Naona wagalatia wanakuja mbio na matusi pasi na kujua Sule kazungumza nini.
Mleta mada ungeweka video watu wasikilize sio kuleta maneno baadhi yenye mkanganyiko.
Sule alichosema ni kuwa kuwatumia majini wenye mali kupata mali sio haramu.
Ila katika kuwatumia huko ni kwa kumuomba Mungu hao majini watii kwa kupitia neno la Mungu.
Kuna majini wanashikilia mali za dhahabu,almasi,ruby.
Unawafanyaje watii wakugaie mali?
Ni kupitia visomo vitakaowafanya wanyeyekee kwa jina la Mungu.
Na Sule alitanabaisha kuwa sio kwa kutumia makafara kutoka kwa waganga na ukapewa mapepo ya kafara laa hasha huo ushirikina.
Ila kwa kutumia kumuomba Mungu ili uwanyenyekeshe majini hilo ni sawa.
Kama Nabii Suleyman alikua akiwanyenyekesha majini kwa kumtaja Mungu maana Mungu ndio kaumba hao majini.
Narudia Sule hakukusudia kutumia mashetani ya kafara.
Kuna kitu katika uislam tunakiita Khadiim,maana yake mtumishi wa kiroho.
Hao watumishi wa kiroho wapo malaika na majini wasafi ambao huwezi kuwaona abadan mpaka ufanye utajo wa Mungu.
Na ukiwa mtu wa ibada sana katika masiku meupe hawa viumbe wanaweza kukutembelea pasi na wewe hata kuwaita ukashangaa wamekutembelea.
Niishie tu hapa ila kiufupi Dr Sule hajakusudia mashetani ya kafara.
Cha kuongezea,hao khudaam huwezi kuwafuga hawafugiki ng'oo.
Bali unawanyenyekesha na wakitimiza ulichoomba wanaondoka na mpaka warudi tena aisee ufanye kazi uache kazi.
Yani khadim ni sawa na nyota ya jaa.