Dkt. Sule: Kutumia Majini kupata Mali si dhambi/ haramu

Umesomeka sheikh kuna watu wanadandia gari kwa mbele
 
Umemaliza kila kitu
 
Aisee...Sasa hii imekomaa sana,hadi sisi wengine tunaihusisha Dini ya Kiislam na hao viumbe ...kuwa Wana undugu! Sasa mbona huwa halikemewi Kwa nguvu! Kama anavyokemewa Nguruwe!?
 
Kati ya majini 99 haya hapa ni baadhi. Sina muda wa kueleza kazi zake ambazo ni mbaya kwa ujumla hakuna jini mzuri hata mmoja. Jini badri/albadri, jini zohari/zuhura, jini zabaniat, jini mwarabu/araba, jini khadtazi/kaim, jini subisubi/subian, jini jabrin/juber, jini maimuna, jini makata. Orodha ni ndefu naishia hapo majini yote ni makorofi ila kuna jini taariki kazi yake ni kufarakanisha na kutoa amani akijifanya ni mwema kumbe ni hatari. Wafuga majini ni washirikina
 
Kama ni suala la kumuomba Allah(the almighty) akukinge na hila za mashaitan ni swahihi , samahani kama sikuelewa nini ulimaanisha .

Ila kuhusu surat kawthar mara 1000 wacha nifuatilie zaidi.

ALLAHU A'LAM.
Elim ni pana sana zaidi tunavyo fikiria,kutojua kitu fulani haimanishi hakipo,tuendelee kujifunz
 
Kuna jini anaitwa Tajirun, ni jini wa kifahari. Hutumwa kwa mtu afanye kila jambo au kazi yeyote ili awe tajiri. Jini huyu hukupa moyo wa kupenda pesa kuliko Mungu. Ana uwezo wa kufanikisha miradi yako na kufanikiwa sana lakini hutakuwa kabisa na Mungu. Hayo yanayosemwa ni majini mazuri mwisho wake hugeuka kuwa mabaya. Hakuna jini mzuri
 
Majini ni viumbe agressive sana.
Ndio maana kidini ni marufuku kushirikiana nao.
Kitendo cha kutumwa kwako umtumie ni sawa na unashirikiana nae.
Haifai.
 
😂😂😂Kaka kuna majini zaidi ya 10000.
Hawa ni vipepo vichafu mkuu.
Ila kuna falme za majini huwezi kutana nao mpaka watake wao.
Hawa ndio huitwa khudaam.
Mfano;
-Aswaarul Kabiir.
-Hamamah.
N.k n.k,hawa wakitia timu sehem hadi mapepo machafu wakina maimuna wanakimbia kwa kishindo.
Huwezi kuwatumia kirahisi na huwezi kuwafuga kamwe.
Hawa ndio majini wa koo za kifalme.
 
Kama ni suala la kumuomba Allah(the almighty) akukinge na hila za mashaitan ni swahihi , samahani kama sikuelewa nini ulimaanisha .

Ila kuhusu surat kawthar mara 1000 wacha nifuatilie zaidi.

ALLAHU A'LAM.
Mkuu kuna kisomo cha ruqyah cha suratul yaasin 71.
Hiko pia unakijua?
Hiyo ni ruqyah kaka kaifuatilie,ina uwanda mpana,ruqyah ni kisomo cha Qur'an cha kumuomba Allah akisaidie kutatua shida zako mbali mbali ikiwemo za kiuchumi.
Kuna kisomo cha suratul ikhlasw 1000 pia.
Hikma yake ni nzito mzee.
Qur'an ina maajabu makubwa ya ruqyah.
 
Suleiman mwenyewe aliwatumia majini kwa kazi zake tena wazi wazi alipouliza majini na watu kipindi anataka wamletee kiti cha malkia wa Sheba ndio jini mmoja akajitokeza akasema atakileta kwa muda kabla ya kukaa akagoma akaja mwenye elimu zaidi ambaye ni binadam kwa muda kupesa jicho mara moja Nabii akamwambia akilete
 
Du ,wewe ni Muislam!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…