jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,329
- 25,263
Tukio la mwanasiasa wa upinzani kushambuliwa kwa risasi halafu uchunguzi ambao wewe na Dr Slaa mnasema polisi waachiwe, bado hata haujaanza!!Nikifaninisha tukio la Lissu na la ndugu zangu waliopoteza uhai Kibiti, na polisi waliopoteza uhai kwa kushambuliwa wakiwa katika malindo yao naona tukio la Lissu ni la kawaida tu. Viachwe vyombo husika vifanye kazi yao katika uchunguzi wa matukio haya.
Zaidi, ni kujaribu kuzuia matokeo yake kisiasa yasiwe mabaya! Hizo ndo mbinu ninazoziona hivi sasa!
Slaa atageuka kuwa balozi wa propaganda dhidi ya shambulizi la Lissu.
Kitu kitakachokuwa kimemfanya akubali ni pesa pamoja na visasi!
Baada ya kumtoa supermarket huko Canada, sasa wanamtumia kama toilet paper.