WanaJF,
Mimi Dr Slaa ambaye kwa siku 4 nimekuwa na ziara ya mkoa wa Iringa,Mbeya na Njombe nilikuwa narudi Dar jana baada ya kulala Iringa mjini kutokea Njombe.
Tukio linaloelezwa ni la kweli na nimelishuhudia mwenyewe. nimeingia kwa jina langu na ID yangu ili kuondoa dhana ya Spinning.
Namshukuru sana aliyetoa Taarifa, na kuliwasilisha kama ilivyotokea bila kuongeza wala kupunguza kitu.
Tuliondoka Iringa majira ya saa 3.30 hivi. Kwa mwanzo hatukutambua kitu, ila mara ya kwanza tuliona gari hilo likitupita kwa kasi km kama 20 hivi baada ya kupita junction ya Ipogolo. Tuliona kawaida. katika hatua hiyo tulijua ni wasafiri wenzetu. baadaye tukawa tunawapita, wanatupita kasi na kupotea, lakini baada ya muda tunawakuta na kutupisha. hatukustuka sana, japo kuanzia Ilula tukaanza kuulizana.
Mlima Kitonga wakatipita kwa kasi sana japo mbele yetu kulikuwa na semitrela kama 4 zikiteremka pole pole sana na nabasi 2 kwenye kona moja basi lililpkuwa mbele yetu kikakwaruzwa na lori lililokuwa lunapanda. Tukachukua tahadhari sana.
Tulipovuka daraja la Mtp Ruaha tukalikuta Lcruiser hiyo imesimama pembeni lakini abiria wake wote walikuwa ndani. tulipolikaribia likaondoka kwa kasi. kidogo tulistuka. sisi tukaamua makusudi kusimama na kununua vitunguu. Tulipofika Mikumi mjini tukalikuta tena likienda taratibu. kuanzia hapo tukawa makini sana hasa kwenye kona na au vichaka vikubwa. kimsingi tukajiweka kwenye hali ya tahadhari kubwa.
Moro tuliingia Petrol Station nao pia wakaingia nyuma yetu lakini hawakujaza mafuta. Punda wakaondoka direction ya Dodoma. Ikumbukwe sisi tumetoka Njombe tumetangaza tunaenda Kongwa ,Jimbo la Ndugai. mimi nikakapata dharura nikapaswa kurudi Dar. hivyo baada ya mufuta tukafuata direction ya Dar. Punde likatokeza tena na kutupita. Tukalipita kidogo kabla ya Chalinze. Baada ya Chalinze hatukuliona tena mpaka tulipolikuta Junction ya Tamko limepaka. mata nyibgine huwa natumia hiyo junction badala ya kuingia Jijini. Na kweli driver akapiga indicator nyingie hapo. nikaagiza tuelekee jijini Dar. ndipo ghafla nao wakaingia barabarani nyuma ya gari langu kabisa. ndipp nikaagiza afisa wangu apande juu ya gari letu -roof top na kulipga picha. kuona hivyo ghafla likatoka pembeni na kupaki. sisi tukaendelea, ndipo mbele kidogo tukakuta askari walioko zamu yao ya kawaida wakatusimamisha na tukawapa taarifa ya halu hiyo.
Sasa katika mazingira hayo kuna mtu bado anafikiria ni spinning anaweza kuamini hivyo hatuwezi kumlazimisha.
Natumaini nimefafanua ya kupotosha. Nawashukuru wote waliotupa pole. Tunaanza na Mungu tunabaki na Mungu. Hatumwogopi Binadamu na mapambano ya ukombozo hayatakoma kwa vitisho vya aiina hiyo, ndiyo kwanza vinatupa ari na mori.