Dodi Al Fayed mchumba wa Princess Diana mpaka Kifo!

Ni kweli,habari zilitrend juzijuzi tu hapa,Mambo ya kina Diana na Dodi Al Fayed na Charles na Camilla Parker bowel,leo twamuongelea Charles kibabu! Ama kweli maisha ya duniani ni mafupi sana
 
Mohamed Al Fayed hajawahi kuwa raia wa Uingereza. Alikuwa anaishi na kufanya biashara UK lakini hakuwahi kupewa uraia. Jambo ambalo alikuwa akilalamika sana.
 
King Charles na Camilla walianza mahusiano yao kabla hata hajalazimishwa kumuoa Diana. Ulipofika muda wa Charles kuoa familia ikamkataa Camila wakidai eti "she has been quiet around" kwa maneno mengine "alikuwa ametumika sana".

Charles alipata presha kali kutoka kwa baba yake Phillip amuoe Diana ambaye alikuwa mwali. Ili kumtoa Camila mchezoni, ukasukwa mpango Camila akaolewa na Ofisa wa jeshi aitwaye Parker Bowles. Lakini yote yalishindikana, Camila hakukaa sana kwenye ndoa yake wakaachana na mumewe na wakaliendeleza libeneke na Charles. Fujo ndio zikaanzia hapo.
 
Kuchanganya damu ni haramu ?
 
Huyo kasoma kitabu kilichotungwa tu maana Chaz alianza mahusiano na Camilla wakati Di alikuwa na miaka 10 tu maishani
 
Diana nafikiri alikuwa na pepo la ngono. Kuna uwezekano mkubwa Harry siyo mtoto wa Charles.
Hamna kitu kama hicho we kijana. Wenzetu kule wameendelea sana na mtoto hata kabla ya kuzaliwa wanapata DNA zake

Mtoto akizaliwa pia anachukuliwa DNA hapo hapo.
 
Baba yake dodi alikuwa mmiliki WA fulham. Mwanae ndio alikuwa anatoka na Diana. Na hadi alipeleka kesi mahakamani kuwa utawala WA uingereza umemuua mtoto wake.....
 
Nadhani walikuwa wameshaachana na Charles kipindi hiko.... Kama sijakosea
 
Dada yake kivipi wakati mwamba ana mtoto?
 
CIA tena how? Nikajua wale MI5 au kwa kukuwa alifia hospital la wamarekani?
 
Na mchezo ukaendelea Andrew Parker Bowles akatembea na Princess Anne Dada yake Chaz haha
 
Bilionea Mohamed Ibrahim au kama wao wanavyopenda kumuita Mo Ibrahim ni Mwingereza mwenye asili ya Sudan kww kuzaliwa na si Egypt.
Mo Ibrahim ni Msudani na sio Mmisri
Na hakuna matajiri wakubwa hapa wamisri
Mo Saleh mcheza mpira na Al Fayed alibebwa na shemeji yake Adnan Khashoghi ambae alikuwa Billionaire la Saudia ambae historia yake alianza kuuza mashuka alipokuwa anasoma Egypt Chuo kikuu
Ni akili ya tangu mdogo
 
Mkuu Dada yake hawezi kuwa Malikia maana next to the throne ni mwanae William halafu mtoto wa William ambae ni Prince George of Wales ndio atakuwa Mfalme baadae kama atafika

Huoni protocol ilivunjwa walisema George asiletwe kwenye jeneza ila wazee wa maamuzi wakasema ni lazima awepo maana anamfuatia baba yake kurithi kiti ni vizuri akaona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…