Dkt. Tulia asikitishwa na kuumizwa sana na kifo cha kada wa CHADEMA. Asema anakichukia Kifo

Dkt. Tulia asikitishwa na kuumizwa sana na kifo cha kada wa CHADEMA. Asema anakichukia Kifo

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Huu ni ujumbe wa speaker wetu wa Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Mbunge wa Mbeya Mjini na ambaye pia ndiye Rais wa umoja wa Mabunge Duniani Mheshimiwa Daktari Tulia Ackson Mwansasu.

Naweka ujumbe wake kama ulivyo bila kuongeza neno wala nukta.

Lakini kwa msioelewa kiingereza vizuri ni kuwa amemaanisha ya kuwa anakichukia kifo yaani I hate Death. Lakini pia akasema kuwa kwa yeyote aliyeshiriki au kuhusika na kukatisha uhai au maisha yako atalipa gharama. Neno Partook ni sawa na neno involved yaani aliyeshiriki au kuhusika katika kifo hicho kwa hakika atalipa gharama au waweza sema atawajibika yaani vyovyote vile unavyoweza kusema,ndio maana ya maneno Surely should pay Dearly.

Screenshot_20240909-225429_1.jpg

Pia Soma
- Spika wa Bunge la Tanzania kwa heshima yake alitakiwa ajiuzulu, analidhalilisha bunge

- Spika Tulia: Tusiweke mazingira ya kuonesha kuwa kila anayepotea amechukuliwa na Vyombo vya Dola. Tusitumie mihemko
 
Ndugu zangu Watanzania,

Huu ni ujumbe wa speaker wetu wa Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Mbunge wa Mbeya Mjini na ambaye pia ndiye Rais wa umoja wa Mabunge Duniani Mheshimiwa Daktari Tulia Ackson Mwansasu.

Naweka kama ujumbe wake kama ulivyo bila kuongeza neno wala nukta.
View attachment 3091984

Pia Soma
- Spika wa Bunge la Tanzania kwa heshima yake alitakiwa ajiuzulu, analidhalilisha bunge

- Spika Tulia: Tusiweke mazingira ya kuonesha kuwa kila anayepotea amechukuliwa na Vyombo vya Dola. Tusitumie mihemko

Kwani kashapata taarifa kama watu wanatekwa na kuuawa? Si alisema bado hajapata taarifa?
 
Huyu dada mnafiki aliyezuia mjadala wa Utekaji Bungeni atavuna anachopanda, Hatokuwa Spika milele

Muda Utaongea
Kwani wewe ndio ulimchagua u speaker? Kama Dunia nzima imemkubali mpaka kumpa urais wa IPU wewe ni nani mpaka uzuie ushindi wake?
 
Utakimbia JF kama Wachawi wenzako walivyokimbia
Utasubiri sana ndugu yangu.si ni wewe uliniambiaga kuwa kufikia mwezi wa 11 mwaka 2022 nitakuwa nimepotea na kukimbia humu jukwaani? Au umesahau maneno hayo? Je ni mwezi wa ngapi huu? Ni mwaka gani huu?
 
Back
Top Bottom