Dkt. Tulia Ackson ateuliwa na CCM kugombea Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Dkt. Tulia Ackson ateuliwa na CCM kugombea Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Itapigwa huko huko iliko sheria si zinatungwa bungeni

Ndio nasema tatizo mnahangaika na chadema Sana mpaka mnapambana hata asipokiwepo. Yani unatunga sheria ili tu kuiumiza CHADEMA na wala huwazi kwamba Bunge Ni chombo kinachowakilisha wananchi na sio kikao Cha chama Cha mapinduzi?. Endeleni kupambana na chadema kwa kuteka mihimili yote mwisho wa siku wananchi ndio wanaoumia kwa sheria mbovu, ikiwemo CCM wenyewe. Kama unabisha muulize Ndugai.
 
Ndio mtu aliyekuwa na sifa sahihi za kuwa speaker akifuatiwa na Zungu.

Kwa mara ya kwanza mama kapatia; nafasi ya speaker traditional ni ya mmbunge mwenye uzoefu wa kuendesha bunge.

Mengine ushabiki wa Kishamba; hakuna speaker asiyekuwa mmbunge duniani.
 
Nonsense!
Ila from CCM ilikuwa Tulia au Mwijaku, na iwe watakavyo, maigizo yaendelee
 
Ndio nasema tatizo mnahangaika na chadema Sana mpaka mnapambana hata asipokiwepo. Yani unatunga sheria ili tu kuiumiza CHADEMA na wala huwazi kwamba Bunge Ni chombo kinachowakilisha wananchi na sio kikao Cha chama Cha mapinduzi?. Endeleni kupambana na chadema kwa kuteka mihimili yote mwisho wa siku wananchi ndio wanaoumia kwa sheria mbovu, ikiwemo CCM wenyewe. Kama unabisha muulize Ndugai.
Hujanisoma
 
Chadema wamekereka sana....maana wanaujua moto wa Dr. sio wa mchezo mchezo.
Yaani Dr. KAJAAA TELE kwenye kiti....
Yaani anatosha na chenji inabaki.
 
Itapigwa huko huko iliko sheria si zinatungwa bungeni

Ndio nasema tatizo mnahangaika na chadema Sana mpaka mnapambana hata asipokiwepo. Yani unatunga sheria ili tu kuiumiza CHADEMA na wala huwazi kwamba Bunge Ni chombo kinachowakilisha wananchi na sio kikao Cha chama Cha mapinduzi?. Endeleni kupambana na chadema kwa kuteka mihimili yote mwisho wa siku wananchi ndio wanaoumia kwa sheria mbovu, ikiwemo CCM wenyewe. Kama unabisha muulize Ndugai.
Chaguo sahihi! CCM ni chemichemi yenye hazina kibao!!!

Hiyo hazina mbona haijawahi kuonekana?. Mimi tangu aunge mkono COVID 19 nilimtoa kwenye watu wa maana. Mtu yupo against haki huyo yupo kutengeneza CV na kula kwa urefu wa kamba zake.
 

Akiongea na wanahabari, msemaji wa Chama cha Mapinduzi, Shaka Hamdu Shaka amesema chama kimeptisha Tulia Acksoni kuwa mgombea wa kiti cha uspika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia soma: Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


PERSONAL DETAILS
Surnname:
Mwansasu
Middle Name: Ackson
First Name: Tulia
Salutation: Hon. Dr
Marital Status: Married
Date of Birth: 23 Dec. 1976
Place of Birth: Tukuyu Mbeya.
Sex: F
Email: tuliaj@gmail.com
Postal Address: 35093 Dar es Salaam


EDUCATION BACKGROUND
1984 - 1990 Mabonde Primary School Primary Education
1991 - 1994 Lolera Secondary School CSE
1995 - 1997 Zanaki Secondary School ACSE
1998 - 2001 University of Dar es Salaam LLB
2001 - 2003 University of Dar es Salaam LLM
2005 - 2007 University of Cape Town Ph. D

EMPLOYMENT EXPERIENCE
2011 - 2015 University of Dar es Salaam Senior Lecturer
2009 - 2015 University of Dar es Salaam Associate Dean
2001 - 2001 Attorney General's Office Trainee

HOBBIES
Reading Books
Physical Exercises

View attachment 2089489
Kitinda Mimba Tulia Ackson, amezaliwa 23 Novema 1976 Katika Kijiji cha Bulyaga, Kata ya Tukuyu, wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwenye familia ya Akson Mwansasu akiwa ni mtoto wa 11

Alianza safari yake ya Masomo katika Shule ya Msingi Mabonde, Tukuyu, Rungwe mkoani Mbeya.

Elimu ya sekondari alisoma katika Shule ya Wasichana ya Loleza iliyoko jijini Mbeya, barabara ya kwenda Mtaa wa Ghana alikohitimu kidato cha nne.

Alijiunga na Shule ya Wasichana ya Zanaki ambako alimalizia masomo yake ya kidato cha sita mwaka 1997.

Mwaka 1998 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kitivo cha sheria na kufanikiwa kuhitimu chuoni hapo. Alitunukiwa shahada ya sheria mwaka 2001.

Mwaka huohuo wa 2001, Chuo hicho Kikuu cha Dar es Salaam kilimtaka kubaki chuoni hapo kwa ajili ya kufundisha sheria, hivyo alifundisha huku akiendelea kusaka shahada ya uzamili.

Akiwa bado anafundisha chuoni hapo, mwaka 2003 alimaliza masomo kabla ya kufanya mtihani wa uwakili wa kujitegemea mwaka 2004. Mwaka 2005 alijiunga na Chuo Kikuu cha Cape Town nchini Afrika Kusini kufanya shahada ya uzamivu na kufanikiwa baada ya miaka miwili.

Mwaka 2008 alikwenda chuo cha Max Planck Institute for International and Social Law cha Munich, nchini Ujerumani alikokuwa akifanya ‘post doctoral research’.

Mwaka 2009 alirudi nchini katika ajira yake ya awali ya ualimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na aliteuliwa kuwa Makamu Mkuu wa Shule Kuu ya Sheria, nafasi ambayo alikuwa nayo mpaka mwaka 2014.

Kutoka wajumbe wa elimu ya juu, Dk. Tulia alikuwa miongoni mwa wajumbe 201 walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete wa Awamu ya Nne katika Bunge la Katiba lililofanyika kwa awamu mbili.

Awamu ya kwanza lilifanyika kuanzia Februari 18, 2014 hadi Aprili 25, 2014. Kwa siku 21 za kwanza alikuwa miongoni mwa wajumbe waliotunga kanuni za Bunge hilo lililoongozwa na Mwenyekiti Samwel Sitta na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan.

Mwaka huohuo wa 2014 aliteuliwa na Chuo Kikuu cha Bayreuth cha nchini Ujerumani ili kufanya utafiti kuhusu hifadhi za jamii, utafiti uliojulikana kama Awarded the Alexander Von Humboldt Research Fellowship.

Hata hivyo, utafiti huo aliufanya kwa kipindi cha miezi sita tu, kwani akiwa katika mapumziko, ndipo alipoteuliwa tena na Kikwete kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Septemba 9, 2014

Amekuwa naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kipindi cha miezi miwili tu kutokana na Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Magufuli, kutengua uteuzi huo na kumteua kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, akiwa ni mbunge wa kwanza kati ya nafasi 10 za wabunge aliopewa Rais kwa mujibu wa sheria.

Kati ya kazi nzito alizofanya akiwa Mwanasheria Mkuu ni kuongoza jopo la mawakili wa Serikali katika kesi maarufu kwa jina la mita 200, kwani kulitokea mvutano baina ya vyama vya upinzani na Serikali katika kutafsiri sheria ya umbali wa wananchi kukaa mara baada ya kupiga kura.

Mahakama Kuu ilitafsiri sheria hiyo kwa kuagiza wapiga kura kukaa mbali kwa zaidi ya mita hizo baada ya kuridhishwa na hoja za upande wa Serikali ambako Dk. Tulia alikuwa kinara kwa kutaka korti iamue hivyo.

Alhamisi Novemba 19, 2015 wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walipiga kura ya kumchagua Tulia kuwa Naibu Spika wa Bunge hilo. Uchaguzi huo ulifanyika mapema asubuhi ndani ya Ukumbi wa Bunge. Katika uchaguzi huo, Dk. Tulia (CCM) alipata kura 250 kati ya 351 za wabunge wote, huku mpinzani wake, Magdalena Sakaya (CUF) akipata kura 101.

Dk. Tulia ambaye ameolewa na James Andilile na wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume

2020 alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini
Naona sirikali haitaki mtu wa kuweza kuisimamia ipasavyo
 
Chadema wamekereka sana....maana wanaujua moto wa Dr. sio wa mchezo mchezo.
Yaani Dr. KAJAAA TELE kwenye kiti....
Yaani anatosha na chenji inabaki.

Acha kusifia vitu visivyostahili sifa. Huyo kibaraka ana Moto gani?. Mnasifia kinafiki tuu mkijua CHADEMA haipo bungeni, na Sasa bunge litasimamiwa na serikali. Mtapata machungu zaidi ya tozo. Muulize mtesaji wa CHADEMA ndugai kilichomtokea.
 
Tutamshtaki kwa mwenye nchi ili amuondoe.

"Tanzania na vyote vijazavyo ni mali ya Mungu"
 
Huyu tayari anamgwaya hangaya, kwa hiyo hana jipya zaidi ya kuwekwa mfukoni.......ni kupotezeana muda tu.
 
Back
Top Bottom