Dodoma: Adaiwa Kumuua Mkewe kwa kumchoma kitu chenye ncha kali shingoni

Dodoma: Adaiwa Kumuua Mkewe kwa kumchoma kitu chenye ncha kali shingoni

Dunia ya sasa hivi watu wanajiingiza kwenye ndoa kwa ajili ya kunufaika, Ndoa za mkataba ndiyo suluhusho wa mauaji ya wanandoa, Maana kama kuna sintofaham yoyote katika kipindi cha mkataba, basi huwo mkataba usitishwe Mara moja.
Yes. Akina Ke waanze sasa kuachana na Tabia ya kuwa ving'ang'anizi eti "tumechuma hizi mali kwa pamoja" :KEKBye:
 
TAHARUKI imetanda katika Mtaa wa Mailimbili Darajani, jijini Dodoma, kufuatia tukio la mwanamume anayedaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali shingoni.

Marehemu ametambuliwa kwa jina la Shukran Riziki (30) na mtuhumiwa ni Khatibu Mfaume, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 39.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, tukio hilo linadaiwa kutokea jana, huku wanandoa hao wakitajwa kuwa na historia ya kugombana mara kwa mara.

Baada ya tukio hilo, Mfaume anadaiwa kwenda kunywa pombe kabla ya kurejea nyumbani na kulala karibu na mwili wa mkewe.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa asubuhi ya leo, Oktoba 9,2026 mtuhumiwa alikwenda kujisalimisha katika kituo cha polisi cha kata kabla ya kuhamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma.

Tayari Jeshi la Polisi limefika katika eneo la tukio kwa ajili ya kuuchukua mwili wa marehemu na kuendelea na taratibu za uchunguzi.

Hata hivyo, maelezo hayo ni ya awali na sababu kamili za tukio hilo bado hazijathibitishwa rasmi.

Soma Pia: Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam

Zamu ya kobaz sasa hivi.

hydroxo Makebo
 
Kila kona kuna mambo ya moto...wahaya nao wapooo
 

Attachments

  • IMG-20261008-WA0064.jpg
    IMG-20261008-WA0064.jpg
    77.7 KB · Views: 4
Hakuna aliyemloga bali Me kajiloga mwenyewe. Mwanaume unaenda kujitundika dripu(Pombe) halafu unarudi nyumbani etti kufanya maamuzi ya jambo zito la kifamilia - unategemea nini? Kuumbaf' sana.
Sad, he'll spend the rest of his fucking life behind bars until the law states otherwise.
 
Back
Top Bottom