Si kila mwanawachuoni ni wa kumfuata narudia tena watu tusome kwa misingi ya salafi swaleh ili tuweze kuielewa dini kama ambavyo inatakikana .
Kuwanyenyekeza kwa minajili ipi? Mtume alishindwa kuwanyenyekeza ili awatumie kwenye vita vyoote alivyopigana? Jibu ni hakushindwa ila alifanya nini kama mbadala? Jibu ni alimtegemea Allah(the all powerful) kwenye kila jambo lake .
Majini waachwe waishi maisha yao na sisi tuishi maisha yetu kwa kumtegemea Allah (the almighty )kwenye kila jambo unapoanza kuingiliana na hao viumbe utajikuta unaingizwa kwenye shirki kubwa angalia aya ya 102 ya surat baqara nanukuu.
Al-Baqarah 2:102
وَٱتَّبَعُوا۟ مَا تَتْلُوا۟ ٱلشَّيَٰطِينُ عَلَىٰ مُلْكِ سُلَيْمَٰنَۖ وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَٰنُ وَلَٰكِنَّ ٱلشَّيَٰطِينَ كَفَرُوا۟ يُعَلِّمُونَ ٱلنَّاسَ ٱلسِّحْرَ وَمَآ أُنزِلَ عَلَى ٱلْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَٰرُوتَ وَمَٰرُوتَۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَآ إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْۖ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِۦ بَيْنَ ٱلْمَرْءِ وَزَوْجِهِۦۚ وَمَا هُم بِضَآرِّينَ بِهِۦ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ ٱللَّهِۚ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْۚ وَلَقَدْ عَلِمُوا۟ لَمَنِ ٱشْتَرَىٰهُ مَا لَهُۥ فِى ٱلْءَاخِرَةِ مِنْ خَلَٰقٍۚ وَلَبِئْسَ مَا شَرَوْا۟ بِهِۦٓ أَنفُسَهُمْۚ لَوْ كَانُوا۟ يَعْلَمُونَ
Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani
Na wakafuata yale waliyo zua mashet'ani kuuzulia ufalme wa Su leiman. Na wala Suleiman hakukufuru, bali mashet'ani ndio walio kufuru, wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyo teremshwa kwa Malaika wawili, Haaruta na Maaruta katika Baabil. Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru. Wakajifunza kwa hao wawili yale ya kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawawezi kumdhuru mtu ila kwa kutaka Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza yatayo wadhuru wala hayawanufaishi. Na hakika wanajua kwamba aliye khiari haya hatakuwa na fungu lolote katika Akhera. Na hakika ni kiovu mno walicho jiuzia nafsi zao laiti wangelijua.
Mwisho wa kunukuu.
Unaposoma aya hiyo hapo unagundua kwamba wapo pia walioweka ukaribu na mashetani (jinni ni jamii ila shetani ni sifa na kuna shetani wa kijini na wa kibinadamu).
Na hao mashetani wakawafundisha wao uchawi ambao ni kufru kubwa kabisa na dhambi ambayo ukifa haujatubia basi haina msamaha na mtu ataingia motoni milele.
Hivyo ushauri wangu ni kuisoma dini kutoka kwa wanawachuoni wanaoaminika na ambao wanafuata quran na sunna .
NA ALLAH (THE ALMIGHTY) ANAJUA ZAIDI.
Mkuu naona kuna sehemu hatujaelewana.
Suala la jihad ni suala lingine huwezi lihusisha na masuala ya rizki.
Pia jihad wamuomba Allah ndio ushinde kama ilivyo rizki.
Kumnyenyekeza kiumbe sio sawa na kumtegemea.
Kumtegemea inamaana unaomba nguvu kwa mwengine akuongeze nguvu.
Na hiyo ayah ulioleta inaelezea assihru/uchawi.
Uchawi ni sehemu ya SHIRKI.
Narudia mfano wangu,unapoenda kutafuta rizki huwa rizki anapanga Allah hapangi mtu wala jini.
Kuna sehemu baadhi ya rizki huwa kuna hao viumbe,kama hautaenda vizuri unaweza kudhurika.
Ndio maana nikatoa mfano wa migodini,zile mali zinashikiliwa na majini.
Sasa ili uzipate muombe Allah mtegemee Allah kwa visomo vyake.
Moja wapo wa kisomo kusoma suratul Kauthar mara 1000,katika kila idadi ya 100 kuna adh'kar unasoma za kumuomba Allah awanyenyekeze wale viumbe,NARUDIA KUNA ADH'KAR YA KUMUOMBA ALLAH AWANYENYEKEZE WALE VIUMBE KWA WAKATI ULE WASIKUDHURU NA WAONESHE UNYENYEKEVU KWA NGUVU ZAKE ALLAH.
Ukifika idadi ya 1000 kaka mzigo unaachiwa huo hapo eidha kwa kuuchimba au hata kwa kuletewa hapo nje.
Bimaana umemuomba Allah akupe ukubwa wa kuwadogosha wale majini.
Ila hujawaomba wale majini,sijui hapo umenielewa kaka?
Ndio maana nikasema ile video watu hawakumuelewa Sule.
Sule hakuzungumzia kuwategemea majini KILA KATIKA UTAFUTAJI WA RIZKI.
Bali kumuomba Allah awanyenyekeze hao majini kwako katika baadhi ya sehem za utaftaji rizki ambazo wao wanazishikilia.
Natumai kaka utaelewa nini nalenga.