Dkt. Slaa amshutumu Magufuli kwamba zuio la mikutano ya hadhara lilikuwa batili na haramu
Hivi wakuu ni kwel njaa inaweza kukutoa akili? Je wazee kama hawa ambao kupitia siasa washapata pesa zao mpaka ubaloz, je ni njaaa hii au ana tatizo la akili au ni unafiki?? Hivi hakuna namna ya kukaa kimya na kula ulichochuma?

..nadhani hoja yake imewashinda kuipangua ndio maana mmeishia kumtukana.
 
Bado anatafuta uteuzi?

Hii nchi imekuwa ilivyo sasa kwa sababu ya watu kama huyu asiyejua kipi anakisimamia maishani mwake.

Kwa hiyo leo ndio amegundua ubatili wa hayo aliyoyafanya Magufuli; mbona hakuhoji alipokuwa anahongwa hongo ya ubalozi?
BTW: Huko ubalozini alifanya jambo lipi la manufaa kwa nchi aliyoiwakilisha kwa muda wote aliokuwa huko. Anaweza kutaja hata jambo moja tu?

Ninashangaa sana bado kuna watu wanampa 'relevance', hadi ya kuleta takataka zake hapa jukwaani.

..uko nje ya mada.

..jadili hoja iliyoko mezani, usimjadili mtoa hoja.
 
..uko nje ya mada.

..jadili hoja iliyoko mezani, usimjadili mtoa hoja.
"Mtoa hoja"? Nani Slaa?

Utatenganisha vipi mtoa hoja na hoja anazowasilisha?
Ninaamini nipo ndani ya hoja kikamilifu.

Kama huniamini, soma mtiririko wa michango inayowekwa hapa.
 
"Mtoa hoja"? Nani Slaa?

Utatenganisha vipi mtoa hoja na hoja anazowasilisha?
Ninaamini nipo ndani ya hoja kikamilifu.

Kama huniamini, soma mtiririko wa michango inayowekwa hapa.

..naamini hoja hii ni muhimu na hatutaitendea haki kama tutajikita kwenye kumchambua na kumshambulia mtoa hoja.
 
..naamini hoja hii ni muhimu na hatutaitendea haki kama tutajikita kwenye kumchambua na kumshambulia mtoa hoja.
Ninakubaliana na we juu ya umuhimu wa hoja; lakini kwa bahati mbaya sana aliyeiwasilisha si mfano mzuri wa hoja inayowasilishwa, ndiyo sababu watu wengi wanageukia kwa mleta hoja badala ya hoja yenyewe.

Mleta hoja ambaye yeye mwenyewe ni hoja tosha, na ni mfano halisi wa kutolea katika hoja anayoiwasilisha.
 
Naumia sana kuona kati ya waliochangia mada mpaka sasa ni mmoja tu kati ya 194 aliyemwelewa Dr. Slaa.

Kwa uelewa wangu mimi, Dr. Slaa yupo sahihi sana tu. Hajakurupuka wala hajakosea.

Maana yake ni kwamba, Samia akisema sasa anaruhusu mikutano ya hadhara, anakubali kwamba alivunja katiba ambayo aliapa kuilinda. Kwa maana hiyo, muda wowote na siku yoyote na Mtu yeyote anaweza akamfungulia mashtaka ya kosa la kukiuka Katiba ya Nchi ambayo aliapa kuilinda.

Kwa kifupi kabisa, waliokuwa wanatii kilichokuwa kikijulikana kama Katazo la mikutano ya hadhara, walikuwa wanatii KIVULI. Yaani, walikuwa wanatii kitu kisichokuwepo.

Ebu fikiri, CHADEMA wanao wanasheria mashuhuri kabisa, walishindwaje kwenda mahakamani kudai haki hiyo?

Hivi karibuni CHADEMA walitamka kwamba, wataanza rasmi kufanya mikutano ya hadhara bila kujali kuna zuio au la, Je, unadhani kwa kusema hivyo walikuwa wanajiandaa kuvunja sheria?
Walishatambua kuwa hicho kitu hakipo, kwa hiyo hata wakifanya hakuna sheria itakayowabana.
 
..uko nje ya mada.

..jadili hoja iliyoko mezani, usimjadili mtoa hoja.
Hata mimi nimeshangaa kwa nini watu hawajadili hoja wanamjadili mtoa hoja,

Lakini nimeshangaa zaidi kwa mtu kama kalamu naye kuingia kwenye mkumbo huo,

Kama hivi ndio Watanzania tulivyo, basi inasikitisha sana.

Dr Slaa kwa mambo aliyozungumza, itoker bahati mbaya aone majibu au mwitikio wa Watanzania ulivyo hapa, basi atakuwa na kitu kigumu sana kuwatetea au hata kuwapa elimu wananchi,

Tuna mihemko ya kijinga sana ninaweza kusema hivyo,

Mimi naungana na Dr Slaa katika yote aliyozungumza humu
 
Nina uhakika, Pamoja na tofauti iliyojitokeza kati ya Dr Slaa na Tundu Lissu, ila alichosema Dr Slaa ndio atachosema Lissu! Kama ulimsikiliza Lissu hivi karibuni huu ndio msimamo wake.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Dkt. Slaa anasema katazo la Magufuli lilikuwa null void ab initio.

Yaani ni agizo haramu na halina tofauti na agizo ambalo halikuwepo.

Msikilizeni Dr hapa chini.

Mbona mama nae alivyoshika madaraka alizuia?vp kuhusu yy
 
Hata mimi nimeshangaa kwa nini watu hawajadili hoja wanamjadili mtoa hoja,

Lakini nimeshangaa zaidi kwa mtu kama kalamu naye kuingia kwenye mkumbo huo,

Kama hivi ndio Watanzania tulivyo, basi inasikitisha sana.

Dr Slaa kwa mambo aliyozungumza, itoker bahati mbaya aone majibu au mwitikio wa Watanzania ulivyo hapa, basi atakuwa na kitu kigumu sana kuwatetea au hata kuwapa elimu wananchi,

Tuna mihemko ya kijinga sana ninaweza kusema hivyo,

Mimi naungana na Dr Slaa katika yote aliyozungumza humu
Watu wengi wanatumia akili ndogo kuchambua mambo magumu yanayohitaji akili kubwa.
 
Mbona mama nae alivyoshika madaraka alizuia?vp kuhusu yy

..hata Ssh naye amekosea kutoa kauli inayoashiria kwamba suala la mikutano si haki ya kikatiba bali ni ridhaa ya Raisi.

..alitakiwa kuliomba taifa radhi kwa ukiukwaji wa sheria na katiba uliotokea ktk awamu ya 5 na kuahidi kutorudia.
 
Dkt. Slaa anasema katazo la Magufuli lilikuwa null void ab initio.

Yaani ni agizo haramu na halina tofauti na agizo ambalo halikuwepo.

Msikilizeni Dr hapa chini.

Kigeugeu. Kwanini hakuyasema wakati simba mwenyewe akiwa hai? Au njaa na kiu ya asali ya mama?
 
Dkt. Slaa anasema katazo la Magufuli lilikuwa null void ab initio.

Yaani ni agizo haramu na halina tofauti na agizo ambalo halikuwepo.

Msikilizeni Dr hapa chini.

Kweli wewe joka kwa hii hadaa kubwa umetisha wewe ni joka
 
Back
Top Bottom