Uchaguzi 2020 Dkt. Tulia atema cheche Mbeya Mjini, awajibu Lissu na Sugu kuhusu maendeleo ya vitu watu wafurika mkutano wake

Uchaguzi 2020 Dkt. Tulia atema cheche Mbeya Mjini, awajibu Lissu na Sugu kuhusu maendeleo ya vitu watu wafurika mkutano wake

Sugu apambane, huyu mama inaonesha atazingua.. Niko mbeya naona hilo! Kamanda akaze buti, ukiwa nje ya Mbeya utaona mtelezo kwa Joseph ila hali sio nzuri kwake inaonesha kuna kujisahau kipindi hiki alichomaliza, watu kama wanataka jambo jipya
 
Kweli kabisa .umewajibu vyema.Kama hawataki ndege wasipande ndege zetu wabande nyongo wanapoenda Kwenye kampeni.na wasitembee na magari kupitia Barabara zetu wapite maporini.

Eeeweeeee mtanzania usidanganyike .Hizo ni mbinu walizokuja nazo baada ya kuishiwa hoja.wanajua mtanzania ni mwepesi wakudanganika maana tunapenda maneno na dezo.zinduka
 
Hongera CCM kwa kuwa na watu makini kama huyu Mama, nimemuona pia mgombea wa jimbo la Bukoba mjini mh! kwali hiki ndio chama tawala!
 
Ahahahahahahah!
Ila uunguana wa kawaida ni kukosoana bila kumundermine au kumuderrate mwenzako! Hata kwenye pointless kuna point!
Kwa mfano, jamaa amesema kitu kizuri tu, kwamba hotel ya Sugu, ni maendeleo ya Mtu, yamepelekea kuwa na vitu! Lakini kwa ujumla hoja ya Lissu na wapinzani, ni kipi ni kipaumbele? Je, ujenzi wa flyovers unamsaidiaje mkulima wa Liwale? Ndege zinasaidiaje mwananchi wa kawaida? Kwanini serikali ijiingize kwenye biashara? Mbona serikali haina basi hata moja, lakini watu wanasafiri? Pia wapinzani wana hoji njia, methods, zilizotumika!!
 
Mkuu kwenye maendeleo zinatumika zaidi dhana mbili; Rostow's Stages of Development na Marxist Stages of Development kutegemea una mrengo gani kisiasa. Wote wanakubaliana kwamba Maendeleo ya Watu ndio hatua ya juu kabisa (High Mass Consumption kwa Rostow) na (Communism kwa Marxism) ya maendeleo ya mwanadamu.

Kama ninyi na Lissu wenu mnaweza kutuaminisha tofauti kwamba unaweza kusafiri kwa haraka kati ya Mwanza na Dar (maendeleo ya watu) bila ndege au SGR au watu kuwa na umeme wa uhakika (maendeleo ya watu) bila kuzalisha umeme wa kutosha na wa uhakika inawezekana, mimi nitaunga mkono hoja.
 
Nikae kimya kwa lipi mkuu? Mtu anayeona Sugu kujenga hotel ni maendeleo ya vitu?
Ni ujinga kudhani una2eza kuendelea bila kuwa na miundo mbinu. Kama ni hivyo mchagueni Cheyo wa UDP. Yeye alikuwa anawajaza Mapesa mifukoni.

Hawa wanasiasa wasifikiri kila mtu ni mpumbavu kiasi hicho kwamba, Haulimi, hauna uzalishaji unaowezeshwa na miundombinu halafu una hela, kwahiyo serkali iwe inawapelekea watu hela majumbani.

Huku wanasema hakuna ajira, ajira bila miundo mbinu utaipata wapi?

Yaani wote tuwe watumishi wa Umma, inawezekana?

Huku wanasema Kaua sector binafsi.

Wanadhani wote tunaelewa inaposemwa miundombinu inamaanisha reli, barabara na viwanja tu. SIO

Siko ssm yenu, sitapiga kura, kadi ipo, ILA Upinzani unaonyesha haujakomaa kupewa nchi.
 
Back
Top Bottom