Azimio la Bunge kuhusu Pendekezo la Kuridhiwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii katika Uendelezaji wa Maeneo ya Bandari Nchini leo Juni 10, 2023.
======
Leo Juni 10, 2023, Bunge la Tanzania linatarajia kujadili mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya DPWorld unaodaiwa kutotaja ukomo kuhusu Ushirikiano katika Uendeshaji, Uendelezaji na Uboreshaji wa Bandari zote za Baharini na Maziwa zilizopo Tanzania Bara
Mkataba umeibua maswali ambayo hayajapatiwa ufafanuzi wa kina ikiwemo thamani na muda wa uendeshaji pamoja na sababu za Tanzania kuingia mkataba na kampuni inayotajwa katika kesi za ukwepaji kodi na migogoro katika utekelezaji mikataba huku baadhi ya Nchi zikiikataa kampuni hiyo.
Je, unaufahamu kiasi gani Ushirikiano wa DP-World na Bandari?
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anawasilisha Pendekezo la Kuridhiwa kwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anawasilisha Pendekezo la Kuridhiwa kwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii katika Uendelezaji wa Maeneo ya Bandari Nchini, leo Juni 10, 2023
Prof. Mbarawa anasema "Pamoja na kuchukua hatua mbalimbali za maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam, bado ufanisi katika utoaji Huduma za haujafikia viwango vinavyotakiwa kimataifa.”
Anaongeza “Hali ya sasa ya utendaji imeendelea kuwa ya kiwango cha chini ikilinganishwa na Bandari shindani kikanda. Kwa mfano, wastani wa meli kusubiri nangani kwa Bandari ya Dar es salaam ni Siku 5 ikilinganishwa na Siku 1.25 kwa Bandari ya Mombasa na siku 1.6 kwa Bandari ya Durban.”