"Ubora wa filamu ya Royal tour ni wa kiwango cha chini kulinganisha na gharama iliyotumika,hata vijana wetu wa bongo movie wangeweza kutengeneza hii filamu, Tanzania ilishajitangaza,tusijidanganye kwamba Royal tour ndio itaitangaza Serengeti/Mlima Kilimanjaro" Dkt.Vicensia Shule
👇
View attachment 2210309
Huku sasa ni kupoteza nini jamani, dira au muelekeo?
Mbona tunakosoa hadi yasiyo tuhusu??
Idea siyo yetu! Filamu siyo yetu! Fedha siyo zetu! Audience lengwa siyo akina sisi!
Sasa kama watengenezaji wenyewe wanatamka wazi kwamba hii ya SSH imekuwa bora zaidi kuliko RT zingine za nyuma sisi ni nani tukatae?
Nadhani kuna wengi hawajui mengi kuhusu Royal Tour. Labda kuna scenes watu walishazizoea basi hawazioni kwenye hii RT.
Mimi nishashiriki maandalizi ya promotional video kwa ajili ya watalii wa dunia ya leo... mtaalamu mmarekani alikazia kuwa iwe very organic as possible, casual na siyo scifi ~science/fictional. Niche ya watalii na wawekezaji wenye fedha zao wanaokuja TZ ni retired veterans. Peter Greenberg wa RT anajua wanataka nini na awapa wanachokita! Nadhani hapo RT wamefanikiwa!
Zaidi ya yote nyuma yake kuna nguvu kubwa sana... Kufanya RT na viongozi wa nchi si jambo la mchezo!
Sisi tuachane kabisa na hoja za ubora turudi kwenye hoja za msingi.
Tufukunyue kuhusu nani yupo nyuma ya harakati za kumuondoa Masai Ngorongoro. Je, ule ujenzi wa mtandao wa mahoteli ya kifahari hifadhini ni muendelezo wake?
Je, hizi harakati za RT zinahusika? Kwa gharama za nani, faida ya nani, ili iwe nini?
NB: Pale unapohisi bidhaa yako inafahamika basi ni wakati wa kuzidisha matangazo!