Dodoma: Adaiwa Kumuua Mkewe kwa kumchoma kitu chenye ncha kali shingoni

Dodoma: Adaiwa Kumuua Mkewe kwa kumchoma kitu chenye ncha kali shingoni

TAHARUKI imetanda katika Mtaa wa Mailimbili Darajani, jijini Dodoma, kufuatia tukio la mwanamume anayedaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali shingoni.

Marehemu ametambuliwa kwa jina la Shukran Riziki (30) na mtuhumiwa ni Khatibu Mfaume, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 39.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, tukio hilo linadaiwa kutokea jana, huku wanandoa hao wakitajwa kuwa na historia ya kugombana mara kwa mara.

Baada ya tukio hilo, Mfaume anadaiwa kwenda kunywa pombe kabla ya kurejea nyumbani na kulala karibu na mwili wa mkewe.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa asubuhi ya leo, Oktoba 9,2026 mtuhumiwa alikwenda kujisalimisha katika kituo cha polisi cha kata kabla ya kuhamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma.

Tayari Jeshi la Polisi limefika katika eneo la tukio kwa ajili ya kuuchukua mwili wa marehemu na kuendelea na taratibu za uchunguzi.


View: https://www.instagram.com/p/DeRweoOqJ_w/

Hata hivyo, maelezo hayo ni ya awali na sababu kamili za tukio hilo bado hazijathibitishwa rasmi.

Soma Pia: Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam


Here we go again.
 
Hii miezi Wanaume wenzangu hebu tuchukue mapumziko twende hata hapo Forodhani tukale urojo, ili kama kuna pepo linatuandama la kuua wenza wetu lishindwe na lilegee

It doesn't make sense to kill your beloved wife whom you promised, you will protect to death

Uko wapi ule upendo wa mwanzoni wakati ambapo majina ya honey, sweetheart, nyonga mkalia ini yalikuwa hayakauki midomoni mwetu?

Haijalishi amekukosea kwa kiwango gani, hastahili kulipwa kifo.

Wanandoa Mungu atusaidie, huyu shetani anayetunyemelea kwa kuua wenza wetu ashindwe na alegee
Mzee mwenzangu wanaume tuna shida sio siri,tumekuwa dhaifu mno, eti kiumbe mwanamke ni wa kumchoma kisu au kumpiga risasi kweli?

Uko wapi uanaume wetu,ipo wapi hekima na busara ya kichwa cha familia?

Haya unakomoa mpaka watoto sasa,hapo mama kafa halafu baba unaenda jela,huu kama si ujinga ni nini?
 
Back
Top Bottom