Dkt. Slaa: Tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na watu ‘wasiojulikana’ ni jambo la kawaida

Dkt. Slaa: Tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na watu ‘wasiojulikana’ ni jambo la kawaida

..Dr.Slaa amejibu kama BALOZI wa Tz.

..kwa wadhifa wake huwezi kutarajia atoe jibu tofauti na alilotoa.

..lakini pia kuna mahali Dr ameteleza.

..kama anadai tukio la TL kushambuliwa kwa risasi ni jambo la kawaida hata huko Canada, basi atueleze ni lini MNADHIMU wa kambi ya UPINZANI ya CANADA alishambuliwa kwa risasi wakati wa vikao vya BUNGE.
Shikamoo Kaka JokaKuu! Nilisahau kwamba Daktari hivi sasa sio mwenzetu!!

Halafu unadhani mimi nina tatzo basi kwenye hili suala la polisi!!! Tatizo langu ni pale, ninapoona sina kukumbukumbu ya kupatikana kwa watuhumiwa wa tukio lolote linalofanana na la TL. Lau kama tungekuwa na historia ya kuwanasa watuhumiwa, wala nisingekuwa na tatizo... ninge-assume it's a matter of time!

Kinyume chake, nakumbuka matukio kama...
-Saed Kubenea kumwagiwa tindikali
-Dr. Ulimboka kusagwa hadi palipoandikwa basi
-Tukio sawa na la Ulimboka likamkuta Absolom Kibanda
-Ben Saanane

Sasa hapo unajiuliza... ni muujiza gani utatokea kwa TL manake sina kumbukumbu kabisa kama kuna mtu amewahi kufikishwa mahakamani kwa tukio lolote hapo juu; japo kwa kuzuga kama ambavyo walifanya kwa yule chizi wa Kenya Joshua kwamba eti ndie karipua kule Arusha!!!!
 
Ahsante sana Mkuu haji humu siku hizi maana anajua atachapwa za uso za kufa mtu labda kama ana ID nyingine tofauti na hii.

Mkuu anaingia sana humu kwa ID fake maana anajua huku ni kwa moto, huku jf sio eneo la kujichia wanafiki hata kama wameanza unafiki uzeeni.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Lile tukio la kukatwa korodani mlinzi wa dr.slaa mbona lissu alisema ni jambo la kawaida, babla jamaa zake kagenzi walilipiza?
Good liar!!Alikatwa pumbu ?Hebu weka habari ya ushahidi au picha niamini ulichoandika.
 
Nadhani dr ajitathmin huyu ni balozi wakutuwakilisha wananchi yaha mambo yao ya lowasa na chadema bora angeyaacha hukohuko, tuangalie maisha ya watu tuangalie ustawi wa nchi yetu.
 
Shikamoo Kaka JokaKuu! Nilisahau kwamba Daktari hivi sasa sio mwenzetu!!

Halafu unadhani mimi nina tatzo basi kwenye hili suala la polisi!!! Tatizo langu ni pale, ninapoona sina kukumbukumbu ya kupatikana kwa watuhumiwa wa tukio lolote linalofanana na la TL. Lau kama tungekuwa na historia ya kuwanasa watuhumiwa, wala nisingekuwa na tatizo... ninge-assume it's a matter of time!

Kinyume chake, nakumbuka matukio kama...
-Saed Kubenea kumwagiwa tindikali
-Dr. Ulimboka kusagwa hadi palipoandikwa basi
-Tukio sawa na la Ulimboka likamkuta Absolom Kibanda
-Ben Saanane

Sasa hapo unajiuliza... ni muujiza gani utatokea kwa TL manake sina kumbukumbu kabisa kama kuna mtu amewahi kufikishwa mahakamani kwa tukio lolote hapo juu; japo kwa kuzuga kama ambavyo walifanya kwa yule chizi wa Kenya Joshua kwamba eti ndie karipua kule Arusha!!!!
Joshua nadhani Kova alisema ndiye aliyemteka Ulimboka kama kumbukumbu zangu zipo sahihi
 
Dk Slaa: Nalindwa na Mungu

Na Gazeti la mwananchi: Dk Slaa amvimbia Waziri Nchimbi


Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa
Fredy Azzah na Fidelis Butahe

KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema hawezi kujipeleka polisi kuhojiwa kutokana na kauli yake kwamba yeye na viongozi wengine wawili wa chama hicho wanatishiwa kuuawa na kigogo mmoja wa Idara ya Usalama wa Taifa, huku akieleza sababu mbili za kugomea wito huo wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi.Juzi, Dk Nchimbi aliliagiza Jeshi la Polisi kuwahoji viongozi wote wa Chadema waliotoa tuhuma za kutaka kuuawa hata kama wao hawana imani na jeshi hilo.

Akizungumzia na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Dk Slaa alisema yeye na wenzake, Mbunge wa Ubunge, John Mnyika na Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema hawatakwenda polisi kuhojiwa na jeshi hilo likitaka liwakamate.

Alilishauri jeshi hilo kutumia njia zake za kiitelijensia kujua ukweli wa mambo badala ya kufikiri kwamba wanaweza kupata maelezo kuhusu suala hilo kutoka kwake au viongozi wengine wa chama hicho.

“Leo (jana) asubuhi Ofisa wa Makao Makuu ya Polisi amenipigia simu kuomba appointment (miadi) lakini nasema sina muda. Sisi hatuendi (polisi) kwa sababu walishatudanganya mara nyingi tu.

Kama wanataka watukamate. Wao wana wapelelezi na usalama wachunguze,” alisema Dk Slaa na kuongeza:
“Kwani wao wanavyotukataza kufanya mikutano wakisema wana taarifa za kiitelijensia, huwa tunawauliza ni nani kawaambia? Na wao wachunguze kwa vyombo vyao kwa sababu ni jukumu lao kulinda usalama wa wananchi .”


Sababu za kutoamini polisi

Dk Slaa alisema sababu ya kutokuwa na imani na polisi ni pamoja na kutomweleza mpaka leo, vilipo vinasa sauti walivyovichukua katika hoteli aliyokuwa akiishi mjini Dodoma... “Walivichukua vile vinasa sauti na hawakutuambia ni nini kilichokuwa ndani, wangetupa tupeleke kwa wataalamu tukavichunguze.”

Alisema sababu nyingine ni tukio la kupigwa kwa wabunge wa chama chake mkoani Mwanza, akidai kwamba licha ya polisi kupewa taarifa mapema, hawakuchukua hatua yoyote.

Kutokana na hayo, alisema haoni sababu ya kuhojiwa na polisi kwani viongozi wa chama hicho kwa muda mrefu wamekuwa wakieleza mambo mbalimbali yanayotishia usalama wa wananchi na nchi, lakini jeshi hilo limeshindwa kuyafanyia kazi.

“Sasa kama wameshindwa hayo sasa wanataka kutuhoji kwa lipi? Hatuendi sisi tumeshawaeleza kinachoendelea kazi ni kwao,” alisema Dk Slaa.
Alisema taarifa walizozipata juzi ni kwamba maofisa wa jeshi hilo walikaa kikao muda mfupi baada ya kusikia tuhuma zilizotolewa na chama hicho na kuongeza kwamba wanachokisubiri hivi sasa ni kukamatwa.

Alidai kuwa jeshi hilo linaendelea kufanya makosa huku likitambua wazi kuwa maisha ya Watanzania yapo hatarini.

“Ndiyo maana, madaktari wameomba Umoja wa Mataifa (UN), kumwekea ulinzi Dk Steven Ulimboka katika hospitali aliyolazwa, hii yote ni ishara kwamba hali si shwari,” alisema Dk Slaa.
Alisema kazi ya polisi ni kutekeleza wajibu wao mara baada ya wananchi kutoa taarifa zinazohitaji kufanyiwa uchunguzi.

“Chadema ni chama makini, tunajua kuwa polisi walifanya kikao, wanatakiwa kujua kuwa nyumba yao inavuja… sasa kama nyumba yao inavuja sisi hatuoni haja ya kwenda kuhojiwa. Tunamuomba Mungu na tunajua atatulinda na wao acha waendelee kufanya vikao vyao.”
 
Ni kweli kabisa na kila siku nimeendelea kusema humu JF ya kuwa hakuna ushahidi wa kutosha unathibitisha mtu aliyemdungua Lissu risasi. Nikaendelea kuwapa member walalamishi wasiotaka kuelewa wakereketwa wa upande wa pili kama wana evidence wapeleke polisi haki itendeke washukiwa wafikishwe kortini.

Note;"huna haki ya kuzungumza pasipo kuwa na ushahidi wa kile unachokizungumza"
Mkuu mbona unajitoa ufahamu,,,, nani alitoa zile camera za security
 
Joshua nadhani Kova alisema ndiye aliyemteka Ulimboka kama kumbukumbu zangu zipo sahihi
Hahaaa!! Wallah Kova hakuwa mzima kichwani yule!!! Nime-confirm, you're right! Joshua ndo alimteka Ulimboka.... hahaaa! Sasa huyu Sele nae hata kudanganya hajui!!! Ni nani angeamini Joshua angekuwa na ubavu wa kumteka Ulimboka na kumsaga namna ile?!
 
Mkuu, kwenye criminal case kwa kawaida huwa kunakuwa na Potential suspects ......... sasa kinachozungumziwa humu ni potential suspects. Potential suspects naye huwa anaweza kujisafisha mwenyewe. Dr. Slaa must know better!!

Hata huko Canada anakokuzungumzia kama kuna potential suspect police huwa wanamfuata na kumhoji .... kama hakuna huwa wanajaribu kuto features au michoro tena hata hadharani ili raia wema wasaidie kuwaidentify wahalifu.

Kwa kawaida watu hawawezi kwenda tu police kutoa ushaidi unless wameombwa ..... kwa nini hawakutangaza number ambayo raia wanaweza kutoa taarifa kwa siri au hata kutoa posho ya million 10 kwa yule atakayesaidia kutoa ushahidi!!?
Duh!! Posho 10mil? Kufa kufaana
 
Back
Top Bottom