Dkt. Slaa: Tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na watu ‘wasiojulikana’ ni jambo la kawaida

Dkt. Slaa: Tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na watu ‘wasiojulikana’ ni jambo la kawaida

Naona huyu naye anataka ampokee Alhad Musa kusemwa na Mangi kimambi
 
Hao wenzetu Mkuu uhuru wa vyombo vya habari ni mkubwa sana na haya mambo wanajifunza kwa kina siyo kama hawa wa kwetu ambao taaluma hii wanababia babia tu na hao CloudsCCM 360 ambao KAMWE hawawezi kuuliza maswali magumu kwa mtu wa “Chama na Serikali”

chige, BAK,

..Tz tunahitaji mwandishi wa habari kama Tim Russet wa kipindi cha " meet the press " cha Wamarekani.

..Tim Russet alikuwa ana tabia ya kuchimba rekodi ya mtu anayemkaribisha ktk studio za " Meet the Press."

..Kwa hiyo wakati wa kipindi anakuwa tayari na rekodi ya matamshi ambayo mhusika aliwahi kuyatoa kabla ya mahojiano kufanyika.

..Kwa mfano, kwenye suala la TL, Tim Russet angemuacha Dr.Slaa apotoshe kama alivyofanya, halafu anakuja kumtolea statement zake za zamani, na kumbana kwanini anabadilisha kauli na misimamo yake ya awali.
 
Kajichanganya sana kwenye, huku yeye anasema alipotaja List of shame alikua na maadui wengi na aliwaita waandisha akawaambia, huku upande wa pili akisema amekimbilia Canada kwa sababu ni moja ya nchi zinazoheshimu haki za binadam, kwa nini hakukimbilia Polisi..
Kaongea vizuri sana kwenye mambo mengine, ila lilipokuja swala la Lissu hekima aliamua kuiweka pembeni... anaonekana ana hasira sana na Lissu
“He wants to have his cake and eat it too”
 
Wageni wa siasa ndo watashangaa hili la Dr slaa, hivi hapa jf kunamtu anaweza kuvaa udr slaa halafu akapingana na msimamo wa serikali?
 
..ulafi wa madaraka huwa unaleta upofu mwingi kwenye hizi banana republics....mfano mmoja ni huyu slaa...yeye akiwa upinzani alikuwa mtu wa kulalamikia vyombo vya habari kila kukicha... Haswa pale alipopigwa mkewe aliymwiba kwa mtu kama sheikh ubwabwa... Sasa hivi kapewa shavu na maccm anaona si vema kulalamikia vyombo vya Usalama visivyofanya majibu wao....hili la Lissu lazima amefurahia......maana lissu alikuwa mstari wa mbele kumpinga pale alipoasi chadema....



Ndio maana kule Arusha mkewe tu ndio alipigwa na Polisi. Yeye hata hakuguswa!

View attachment 691715
 
Ikiwa mwanadamu mwenye akili timamu anaweza kuliona tukio lile kuwa ni jambo la kawaida....tumedidimia chini mno.
Kinachoisumbua sana nchi hii ni njaa na unafiki bila kujali umesoma hadi wapi hayo masuala mawili ni balaa maana njaa huingia hata kula ubongo kisha mtu anaongea bila kujitambua.
 
Kapewa ulaji ninyi mnamhoji ili aharibu sahani aliyopewa hata mimi siwezi kusimama kwenye haki kwa hilo yuko sahihi
 
Hakuna mpinzani nilikuwa namuamini kama Slaa, na hakuna mwanasiasa ameniuma kutoka kwenye upinzani kama Slaa. Lakini nadhani sasa ni wakati sahihi wa kukubali kwamba yule wameshamchukua na sio mwenzetu tena.
 
Ni kweli kabisa na kila siku nimeendelea kusema humu JF ya kuwa hakuna ushahidi wa kutosha unathibitisha mtu aliyemdungua Lissu risasi. Nikaendelea kuwapa member walalamishi wasiotaka kuelewa wakereketwa wa upande wa pili kama wana evidence wapeleke polisi haki itendeke washukiwa wafikishwe kortini.

Note;"huna haki ya kuzungumza pasipo kuwa na ushahidi wa kile unachokizungumza"
Aliyemtolea bastola Nape hadharani mbele ya polisi na hajulikani hadi leo naye unamwongeleaje?
 
Slaa umemsariti Mungu utashindwaje kuona tukio la Lissu ni la kawaida? Unatakiwa utuambie kwanza ilikuwaje kazi ya utumishi wa Mungu ikakushinda?
 
Back
Top Bottom