Dodoma: Adaiwa Kumuua Mkewe kwa kumchoma kitu chenye ncha kali shingoni

TAHARUKI imetanda katika Mtaa wa Mailimbili Darajani, jijini Dodoma, kufuatia tukio la mwanamume anayedaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali shingoni.

Marehemu ametambuliwa kwa jina la Shukran Riziki (30) na mtuhumiwa ni Khatibu Mfaume, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 39.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, tukio hilo linadaiwa kutokea jana, huku wanandoa hao wakitajwa kuwa na historia ya kugombana mara kwa mara.

Baada ya tukio hilo, Mfaume anadaiwa kwenda kunywa pombe kabla ya kurejea nyumbani na kulala karibu na mwili wa mkewe.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa asubuhi ya leo, Oktoba 9,2026 mtuhumiwa alikwenda kujisalimisha katika kituo cha polisi cha kata kabla ya kuhamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma.

Tayari Jeshi la Polisi limefika katika eneo la tukio kwa ajili ya kuuchukua mwili wa marehemu na kuendelea na taratibu za uchunguzi.

Hata hivyo, maelezo hayo ni ya awali na sababu kamili za tukio hilo bado hazijathibitishwa rasmi.

Soma Pia: Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam

Iko shida kubwa kwenye jamii haya mambo tusiyachkulie poa ,Mungu tusaidie haya mambo yasiwepo kwenye hii jamii ya watanzania
 
TAHARUKI imetanda katika Mtaa wa Mailimbili Darajani, jijini Dodoma, kufuatia tukio la mwanamume anayedaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali shingoni.

Marehemu ametambuliwa kwa jina la Shukran Riziki (30) na mtuhumiwa ni Khatibu Mfaume, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 39.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, tukio hilo linadaiwa kutokea jana, huku wanandoa hao wakitajwa kuwa na historia ya kugombana mara kwa mara.

Baada ya tukio hilo, Mfaume anadaiwa kwenda kunywa pombe kabla ya kurejea nyumbani na kulala karibu na mwili wa mkewe.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa asubuhi ya leo, Oktoba 9,2026 mtuhumiwa alikwenda kujisalimisha katika kituo cha polisi cha kata kabla ya kuhamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma.

Tayari Jeshi la Polisi limefika katika eneo la tukio kwa ajili ya kuuchukua mwili wa marehemu na kuendelea na taratibu za uchunguzi.

Hata hivyo, maelezo hayo ni ya awali na sababu kamili za tukio hilo bado hazijathibitishwa rasmi.

Soma Pia: Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam

Ilaumiwe CCM milele. Haya yote yanasababishwa na ugumu wa maisha watu wanachanganyikiwa sana na maisha magumu huku maccm yakifanya ufisadi tu
 
Aisee!

Kama migogoro imezidi ndani ya ndoa jipeni mapumziko.

Kila mtu aende kwao, si kila mtu ana kwao??
 
Mzee mwenzangu wanaume tuna shida sio siri,tumekuwa dhaifu mno, eti kiumbe mwanamke ni wa kumchoma kisu au kumpiga risasi kweli?

Uko wapi uanaume wetu,ipo wapi hekima na busara ya kichwa cha familia?

Haya unakomoa mpaka watoto sasa,hapo mama kafa halafu baba unaenda jela,huu kama si ujinga ni nini?
Kwa kweli tunaonesha udhaifu mkubwa sana

Watu kama mapenzi yameisha, vyema kuachana kwa amani kuliko kuuana kama hivyo

Kuna haja tubadirike Wanaume, haya mambo ya kuuana, tunawatesa watoto

Maana Mama amekufa, na Baba atafungwa jela maisha

Then watoto wanabaki wapweke
 
Back
Top Bottom