Dkt. Slaa kuongoza kongamano kujadili falsafa ya Hayati Magufuli

Dkt. Slaa kuongoza kongamano kujadili falsafa ya Hayati Magufuli

Balozi Dk Wilbroad Slaa anatarajiwa kuongoza kongamano la tafakuri tunduizi ya kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kifo cha hayati John Pombe Magufuli...
Kwani ubalozi wa kuwakilisha nchi ulisha koma?
 
Hasara ni kuja kusahaulika kabisa!! Kwa wananchi wengi, kutokana na matendo yake maovu kuwa mengi kuliko mazuri!!unaona kina Mandela , Nyerere, na wengine hawatasahaulika lakini .Na legacy wala haihitaji nguvu kuelezwa bali hujieleza yenyewe!! Na kibaya zaidi kwa njinsi mama anayofanya mengi mazuri ya kuliponya taifa ndio kabisaa, jamaa anazidi kusahaulika!!
Utamsahau wewe, sisi wengine tume apa kuendeleza legacy yake na huo uwezo tunao, nguvu tunazo na sababu tunazo.
 
Hasara ni kuja kusahaulika kabisa!! Kwa wananchi wengi, kutokana na matendo yake maovu kuwa mengi kuliko mazuri!!unaona kina Mandela , Nyerere, na wengine hawatasahaulika lakini .Na legacy wala haihitaji nguvu kuelezwa bali hujieleza yenyewe!!
Na kibaya zaidi kwa njinsi mama anayofanya mengi mazuri ya kuliponya taifa ndio kabisaa, jamaa anazidi kusahaulika!!
Ni pimbi peke yake ambaye anaamini hao uliowataja hawana wa kupinga falsafa zao!

Wa kwanza ambaye humpinga mwl ni Lisu shujaa wako, Jpm anapingwa na mamia ya watu na anakubalika kwa Mamilioni ya watanzania
 
Mwanasiasa bora kabisa kuwahi kutokea ktk nchi hii.

Viva Dr slaaa!

Mwanasiasa mkweli asiyeyumba wala kuyumbishwa ktk misimamo yake.

Hana mvuto kwa sasa, nyota anayotaka kutembelea kwenye hilo kongamano ni aliyotoka nayo cdm. Toka ajiunge ccm nyota imefubaa.
 
Balozi Dk Wilbroad Slaa anatarajiwa kuongoza kongamano la tafakuri tunduizi ya kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kifo cha hayati John Pombe Magufuli.

Kongamano hilo litakalofanyika Ijumaa Machi 25, mwaka huu katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Mwanza pia linalenga kufanya tafakuri ya miaka sita ya utekelezaji wa falsafa aliyoitumia hayati Magufuli wakati akiomba ridhaa ya kuiongoza nchi 2015.

Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake, Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT) Mwanza, Profesa Costa Mahalu ametaja wazungumzaji wengine katika kongamano hilo kuwa ni Mbunge Mstaafu wa Bariadi Mashariki, John Shibuda na Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma.



Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Profesa Costa Mahalu akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Mwanza.

Wengine ni wahadhiri na watafiti wabobezi wa Historia na Uchumi katika chuo hicho, Profesa Mihanjo Eginald na Dk Anne Gongwe.

"Wakati wa uchaguzi mwaka 2015, tulisikia CCM ikitumia slogani ya Magufuli for Change huku Chadema ikitumia- Movement for Change, kongamano hili litaenda kutafakari utekelezaji kwa vitendo vya slogan hizo," amesema Profesa Mahalu

Profesa Mahalu amewaomba wasomi, wanataaluma na watanzania kujitokeza kwa wingi katika kongamano hilo ili kutoa mchango wao wakati huu ambao nchi inafanya kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kifo cha Hayati John Magufuli na mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Hili ni kongamano la kujadili mizimu ya jehanamu.

Ni kongamano haramu
 
Back
Top Bottom