Ukweli uliowazi tunahitaji upinzani wenye nguvu na wenye hoja na hekima, unaotambua serikeli mbili za muungano na kuheshimu vyombo vya dola pamoja na kuheshimu viongozi wa vyama vingine.
Hatuhitaji upinzani unaochafua watu wengine ambao unahisi watakuja kugombea urais huko mbeleni. Upinzani ni lazima uwe na agenda zenye mashiko na zakitaifa, hatuhitaji upinzani ambao ukitafuta nani anafaa kugembea urais hupati, wao ni kuchafua viongozi ambao wamebana maslahi yao, upinzani ni lazima uwe sauti ya wananchi la sivyo huo sio upinzani.