Kama Hayati Magufuli alimrubuni kirahisi hivyo na kuwasaliti Chadema na wapenda mageuzi kisa Ubalozi, basi wala msimuamini.
Fikiri kwa kina, Kama Rais Samia angelimbakiza Sweden Ubalozini mnadhani angelikuwa na Mwabukutu, hii movement ya SautI ya Watanzania angelikuwa Member? MUWE MNATUMIA AKILI NDOGO KUYAONA HAYA YA HUYU MTU
KAMA ALIDIRIKI KUSEMA "KUPIGWA LISU RISASI NI KITU CHA KAWAIDA", HUYU MSIMUAMINI KATU!
Bado siamini kama kweli ninakusoma wewe, mkuu 'Retired'!
Uko sahihi kabisa kuhusu hilo la kuwa na mashaka juu ya Slaa. Binafsi sijawahi kuwa na imani kubwa juu yake hata wakati angali yupo CHADEMA.
Lakini kuna mambo ambayo huwezi kumnyima heshima yake. Kwa mfano; kazi yake kubwa na nzuri kabisa aliyokuwa akiifanya akiwa Katibu Mkuu wa chama hicho, rekodi hiyo ipo wazi na CHADEMA haijaweza kufikia rekodi yake hiyo tokea aondoke.
Kazi zake Bungeni akiwa Mbunge zilionekana; hakuwa mbunge wa kwenda kulala Bungeni.
Kwa hiyo, ni swala muhimu la kujiuliza, huyu Slaa ilikuwa kuwaje akakengeuka vile wakati ule wa kuondoka CHADEMA? Bila shaka yapo mengi ya kueleza hapo, na mtu pekee anayeweza kufanya hivyo ni yeye.
Na zaidi ya hivyo, baada ya kuondoka ndani ya chama alichokiongoza, halafu na kutumia maneno anayosemekana kuyatumia dhidi ya viongozi wenzake, hili ni jambo la kusikitisha kwelikweli juu ya huyu mtu
Sasa, baada ya kuyasema yote hayo, huyu Slaa anachopigania sasa, pamoja na historia yake hiyo mchanganyiko, hatuwezi tukamtazama katika haya yaliyopo sasa?
Yupo upande gani.
Anatetea maslahi ya nchi, au yupo kwenye kukandamiza maslahi hayo
Hatuwezi kutenganisha historia yake hiyo katika haya maswala yaliyopo sasa?
Kwani lengoletu hasa ni nini? Kumwamini Slaa, au kushiriki na yeyote atakayechangia ili taifa letu lifikie mahali tunapoamini kuwa maslahi yake yanalindwa?
Mimi simwamini Slaa, lakini kama yupo tayari kusaidia kupambana na janga la CCM, hiyo ni sababu kuu zaidi ya kushirikiana naye kadri iwezekanavyo ili lengo letu lifanikiwe.
Mbowe amekwishauza roho yake kwa shetani; shetani yule yule aliyewahi kuiteka roho ya Slaa.