Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Naona umuhimu wa wapinzani kuwapo bungeni, Magufuli umetuletea balaa kwa kupitisha pitisha wabunge wa ccm kwa mabavu
Wabunge wenyewe vilaza kama kina babu......aibu tupu.

Lengo la Jiwe lilikuwa ni nn hasa kupitisha watu wale kuwa wagombea na kuwa Wabunge? Mbaya zaidi ni kuhakikisha Bunge kuwa ni la Chama kimoja na alilenga nn hasa kwenye hilo?? Huu upuuzi unaoendelea hivi sasa chimbuko lake yaweza kuwa ni yeye mwenyewe. Kwanini Msukuma kawa kinara wakulitetea??
 
Azimio la Bunge kuhusu Pendekezo la Kuridhiwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii katika Uendelezaji wa Maeneo ya Bandari Nchini leo Juni 10, 2023.



======

Leo Juni 10, 2023, Bunge la Tanzania linatarajia kujadili mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya DPWorld unaodaiwa kutotaja ukomo kuhusu Ushirikiano katika Uendeshaji, Uendelezaji na Uboreshaji wa Bandari zote za Baharini na Maziwa zilizopo Tanzania Bara

Mkataba umeibua maswali ambayo hayajapatiwa ufafanuzi wa kina ikiwemo thamani na muda wa uendeshaji pamoja na sababu za Tanzania kuingia mkataba na kampuni inayotajwa katika kesi za ukwepaji kodi na migogoro katika utekelezaji mikataba huku baadhi ya Nchi zikiikataa kampuni hiyo.

Je, unaufahamu kiasi gani Ushirikiano wa DP-World na Bandari?

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anawasilisha Pendekezo la Kuridhiwa kwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anawasilisha Pendekezo la Kuridhiwa kwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii katika Uendelezaji wa Maeneo ya Bandari Nchini, leo Juni 10, 2023

PROF. MAKAME MBARAWA
"Pamoja na kuchukua hatua mbalimbali za maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam, bado ufanisi katika utoaji Huduma za haujafikia viwango vinavyotakiwa kimataifa.”

“Hali ya sasa ya utendaji imeendelea kuwa ya kiwango cha chini ikilinganishwa na Bandari shindani kikanda. Kwa mfano, wastani wa meli kusubiri nangani kwa Bandari ya Dar es salaam ni Siku 5 ikilinganishwa na Siku 1.25 kwa Bandari ya Mombasa na siku 1.6 kwa Bandari ya Durban.”

"Ufanisi mdogo wa Bandari ya Dar umetokana na changamoto ikiwemo kukosekana kwa Mifumo ya kisasa ya TEHAMA, maeneo ya kutosha ndani na nje ya Bandari kwa ajili ya kuhifadhia shehena, Maegesho ya Meli, mitambo ya kutosha na ya kisasa ya kuhudumia shehena ambayo ina gharama kubwa ya Uwekezaji.”

“Meli kutumia muda mrefu kupakia na kupakua shehena gatini kwa wastani wa Siku 5 ikilinganishwa na Siku 1 inayokubalika Kimataifa, pamoja na Meli kubwa kutokuja katika Bandari ya Dar kutokana na kuchukua muda mrefu kuhudumiwa


Sasa halima mdee akili imerudi
 
Wabunge walioko bungen kwao aya mambo yako juu ya uwezo wao , mbunge anasema wenzetu wanapakua mizigo kwa siku tatu tena majirani , sasa si watume watu wajue why iko hivyo , badala yake mnakimbia mpa mwarabu why msimpe mkenya ambae inaonesha amekua na ufanisi katika endesha bandari zake , hamna akili
Mimi mbunge wangu simlaumu sababu najua ni darasa la nne hivyo haya mambo kwake ni makubwa sana. Uchaguzi wa 2020 unatuletea shida sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namwona Mpina kwa mbali akiwa ananukuu kipengele kwa kipengele.

Atakaposimama tu anasambaratisha Bunge zima.
 
Hizi Mahakama za CCM nani aziamini? zimeshindwa kuwaondoa Wabunge haramu 19 waliofukuzwa Bungeni zinamsubiri Mwenyekiti wa CCM aziamrishe.

Invester anayeingiza Millions of Dollars ya mtaji wake si akizulumiwa ndio utegemee atapewa haki na hizo Mahakama za Lumumba?
Za South Afrika je ambazo zimeshindwa kumwajibisha zuma kwa kuwakabidhi nchi wale wahindi ndizo zitaweza hili. Narudia tena hapa shida ni vipengele au kutoelewa kwa wananchi. Na sioni shida kwanini wizara isingeleta wataalamu wakafanya mdaharo hata ITV wakafafanua na watu wakauliza maswali kuliko mara tutawachukulia hatua mara msigwa ajichangamye figures.
Inawezekana ni wananchi kutoelewa masuala ya kitaalam sasa ni juku la serikali kuwaelewesha
 
Back
Top Bottom