Pre GE2025 Dkt. Slaa akamatwa usiku nyumbani kwake Mbweni

Pre GE2025 Dkt. Slaa akamatwa usiku nyumbani kwake Mbweni

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
JESHI la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, linamshikilia kwa mahojiano aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Sweeden, Dk Willibrod Slaa.

Slaa alikamatwa jana usiku nyumbani kwake Bweni na mpaka sasa Jeshi hilo halijaweka wazi tuhuma zinazomkabili mwanasiasa huyo ambaye pia amepata kuhudumu katika wadhifa wa Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mbunge wa Karatu.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, mahojiano na mwanasiasa huyo yamekwenda vizuri na hivi sasa wanaangalia sheria zinasemaje ili wachukue hatua zaidi.

Hata hivyo kamanda Muliro hakuwa tayari kueleza kwa undani tuhuma zinazomkabili Dk Slaa ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali na viongozi wake.
huyo Mzee mwenye roho ya tamaa na usaliti sio balozi gentleman ni mnafiki tu,

acha akaeleze unafiki wake huko polisi na basdae mahakamani ili angalau awe na adabu kidogo kwa viongozi wa kitaifa 🐒
 
Panawaka,

Zile Shutuma alizotoa Kwa Rais mnaona zipo sawa?

Hakuna siasa au harakati za vile tuache siasa za Kishamba.

----
Aina ya Siasa wanazofanya SyW zitawaponza wengi sana... Honestly..
Shutuma chafu sana dhidi ya Mbowe, Rais na watu wanomuunga mkono Mbowe.

Wasichojua hakuna kitu cha maana wanaweza panga CH kisivuje..

Sasa Dr. Slaa kadakwa wanahangaika kufanya updates CH na kutafuta mawakili bila hata utaratibu.

Vijana kuweni makini, mtaingia kwenye matatizo na wakukusaidieni hawatakuwepo
Acha vitisho vya kijinga, unataka kila mtu awe chawa kama wewe
 
Pamoja na kwamba Slaa ni mnafiki wala hastahili kuhesabiwa kama mpinzani wa CCM na hata huko CCM kwenyewe hawawezi kumkubali, ni mropokaji anayehaha kukubalika tena, lakini linapokuja suala la kumshutumu rais hiyo ni haki yake kama raia.
Ni upuuzi uliokithiri kufikiri kwamba rais anapaswa kusifiwa tu na haipaswi kushutumiwa, huo upumbavu wa aina hiyo ndiyo unafanya viongozi wanajifanyia mambo hovyohovyo wakijua raia wanawaona wao kama 'miungu-watu' na hakuna anayeweza kuwalaumu wala kuwakosoa.
Mkuu kwao wanaona ni kosa sababu wao wanamuabudu. Sasa ukimkosoa umemgusa kamungu kao.
 
Dr Slaa amekamatwa usiku huu.

Inasemekana amepelekwa kituo cha Polisi Mbweni.

Matukio ya kiusalama kuelekea uchaguzi mkuu 2025 angalia hapa: Kuelekea 2025 - Uzi Maalum wa Matukio ya Kiusalama kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Akizungumza kwa njia ya simu Dkt. Slaa ameeleza kuwa, polisi wamefika nyumbani kwake na kumchukua na kuelekea naye kituo cha polisi Mbweni.

- Kuelekea 2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Soma pia: Dkt. Slaa: Tundu Lissu anafaa kuwa Rais wa JMT leo na siyo Oktoba 2025...

View attachment 3197059
ni muhimu sana akapelekewa sobar house moja kwa moja kwasababu huenda amepata changamoto ya Afya ya akili,

mzee amekua hana adabu kabisa kwa viongozi wa kitaifa, utadhani katoto kadogo,

lakini pia mzee amezidisha unafiki kwa kiwango cha juu sasa. Nadhan jeshi la police limefanya kazi nzuri kumtia nguvuni mzee huyu mwenye tamaa kupindukia, msaliti na asie na shukrani 🐒
 
Back
Top Bottom