Dodoma: Adaiwa Kumuua Mkewe kwa kumchoma kitu chenye ncha kali shingoni

Dodoma: Adaiwa Kumuua Mkewe kwa kumchoma kitu chenye ncha kali shingoni

Afya ya akili na mihemko inachangia..!!
Kuna mmoja ka comment huko juu et here we go anajiona mwamba kumbe jinga la mwisho na mihemko ipo juu kuliko ufanisi wa akili
Si umeona hapa jukwaani baadhi ya wanaume wanamsifu Kweka bila aibu.
Vipi huko mtaani kwenye vijiwe?

Wanapeana ushauri mbovu na hao vichaa kwa mihemko yao wanatekeleza wakijua ndo UANAUME kumbe ni upumbavu..!!
Sikujua kama watu wengi wana tatizo la afya ya akili
 
Mimi naona hii athabu ya kufungwa cjui miaka 30 haifai kwa makosa kama haya

In short aliyeua auwawe
 
TAHARUKI imetanda katika Mtaa wa Mailimbili Darajani, jijini Dodoma, kufuatia tukio la mwanamume anayedaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali shingoni.

Marehemu ametambuliwa kwa jina la Shukran Riziki (30) na mtuhumiwa ni Khatibu Mfaume, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 39.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, tukio hilo linadaiwa kutokea jana, huku wanandoa hao wakitajwa kuwa na historia ya kugombana mara kwa mara.

Baada ya tukio hilo, Mfaume anadaiwa kwenda kunywa pombe kabla ya kurejea nyumbani na kulala karibu na mwili wa mkewe.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa asubuhi ya leo, Oktoba 9,2026 mtuhumiwa alikwenda kujisalimisha katika kituo cha polisi cha kata kabla ya kuhamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma.

Tayari Jeshi la Polisi limefika katika eneo la tukio kwa ajili ya kuuchukua mwili wa marehemu na kuendelea na taratibu za uchunguzi.

Hata hivyo, maelezo hayo ni ya awali na sababu kamili za tukio hilo bado hazijathibitishwa rasmi.

Soma Pia: Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam

Katazo la kufunga ndoa la dharura lipitishwe ndoa zianze kufungwa tena hali itakapokuwa shwari nchi nzima...
 
Afya ya akili na mihemko inachangia..!!

Si umeona hapa jukwaani baadhi ya wanaume wanamsifu Kweka bila aibu.
Vipi huko mtaani kwenye vijiwe?

Wanapeana ushauri mbovu na hao vichaa kwa mihemko yao wanatekeleza wakijua ndo UANAUME kumbe ni upumbavu..!!
Kuna kitu cha kufanya kuwaandaa vijana toka msingi huko kwa ajili ya maisha ya familia - emotional intelligence, familia na malezi, wajibu na haki katika ndoa, etc ni maandalizi muhimu sana hasa hawa Gen Z na watakaofuata. Yaani kuna vijana wanaingia kwenye ndoa bila hata kujua kwanini wanaoana!
 
Sasa si umesikia alienda kulewa akarudi kufanya tukio! 😊
Hukawii kuingiza uchaga hapa wewe!
Lini uliona nikiongelea ukabila mimi
Ukabila na udini ndio upumbavu no moja nisiopenda

Hakuna kisingizio cha kuua mtu hakuna sababu inayotosha kumuua mkeo

Wanaume wenye roho za kuku acheni kujihusisha na mahusiano nendeni mkafie kwenye vibanda vya betting
 
Hii miezi Wanaume wenzangu hebu tuchukue mapumziko twende hata hapo Forodhani tukale urojo, ili kama kuna pepo linatuandama la kuua wenza wetu lishindwe na lilegee

It doesn't make sense to kill your beloved wife whom you promised, you will protect to death

Uko wapi ule upendo wa mwanzoni wakati ambapo majina ya honey, sweetheart, nyonga mkalia ini yalikuwa hayakauki midomoni mwetu?

Haijalishi amekukosea kwa kiwango gani, hastahili kulipwa kifo.

Wanandoa Mungu atusaidie, huyu shetani anayetunyemelea kwa kuua wenza wetu ashindwe na alegee
We bhana.. kusema kuna pepo la taifa linaandama labda tupo pamoja.. Maana damu imemwagika shekhe.!

Mimi nimesikiliza na kuamini kabisa Wife akitongozwa na Mume wa mtu kwa phone ..!? Bora hata angekuwa boda au mla skanka ningesema uchu umemponza wife labda sifanyi vizuri na ningemsamehe.🤔

Eti skrepa mume ba mutu kweli.! Itoshe kusema wife ni mnafiki na malaya aliyetengenezwa kwao kwa wivu mkubwa kuwanyanyua vigagula vya kwao kwa utapeli wa familia na ndoa
 
Lini uliona nikiongelea ukabila mimi
Ukabila na udini ndio upumbavu no moja nisiopenda

Hakuna kisingizio cha kuua mtu hakuna sababu inayotosha kumuua mkeo

Wanaume wenye roho za kuku acheni kujihusisha na mahusiano nendeni mkafie kwenye vibanda vya betting

Basi sawa, nimekuelewa. 😊
 
TAHARUKI imetanda katika Mtaa wa Mailimbili Darajani, jijini Dodoma, kufuatia tukio la mwanamume anayedaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali shingoni.

Marehemu ametambuliwa kwa jina la Shukran Riziki (30) na mtuhumiwa ni Khatibu Mfaume, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 39.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, tukio hilo linadaiwa kutokea jana, huku wanandoa hao wakitajwa kuwa na historia ya kugombana mara kwa mara.

Baada ya tukio hilo, Mfaume anadaiwa kwenda kunywa pombe kabla ya kurejea nyumbani na kulala karibu na mwili wa mkewe.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa asubuhi ya leo, Oktoba 9,2026 mtuhumiwa alikwenda kujisalimisha katika kituo cha polisi cha kata kabla ya kuhamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma.

Tayari Jeshi la Polisi limefika katika eneo la tukio kwa ajili ya kuuchukua mwili wa marehemu na kuendelea na taratibu za uchunguzi.

Hata hivyo, maelezo hayo ni ya awali na sababu kamili za tukio hilo bado hazijathibitishwa rasmi.

Soma Pia: Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam

Ndoa ndio fani pekee yenye cheti ambacho watu wanakipata bila proof of mastery of the art!
 
Back
Top Bottom