Dodoma: Adaiwa Kumuua Mkewe kwa kumchoma kitu chenye ncha kali shingoni

Dodoma: Adaiwa Kumuua Mkewe kwa kumchoma kitu chenye ncha kali shingoni

Ni ujinga mkubwa sana,naomba katika hili wadada muungane mpaze sauti,kemeeni huu ujinga
Nafikiri Hoja ya kusema Wanaume wakemewe na Watu waungane kupaza sauti kupinga ukatili ndio ya KIJINGA kuwahi kuisikia kutoka kwa wanaharakati..

Hakuna dunia yeyote or jamii yeyote ambayo ukatili uliisha au kupungua sababu watu walikatazwa kua makatili na kuacha ukatili,.

human nature na justice kwa mujibu wa tafiti nyingi HAIPO HIVYO KAMWE

Watu wengi wanatenda uovu intentional,Matendo ya ukatili hayatokei kama ajali watu wanajua wanafanya ubaya and they dont care,kama unafikiri wanafanya sababu hawana information POLENI SANA.

Kuwapa elimu au kuwataka waache ni kufikiri kua they care about the same moral boundaries kama wewe,mimi na yule

Wakati uhalisia ni kwamba wamechagua kupuuza hatari itakayowapata wao na wapendwa wao baada ya kutimiza Ubaya wao..

But kuna njia nyingi za kusaidia jamii kupunguza kama sio kumaliza tatizo hili tukiwa tayari tujadili wote hapahapa..

Kitu kibaya zaidi tunajadili sana matokeo but not how we get here,.

bad actors ndio hawa vijana wadogo hatuwapi elimu yeyote ya maana,wanawake wote now wana feel like they're potential victims..
 
Yaan kuna upepo mbaya unapita kwenye mahusiano na ndoa za watu. Wakati huu.
Ukifatilia karibu waliofanya ukatili wa mauaji wengi ni msongo wa mawazo unaosababishwa na mdororo wa kiuchumi, hivh si ndo hawa huwa wanajishaua humu kwamba hawababaishwi na k,,, mbona sasa wanatuua maana kuua mwenzi wako ni kiwango cha mwisho cha udhaifu wa kiakili kimwili nk
 
Ndoa zenye miaka 20 kushuka chini zisitishwe kwa muda, wanandoa wasubiri kupangiwa utaratibu mwingine wa kuishi baada ya kujiridhisha kuwa wapo sawa.
Naunga mkono hoja. Wengi haswa wanaume vichwa haviko sawa kabisa.
 
Ukifatilia karibu waliofanya ukatili wa mauaji wengi ni msongo wa mawazo unaosababishwa na mdororo wa kiuchumi, hivh si ndo hawa huwa wanajishaua humu kwamba hawababaishwi na k,,, mbona sasa wanatuua maana kuua mwenzi wako ni kiwango cha mwisho cha udhaifu wa kiakili kimwili nk
Huko kujishaua ndiko kunatuma ujumbe ni kiasi gani wanababaishwa.
 
TAHARUKI imetanda katika Mtaa wa Mailimbili Darajani, jijini Dodoma, kufuatia tukio la mwanamume anayedaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali shingoni.

Marehemu ametambuliwa kwa jina la Shukran Riziki (30) na mtuhumiwa ni Khatibu Mfaume, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 39.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, tukio hilo linadaiwa kutokea jana, huku wanandoa hao wakitajwa kuwa na historia ya kugombana mara kwa mara.

Baada ya tukio hilo, Mfaume anadaiwa kwenda kunywa pombe kabla ya kurejea nyumbani na kulala karibu na mwili wa mkewe.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa asubuhi ya leo, Oktoba 9,2026 mtuhumiwa alikwenda kujisalimisha katika kituo cha polisi cha kata kabla ya kuhamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma.

Tayari Jeshi la Polisi limefika katika eneo la tukio kwa ajili ya kuuchukua mwili wa marehemu na kuendelea na taratibu za uchunguzi.

Hata hivyo, maelezo hayo ni ya awali na sababu kamili za tukio hilo bado hazijathibitishwa rasmi.

Soma Pia: Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam

Ugumu wa Maisha plus ugonjwa wa akili
 
Jamaa hadi anamzini..inaonekana alikuwa ananyimwa..ila hiyo haiwez kuwa sababu kutoa uhai wa mtu
 
Back
Top Bottom