Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Prof. Mbarawa kama amekiri kuwa usimamizi wa bandari upo chini Kwanini asijiuzulu kumpisha mzawa Dr Charles Kimei?
 
Mpina yuko kimya anaandaa nondo wala hagongi meza sijui kama spika atamnyanyua.
 
Hivi wabunge wanaposema jirani anafanya vizuri kwenye bandari,naye amewaita DP? Au waliwekeza akili za wananchi wao?
 
Kuna bomu linaandaliwa na Mpina hapa nadhani hili litakuwa ni ICBM, sijui atapona nani
 
Mbunge amethibitisha kuwa mkataba huu ni kweli hauna mkomo na auna ukomo kwa manufaa ya watanzania

Kwa hiyo ni kweli mkataba ni wa milele
 
Pona pona ya hili taifa ni pale tu wananchi watakapo tambua CCM ni adui wa hii nchi anaye takiwa kupingwa kwa nguvu zote.
Lasivyo tusilaumu maana ujinga wetu na njaa zetu ndio nguzo yao kuu ya kuendelea kubaki hapo walipo sasa.
 
Anaongeza “Hali ya sasa ya utendaji imeendelea kuwa ya kiwango cha chini ikilinganishwa na Bandari shindani kikanda. Kwa mfano, wastani wa meli kusubiri nangani kwa Bandari ya Dar es salaam ni Siku 5 ikilinganishwa na Siku 1.25 kwa Bandari ya Mombasa na siku 1.6 kwa Bandari ya Durban
Mbarawa atuambie Bandari ya Mombasa na Durban zinaendeshwa na DP World hadi zikafikia huo ufanisi?

Kwa nini Bandari za Zanzibar hazihusishwi kwenye mkataba?
 
Back
Top Bottom