Sio kwamba dini, imani, the so called kiroho zimefeli?
Yamkini wewe ni miongoni mwa wahanga wa kutoelewa kwa nini Yesu aliacha enzi yake mbinguni akaja duniani. Ndio maana huoni tofauti Kati ya Dini/Imani na Wokovu.
Kwa faida yako ni kwamba Dini or the so called Imani has nothing to do with setting individuals free from spiritual slavery. Mtu akiwa mtumwa anatenda mambo ambayo hayapendi ndio kama haya ya kuua halafu baadae unaanza kujutia.
Utumwa wa kiroho ndio anguko la Mwanadamu lilipo bila kujali status yake!
WARUMI 7
14 Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi.
15 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.
16 Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema.
17 Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu
18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.
19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.
20 Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
YOHANA 8
36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.