Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kazi ipoMizimu kila mtu anayo, tunachotofautiana ni unamizimu ya aina gani? Ipo mizimu ya kimasikini, mizimu ya maradhi, mizimu ya kuvuruga mahusiano mizimu ya utambuzi , mizimu ya kichawi , mizimu ya utajiri n.k
Hao ulio wataja wana mizimu ya utambuzi mizimu ya kiganga kwenye watu elfu 30 unaweza kupata wawili au watatu tu.
Wachilia mbali mashekhe wakubwa huyo dokta sule hata mimi na ungumbaru wangu namfundisha mpaka anatoka mvi hajamaliza ninachokijua.Sule ni mwanazuoni mkubwa kwaiyo anajua dini hiyo kuliko wewe
.أنت ممّن تنادى من مكان بعيدHivi ikitokea sule kaokoka na kuachana na uislam atabaki salama? Wenzake watakubali kumuacha hai atoe siri za ushetani wa dini ya kiislam?
Mimi sio mwisilam ila Mganga sule ni yuko shallow sana kwenye dini lakini anatafuta attention to mitandaoni mara awadiss wasanii Yani ni chizi wa umaarufuWachilia mbali mashekhe wakubwa huyo dokta sule hata mimi na ungumbaru wangu namfundisha mpaka anatoka mvi hajamaliza ninachokijua.
Samahani mkuu, kwa hiyo wewe hauamini kama kuna ushirika wa Majini na Waislam ambao unaruhusiwa kwa mujibu wa imani?.Hawa watu ni waganga wa kienyeji wanawashika masikio waislamu wanaopenda short cut na wasio na maarifa wala utambuzi juu ya dini yao, habari za kuabudu na kuomba msaada majini ni katika madhambi yanayomtoa mtu kwenye uislamu.
Na siku atakayowakusanya wote, kisha atawaambia malaika: "Hivi hawa walikuwa wakiwaabudu nyinyi"? watasema: "Tunakutakasa kukutakasa, wewe ndiye kipenzi chetu kinyume na wao, bali wao walikuwa wakiwaabudu majini, wengi wao wakiwaamini hao".
Qur'an 34:40-41
Huu ndio uislamu wa sawasawa unamtaka mtu kufanya kazi na kutafuta rizki ya halali, na si kutumia ushirikina wala kafara na matambiko na kuwanyenyekea majini kupata mali, nimeona hapo juu watu wengi wameutukana uislamu kwasababu ya neno la mtu mmoja asiyejua hata uislamu ni nini.
Wakuu kuweni na uvumilivu sisi ndo tumeshakuwa waislamu na tutabaki hivyo mpaka siku ya kufa kwetu kwa idhini ya allah, punguzeni chuki na muache matusi yasiyo na maana, uislamu uko mbali na kuabudu na kuwataka msaada mashetani.
Exactly anatumia ule uwezo wa kuongea sana wa huko pwani, na hawa watu wa kufanya mijadala ya biblia na wachungaji ndio zao, na wanagawana sadaka zinazopatikana na wanawauzia watu dua, dua zinauzwa?.Mimi sio mwisilam ila Mganga sule ni yuko shallow sana kwenye dini lakini anatafuta attention to mitandaoni mara awadiss wasanii Yani ni chizi wa umaarufu
Naam mkuu wangu, mimi ni muislamu wa kuzaliwa na ni mwanafunzi niliyechukua faragha kuisoma dini namaanisha nina miaka 10+ nikiwa nasoma na bado ningali darasani, ninachokueleza hakuna ushirika wowote baina ya majini na wanadamu bali wao ni viumbe mbali na sisi ni viumbe mbali.Samahani mkuu, kwa hiyo wewe hauamini kama kuna ushirika wa Majini na Waislam ambao unaruhusiwa kwa mujibu wa imani?.
Vipi zile kauli za uwepo wa Majini mema yanayomuabudu Allah kwa kushirikiana na Waislam si za kweli?.
Naomba unisaidie kuondoa mkanganyiko huo.
Mbona nawasikiaga' Waislam wengi tu wanazungumzia hayo.majini.kama maswahiba waoHawa watu ni waganga wa kienyeji wanawashika masikio waislamu wanaopenda short cut na wasio na maarifa wala utambuzi juu ya dini yao, habari za kuabudu na kuomba msaada majini ni katika madhambi yanayomtoa mtu kwenye uislamu.
Na siku atakayowakusanya wote, kisha atawaambia malaika: "Hivi hawa walikuwa wakiwaabudu nyinyi"? watasema: "Tunakutakasa kukutakasa, wewe ndiye kipenzi chetu kinyume na wao, bali wao walikuwa wakiwaabudu majini, wengi wao wakiwaamini hao".
Qur'an 34:40-41
Huu ndio uislamu wa sawasawa unamtaka mtu kufanya kazi na kutafuta rizki ya halali, na si kutumia ushirikina wala kafara na matambiko na kuwanyenyekea majini kupata mali, nimeona hapo juu watu wengi wameutukana uislamu kwasababu ya neno la mtu mmoja asiyejua hata uislamu ni nini.
Wakuu kuweni na uvumilivu sisi ndo tumeshakuwa waislamu na tutabaki hivyo mpaka siku ya kufa kwetu kwa idhini ya allah, punguzeni chuki na muache matusi yasiyo na maana, uislamu uko mbali na kuabudu na kuwataka msaada mashetani.
Inafikirisha 🤔
Wapo wengi sana, we angalia waganga wote na wapiga ramli utajionea mwenyewekwa hiyo unaihukumu dini mzima kwa ajili ya sule...sio?
Naam hao ni waislamu washirikina mkuu, wanadai uislamu na bado wana makando kando yao na wengi utakuta ni waislamu wa ukanda wa pwani yaani dar, zanzibar, lindi, mtwara, na tanga na uislamu uko mbali kuliko umbali wa mbingu na ardhi kuhusu huo ushirika.Mbona nawasikiaga' Waislam wengi tu wanazungumzia hayo.majini.kama maswahiba wao
.mara nna jina langu !na blabla.kibao....
Mwanazuoni ? nani alimpa title ya mwanazuoni ? Alisomea chuo gani kinachojulikana duniani kwa elimu ya dini ya kiislamu? University of madina?, dammaj ? Al azhar ? E.t.cSule ni mwanazuoni mkubwa kwaiyo anajua dini hiyo kuliko wewe
Pole Sana.ikitokea sule kaokoka
Nimekuelewa, ingawa sasa matendo ya viongozi na maneno yao ya kiimani wanayoyatenda huku mitaani, nadhani yamechagiza baadhi kuisema isivyofaa imani hiyo.Naam mkuu wangu, mimi ni muislamu wa kuzaliwa na ni mwanafunzi niliyechukua faragha kuisoma dini namaanisha nina miaka 10+ nikiwa nasoma na bado ningali darasani, ninachokueleza hakuna ushirika wowote baina ya majini na wanadamu bali wao ni viumbe mbali na sisi ni viumbe mbali.
Mkanganyiko uliopo ni huu ufuatao na nitasema ukweli kwa mujibu wa uislamu, majini ni viumbe kama sisi wameumbwa kwa malengo ya kuabudu kama sisi, wao wapo kwenye ulimwengu usioonekana na sisi tupo kwenye ulimwengu huu unaoufahamu, kuna wema na waovu kama ilivyokuwa kwetu wanadamu, na wao wana maisha yao na sisi tuna maisha yetu.
Ama kuhusu ushirika au ushirikiano wowote baina ya waislamu wanadamu na waislamu majini huu haupo kabisa, bali ukifanya hivyo ndio maana halisi ya ushirikina unaopigwa vita na uislamu tangu hapo kale.
Amesema allah aliyetukuka: "Na wamemfanyia Allah majini kuwa washirika wake, na hali ya kuwa yeye ndiye aliyewaumba, na wakamzulia kuwa ana watoto wa kiume na wa kike pasi na elimu yoyote, ametakasika kutakasika kabisa! na ametukuka juu ya hayo wanayomsifia!".
Qur'an 6:100
Sasa ni jambo lisilowezekana Qur'an ambayo ndiyo sheria mama kwenye uislamu ijigonge yenyewe kwa yenyewe, nadhani nimefafanua kama una swali au hujaelewa naweza kueleza tena kwa namna nyingine, asante.
Kwa wasioelewa niwafungue ufahamu. Majini Ni malaika walioasi Wakatupwa Duniani pamoja na Bosi wao Lucifer . Hiyo Ndio maana ya Majini.
Hao ni waganga wa kienyeji mkuu na ukifanya utafiti utakuta ndio wapiga ramli wanaosaidia watu sijui kupata kazi kumleta mpenzi karibu, kuwawekea limbwata wanandoa na mambo kama hayo, jua mkuu uislamu ni mpana sana wengi katika hao unaowataja wala hawana maarifa stahiki ya uislamu.Nimekuelewa, ingawa sasa matendo ya viongozi na maneno yao ya kiimani wanayoyatenda huku mitaani, nadhani yamechagiza baadhi kuisema isivyofaa imani hiyo.
Utakuta mhusika ni Imam, Shekh au Usitadhat ila anahubiri habari za majini na ushirika wake na Waislam au anamiliki kiringe kihalali kwa ajili ya tiba zinazohusisha majini.
Nimeelewa wafanyayo hayo, wako kinyume na Uislam ingawa bado wanaitwa/wanajiita Waislam.