Pre GE2025 Dkt. Slaa akamatwa usiku nyumbani kwake Mbweni

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mpaka sasa hatujapata taarifa kama Dr. Slaa kaachiwa au Laah. Ni vizuri pia mtujulishe amefanya tukio gani tena huyu Dr. Baloz mstaafu. Ana uhatari wowote kwa Taifa au kwa mtu yeyote kama mama abdul et al?

Je anaweza akawa anasababisha watu wazidi mchukia mbowe?kama anamharibia mbowe kwa kweli hapo akamatwe na serikali isimwache kabisa amharibie mwenyekiti wetu chadema. Mbowe kwa sasa ndo anafaa kuwa mwenyekiti chadema. Tunaona Dr. Slaa anampinga mbowe. Akamatwe afungwe.

Leo Mbowe alikuwa na mahojiano na kituo flani cha radio. Je ameongea nini?sioni taarifa yoyote about that. Nashangaa....mbowe alikuwa anaongea na taifa leo na watu mnataka kufanya kama mazungumzo yake yalikuwa siri. Siyo sawa
 
CCM mwenzao naona wamechokana wameanza kulana wenyewe kwa wenyewe.
KAZI ni kipimo cha UTU
 
Mchafu hachafuliwi
 


Bila shaka timu mwamba na washirika wenu CCM mtakuwa na tafrija ya pamoja
 
Wanaosema Slaa ni balozi mstaafu, nakumbuka Rais alimvua hadhi ya ubalozi, je ni sawa kuendelea kumwita balozi mstaafu?
 
Ila Slaa ni mtu mahiri wa kucheza mind games.
 
Yaani unajaribu kumfunza nini Cha kuongea Dr Slaa?

Kwa Maarifa, uzoefu na umri alionao Unadhani aweza kukurupuka?
 
Moto ndani ya Chadema unawababua CCM

Amazing
 
Hauwezi kusema hadharani uwa umeambiwa na afisa wa Usalama wa Taifa kuhusu mazungumzo binafsi kati ya Rais na raia mwingine wakipanga kuvunja sheria kwa kuwahonga watu ili wa subvert uchaguzi wa ndani wa chama pinzani ha siasa. Lazima ujue TISS watataka kujua ni nani aliyevujisha mazungumzo ya faragha ya rais.

Mimi siwezi kujua sababu za kumkamata usiku lakini inawezekana kuwa walitaka kuepuka tukio kuwa spectacle. The irony is, inawezekana ilikuwa ni sting operation. Kuwa alichomekewa huyo aliyedhani kuwa ni mtu wa TISS. He should have known better. Hakuwa na sababu yeyote ya kutaja source ya taarifa yake au hata kuwa yalikuwa ni mazungumzo yaliyomhusu Rais. Angesema tu kuwa ana taarifa ya mpango wa kuhujumu uchaguzi. Hayo ya nani kamwambia angeyamezea au angemwambia Lissu peke yake. Inasikitisha lakini kwenye hili kajitakia mwenyewe.

Amandla...
 
Nani hajui kwamba ccm inaingilia michakato ya Cbadema?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…