Pre GE2025 Dkt. Slaa akamatwa usiku nyumbani kwake Mbweni

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
hiyo si sababu ya ku-arrest mtu
 
Dr. Slaa siyo mjinga. Anajua anachokifanya. Hiyo kamata kamata yake ni kuwatisha wengine. Mwisho wa siku watamuachia aendelee na shughuli zake. Maza hana ubavu wa kuhandle mambo mazito ka haya.
Sasa nani hajui anachokifanya? Na Serikali imemtia kibindoni Ili akome kumchafua Rais kisa upumbavu wao wa huko Chadomo.
 
Unfortunately ndio aina ya siasa tuliyoichagua kuwa nayo hapa nchini.

Watu badala ya kujikita kwenye hoja za kusaidia kutatua matatizo ya wananchi, huwa tunapenda kusikia umbea kama huu unaoibuliwa na kina Slaa.

Raia wanapenda kusikia mambo kama hayo, hivyo wanasiasa nao hawawezi kuacha kuwapa wanachokitaka.
 

Kama wanemkamata Dr. Slaa kwa kuvujisha Mshiko wa Maza kwa FAM kwa nini wasifanye hivyo pia kwa TAL kwa kudai hela za Abdul na Mama yake zimeingizwa CHADEMA kuchafua uchaguzi.

Binafsi sioni tofauti ya alichokisema Lissu na kile alichokisema Silaa.
 
Mzee anaendeshwa na vijana huko club house anajisahau atakuwa karopoka polisi wakamfuata alisaidie jeshi.
 
Hii inaonyesha ni jinsi gani unavyowachukulia watu kuwa ni miungu kwako. Kwa taharifa yako Siri zinavuja ili kutimiza maneno ya Mungu tu. Kuwa Yalio sirini yatahubiriwa juu ya mapaa ya nyuma By Jesus
 
JESHI la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, linamshikilia kwa mahojiano aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Sweeden, Dk Willibrod Slaa.

Slaa alikamatwa jana usiku nyumbani kwake Bweni na mpaka sasa Jeshi hilo halijaweka wazi tuhuma zinazomkabili mwanasiasa huyo ambaye pia amepata kuhudumu katika wadhifa wa Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mbunge wa Karatu.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, mahojiano na mwanasiasa huyo yamekwenda vizuri na hivi sasa wanaangalia sheria zinasemaje ili wachukue hatua zaidi.

Hata hivyo kamanda Muliro hakuwa tayari kueleza kwa undani tuhuma zinazomkabili Dk Slaa ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali na viongozi wake.
 
Hawa wana ccm wamejijengea mfumo wa kutetemekea wenye mamlaka hata kama wamekosea wana ujinga mwingi sana hawa
Siyo kutetemekea mkuu ni kuabudu. Hao watu wanawaabudu watu alafu wanataka kulazimisha kila mtu aabudu watu Kama wanavyofanya wao na ukikataa wanatamani hata wakuuwe uwa wanaona dunia hii Kama wameiumba mama zao
 
Kule slaa kakamatwa, huku mbowe anaongea na clouds kuhusu chadema na mambo yake, tujadili lipi?
 
JESHI la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, linamshikilia kwa mahojiano aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Sweeden, Dk Willibrod Slaa.

Slaa alikamatwa jana usiku nyumbani kwake Bweni na mpaka sasa Jeshi hilo halijaweka wazi tuhuma zinazomkabili mwanasiasa huyo ambaye pia amepata kuhudumu katika wadhifa wa Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mbunge wa Karatu.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, mahojiano na mwanasiasa huyo yamekwenda vizuri na hivi sasa wanaangalia sheria zinasemaje ili wachukue hatua zaidi.

Hata hivyo kamanda Muliro hakuwa tayari kueleza kwa undani tuhuma zinazomkabili Dk Slaa ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali na viongozi
wake.
 
Naangaliaga maoni yako, Kisha najisemea ya kwamba tuna safari ndefu sana.
 
Pamoja na kwamba Slaa ni mnafiki wala hastahili kuhesabiwa kama mpinzani wa CCM na hata huko CCM kwenyewe hawawezi kumkubali, ni mropokaji anayehaha kukubalika tena, lakini linapokuja suala la kumshutumu rais hiyo ni haki yake kama raia.
Ni upuuzi uliokithiri kufikiri kwamba rais anapaswa kusifiwa tu na haipaswi kushutumiwa, huo upumbavu wa aina hiyo ndiyo unafanya viongozi wanajifanyia mambo hovyohovyo wakijua raia wanawaona wao kama 'miungu-watu' na hakuna anayeweza kuwalaumu wala kuwakosoa.
 
Kazi imeanza tena.

Hizo ndio 4R za mama Abdul
Unajuaje kama kuna makosa ameyafanya?.Sheria za nchi ziko vile vile.4r nikatika mambo ya kisiasa nakijamii sio kwenye uhalifu wakijinai na mengine.nakumbuka huyo alishapewa hadi ubalozi kwahiyo inawezekana kuna kitu kazingua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…