Pre GE2025 Dkt. Slaa akamatwa usiku nyumbani kwake Mbweni

Pre GE2025 Dkt. Slaa akamatwa usiku nyumbani kwake Mbweni

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mpaka sasa hatujapata taarifa kama Dr. Slaa kaachiwa au Laah. Ni vizuri pia mtujulishe amefanya tukio gani tena huyu Dr. Baloz mstaafu. Ana uhatari wowote kwa Taifa au kwa mtu yeyote kama mama abdul et al?

Je anaweza akawa anasababisha watu wazidi mchukia mbowe?kama anamharibia mbowe kwa kweli hapo akamatwe na serikali isimwache kabisa amharibie mwenyekiti wetu chadema. Mbowe kwa sasa ndo anafaa kuwa mwenyekiti chadema. Tunaona Dr. Slaa anampinga mbowe. Akamatwe afungwe.

Leo Mbowe alikuwa na mahojiano na kituo flani cha radio. Je ameongea nini?sioni taarifa yoyote about that. Nashangaa....mbowe alikuwa anaongea na taifa leo na watu mnataka kufanya kama mazungumzo yake yalikuwa siri. Siyo sawa
 
CCM mwenzao naona wamechokana wameanza kulana wenyewe kwa wenyewe.
KAZI ni kipimo cha UTU
 
Safi sana huyu Mzee mpumbavu amekuwa anamchafua Rais kisa upuuzi wao wa kugombea madaraka huko Chadomo via vibaraka wake.

Pia huyu Mzee na Kitima wanatumia Kanisa lao kueneza chuki za kijinga Kwa Rais.

Huyu atiwe adabu asitoke Hadi 2026 itapendeza sana,anajikuta spesho sana na Nchi ni familia yake anaichezea anavyojiskia.
Mchafu hachafuliwi
 
Panawaka,

Zile Shutuma alizotoa Kwa Rais mnaona zipo sawa?

Hakuna siasa au harakati za vile tuache siasa za Kishamba.

----
Aina ya Siasa wanazofanya SyW zitawaponza wengi sana... Honestly..
Shutuma chafu sana dhidi ya Mbowe, Rais na watu wanomuunga mkono Mbowe.

Wasichojua hakuna kitu cha maana wanaweza panga CH kisivuje..

Sasa Dr. Slaa kadakwa wanahangaika kufanya updates CH na kutafuta mawakili bila hata utaratibu.

Vijana kuweni makini, mtaingia kwenye matatizo na wakukusaidieni hawatakuwepo

Bila shaka timu mwamba na washirika wenu CCM mtakuwa na tafrija ya pamoja
 
Wanaosema Slaa ni balozi mstaafu, nakumbuka Rais alimvua hadhi ya ubalozi, je ni sawa kuendelea kumwita balozi mstaafu?
 
Watu wanachukulia poa lakini sasa hivi huko CCM na serikalini kuko moto zaidi kuliko huu moto wa mabua unaowaka Chadema. Dr. Slaa amesema hao wasiri wake wamemwambia aeleze wazi kuwa taarifa hizo zimetoka huko na kwa sasa wameamua kutoka hadharani hivyo hili jambo ni kubwa,Mama amechokwa kama alivyochokwa Sultan Mbowe ndiyo maana wana maagano yao kusaidiana katika hizi vita zao.
Ila Slaa ni mtu mahiri wa kucheza mind games.
 
Kifo cha Kujitakia Hakina Msiba..

Kama Usalama wa Taifa walimwambia Kuhusu Njama za Mama Abdul katika kuharibu au Kumpa Uenyekiti Mbowe Na Kumfedhehesha TAL..

Alitakiwa Ampe TAL Taarifa na Baada ya hapo wafanye Harakati Underground na Sio kwenda Media Na Kuongea alichoongea Serkali haijaribiwi..

Yeye kuwa na Mtu wa Ndani Ndani ya Idara ya TISS tayari ni Tishio kwa Serikali (Hasa kama Taarifa zake Ni za Kweli)..

Na Kibaya zaidi kama Taarifa yake aliyoitoa Ni ya Kweli Inaweza Kupelekea Au Kuhatarisha Maisha yake binafsi..

Wengi wana Watu pandikizi kwenye System Kina Lissu, Kina Mbowe na hata Kina Zitto ila Huwezi kuwakuta Mitandaoni au Club House wanatangaza Hilo..

Hiyo ni uchonganishi baina ya Serikali na Idara zake au Na majeshi yake..

Kutaka Kuonyesha Ufalme Umefitinika..

Pole zake na Akitoka Hapo Ajifunze..

"Sumu Aionjwi kwa Kulambwa"
Yaani unajaribu kumfunza nini Cha kuongea Dr Slaa?

Kwa Maarifa, uzoefu na umri alionao Unadhani aweza kukurupuka?
 
Watu wanachukulia poa lakini sasa hivi huko CCM na serikalini kuko moto zaidi kuliko huu moto wa mabua unaowaka Chadema. Dr. Slaa amesema hao wasiri wake wamemwambia aeleze wazi kuwa taarifa hizo zimetoka huko na kwa sasa wameamua kutoka hadharani hivyo hili jambo ni kubwa,Mama amechokwa kama alivyochokwa Sultan Mbowe ndiyo maana wana maagano yao kusaidiana katika hizi vita zao.
Moto ndani ya Chadema unawababua CCM

Amazing
 
Really? Alichokisema kinahatarisha usalama wa nchi kweli?

Hata kama walihitaji kumhoji, sioni ulazima wa kumkamata usiku.

Mambo mengine huwa wanaenda overboard. Labda kama hatua za awali za kutaka kuongea naye hazikuzaa matunda.

Ila kama shida yao ilikuwa ni kuongea naye tu, hakuna haja ya kumkamata usiku.

Dkt. Slaa siyo jambazi.
Hauwezi kusema hadharani uwa umeambiwa na afisa wa Usalama wa Taifa kuhusu mazungumzo binafsi kati ya Rais na raia mwingine wakipanga kuvunja sheria kwa kuwahonga watu ili wa subvert uchaguzi wa ndani wa chama pinzani ha siasa. Lazima ujue TISS watataka kujua ni nani aliyevujisha mazungumzo ya faragha ya rais.

Mimi siwezi kujua sababu za kumkamata usiku lakini inawezekana kuwa walitaka kuepuka tukio kuwa spectacle. The irony is, inawezekana ilikuwa ni sting operation. Kuwa alichomekewa huyo aliyedhani kuwa ni mtu wa TISS. He should have known better. Hakuwa na sababu yeyote ya kutaja source ya taarifa yake au hata kuwa yalikuwa ni mazungumzo yaliyomhusu Rais. Angesema tu kuwa ana taarifa ya mpango wa kuhujumu uchaguzi. Hayo ya nani kamwambia angeyamezea au angemwambia Lissu peke yake. Inasikitisha lakini kwenye hili kajitakia mwenyewe.

Amandla...
 
Panawaka,

Zile Shutuma alizotoa Kwa Rais mnaona zipo sawa?

Hakuna siasa au harakati za vile tuache siasa za Kishamba.

----
Aina ya Siasa wanazofanya SyW zitawaponza wengi sana... Honestly..
Shutuma chafu sana dhidi ya Mbowe, Rais na watu wanomuunga mkono Mbowe.

Wasichojua hakuna kitu cha maana wanaweza panga CH kisivuje..

Sasa Dr. Slaa kadakwa wanahangaika kufanya updates CH na kutafuta mawakili bila hata utaratibu.

Vijana kuweni makini, mtaingia kwenye matatizo na wakukusaidieni hawatakuwepo
Nani hajui kwamba ccm inaingilia michakato ya Cbadema?
 
Back
Top Bottom