataka wapewe nchi!!!

Nchi sio kichwa cha mwendawazimu...
 
Wivu na chuki uzushi utawapeleka wapi chadema.Nani ana Muda wa kumfuatilia huyu babu .He is irrelevant mkajipange upya.mmefulia
 
Verified ID?Ni mambo mangapi yameletwa hapa kwa ID hizi hizi kuanzia EPA hadi RICHMOND na kuwa chanzo kikuu cha habari.Masharti na kanuni za JF zimezingatiwa.Tafadhali usituondoe kwenye mijadala
What are you talking about?
Hayo ya EPA, RICHMOND unayosema yameletwa hapa jf na kuwa backed up by hard evidence.

Jf siyo kijiwe cha kahawa kama unataka habari yako watu wenye fikra pevu waiangalie kwa macho mawili na waichukue serious.

Ulicholeta hapa ni kama udaku ambao unaweza kuokota sehemu yoyote ile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…