Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Hivi Nape huwa hajui kutoa hoja kulingana na mada husika, yeye yupo kutisha watu tyuuh, ko Mbowe asiseme ukweli kisa maridhiano? Ko maridhiano yalikua ili awe kimya kwa mambo ya kitapeli km mkatabaa huu??

Afu haoni aibu anafananisha mkataba wa bomba LA mafuta na huu wa bandarii, khaaah

Hivi ana Elimu gani huyu Nape?? Mxxxiiiiieeeeeewwwww
Kwanza mkataba wa Bomba la mafuta niwausafirishaji tu kama Bomba la mafuta Zambia na reli ya TAZARA ila swala la Bandari ni kukabizi sisi tuondoke kwenye majukumu ya usimamizi waingie waarabu.
 
Azimio la Bunge kuhusu Pendekezo la Kuridhiwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii katika Uendelezaji wa Maeneo ya Bandari Nchini leo Juni 10, 2023.

======

Leo Juni 10, 2023, Bunge la Tanzania linatarajia kujadili mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya DPWorld unaodaiwa kutotaja ukomo kuhusu Ushirikiano katika Uendeshaji, Uendelezaji na Uboreshaji wa Bandari zote za Baharini na Maziwa zilizopo Tanzania Bara

Mkataba umeibua maswali ambayo hayajapatiwa ufafanuzi wa kina ikiwemo thamani na muda wa uendeshaji pamoja na sababu za Tanzania kuingia mkataba na kampuni inayotajwa katika kesi za ukwepaji kodi na migogoro katika utekelezaji mikataba huku baadhi ya Nchi zikiikataa kampuni hiyo.

Je, unaufahamu kiasi gani Ushirikiano wa DP-World na Bandari?

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anawasilisha Pendekezo la Kuridhiwa kwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anawasilisha Pendekezo la Kuridhiwa kwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii katika Uendelezaji wa Maeneo ya Bandari Nchini, leo Juni 10, 2023

UTOAJI HUDUMA HAUJAFIKIA VIWANGO VINAVYOTAKIWA KIMATAIFA
Prof. Mbarawa amesema: "Pamoja na kuchukua hatua mbalimbali za maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam, bado ufanisi katika utoaji Huduma za haujafikia viwango vinavyotakiwa kimataifa.”

“Hali ya sasa ya utendaji imeendelea kuwa ya kiwango cha chini ikilinganishwa na Bandari shindani kikanda. Kwa mfano, wastani wa meli kusubiri nangani kwa Bandari ya Dar es salaam ni Siku 5 ikilinganishwa na Siku 1.25 kwa Bandari ya Mombasa na siku 1.6 kwa Bandari ya Durban.”

"Ufanisi mdogo wa Bandari ya Dar umetokana na changamoto ikiwemo kukosekana kwa Mifumo ya kisasa ya TEHAMA, maeneo ya kutosha ndani na nje ya Bandari kwa ajili ya kuhifadhia shehena, Maegesho ya Meli, mitambo ya kutosha na ya kisasa ya kuhudumia shehena ambayo ina gharama kubwa ya Uwekezaji.”

“Meli kutumia muda mrefu kupakia na kupakua shehena gatini kwa wastani wa Siku 5 ikilinganishwa na Siku 1 inayokubalika Kimataifa, pamoja na Meli kubwa kutokuja katika Bandari ya Dar kutokana na kuchukua muda mrefu kuhudumiwa

MSINGI WA MKATABA HUU KUENDANA NA MIKATABA
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema Mkataba wa DP World kuendesha Bandari utakuwa hai mpaka pale ambapo shughuli za Miradi zitasitishwa au kuisha kwa muda wa Mikataba ya Nchi mwenyeji na Mikataba ya miradi

Amesema "Msingi wa Mkataba huu kuendana na Mikataba ya miradi ni kutokana na kwamba unaweka msingi unaowezesha kuingia na kutekelezwa kwa Mikataba 10 Nchini."

KAMPUNI YA DP WORLD INA UZOEFU WA KUENDESHA BANDARI BARANI AFRIKA
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi amesema Kampuni ya DP World ina uzoefu katika uendeshaji wa shughuli za Bandari Barani Afrika, Asia, Ulaya na Amerika ya Kaskazini na Kusini

Amesema "Baadhi ya Kampuni zilizowasilisha nia ya kuwekeza Bandarini hazina wakati Kampuni ya DP World inaendesha takriban Bandari 6 Afrika na Bandari zaidi ya 30 Duniani kote kwa ufanisi mkubwa.”

DP WORLD INATAKIWA KUENDELEZA AJIRA ZA WATUMISHI WALIOPO
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema “Uwepo wa ajira za Watanzania hususani Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam ni kipaumbele kikubwa cha Serikali sio tu katika Azimio hili bali katika kila aina ya uwekezaji ambao Nchi itaufanya.”

Amesema “Ibara ya 13 ya Mkataba huu inaitaka DP World kuendeleza ajira za Watumishi wote waliopo, kuwaajiri Watanzania pamoja kuwaendeleza kitaaluma.”

TAUHIDA: KIONGOZI ANAYETAMKA KAULI ZA UBAGUZI TUNAMSHANGAA SANA

Mbunge Tauhida Gallos Nyimbo amesema “Nikimuona kiongozi anayewaongoza watu anatamka kauli ya kibaguzi tunamshangaa sana, mimi natokea Songea, mama yangu ni Mzaramu lakini ni Mbunge wa #Zanzibar.”

Ameongeza “Serikali haikatai kukosolewa, ikikosolewa inafanya uboreshaji zaidi.”

MDEE: MKATABA WA DP WORLD UMETAJA VITU KIJUMLAJUMLA
Akizungumzia mkataba wa #Tanzania na Kampuni ya #DPWorld, Mbunge #HalimaMdee amesema “Tuna nafasi ya kubadilisha baadhi ya vitu katika Mkataba huu lakini najua hatutabadilisha

Ameongeza “Kama Mkataba huu unagusa Mtwara, Tanga, Mwanza, Dar es Salaam na Kigoma kwani usizungumzwe kwa mapana yake? Tukiupitisha unaenda kuwa mkataba wa Kimataifa, chochote ambacho kimetajwa kijumlajumla kuhusu Bandari kitahusika.”

BOFYA HAPA KUSOMA: Maoni ya Kamati ya Pamoja Kuhusu Azimio la Bunge Kuridhia Makubaliano Kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali Ya Dubai Kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii Kwa Ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji Wa Utendaji Kazi wa Bandari Tanzania la Mwaka 2023

Mimi (Involved) ni mgeni sana kwenye haya mambo ya mikataba ya kimataifa! Ila swali langu ni moja tuu, baada ya Bunge letu kupitisha muswaada huu kwa maelezo mazuri.

Je kwa upande wa mwekezaji nao bunge la huko (baraza la mapinduzi ya Dubai) nao walikaa kujadili hoja ya kuja kuwekeza Tanzania!

Naomba mwenye majibu ya Kitaalamu atujulishe kwa hilo !!!!!
 
Wao wanajiita wazanzibar
Wana serikali yao
Wana nchi yao
Wana kila kitu chao
Wana vitambulisho vyao
Wanajitambulisha kama wazanzibar kokote duniani
Ni wakati kula RASILIMALI ZA TANGANYIKA PEKEE NDIO WANAJIITA WATANZANIA WAKISHIBA wanaendelea kujitambulisha kama Wazanzibar
 
Huu mkataba Magufuli kamwe asingeweza kukubali, hata hawa Waarabu wasingesogeza pua zao. kwa hili bunge Magufuli alikosea sana Taifa bunge la kijinga sana hili. Mama aliwekwa kwenye mnara pale Dubai kumbe wana lao. Huu muungano wa kijinga mno, Nyerere achomeke sawa sawa huko.

IMG_6767.jpg

Eti serikali haijalipia
si bora tu ingelipia cash kuliko hili waloenda kulifanya?
unafurahia ofa bila kujua inreturn watahitaji nini
IMG_6765.jpg

Kusaini mikataba 37 ndani ya siku 1
then tunahjisifu hapa
 
Azimio la Bunge kuhusu Pendekezo la Kuridhiwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii katika Uendelezaji wa Maeneo ya Bandari Nchini leo Juni 10, 2023.

======

Leo Juni 10, 2023, Bunge la Tanzania linatarajia kujadili mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya DPWorld unaodaiwa kutotaja ukomo kuhusu Ushirikiano katika Uendeshaji, Uendelezaji na Uboreshaji wa Bandari zote za Baharini na Maziwa zilizopo Tanzania Bara

Mkataba umeibua maswali ambayo hayajapatiwa ufafanuzi wa kina ikiwemo thamani na muda wa uendeshaji pamoja na sababu za Tanzania kuingia mkataba na kampuni inayotajwa katika kesi za ukwepaji kodi na migogoro katika utekelezaji mikataba huku baadhi ya Nchi zikiikataa kampuni hiyo.

Je, unaufahamu kiasi gani Ushirikiano wa DP-World na Bandari?

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anawasilisha Pendekezo la Kuridhiwa kwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anawasilisha Pendekezo la Kuridhiwa kwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii katika Uendelezaji wa Maeneo ya Bandari Nchini, leo Juni 10, 2023

UTOAJI HUDUMA HAUJAFIKIA VIWANGO VINAVYOTAKIWA KIMATAIFA
Prof. Mbarawa amesema: "Pamoja na kuchukua hatua mbalimbali za maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam, bado ufanisi katika utoaji Huduma za haujafikia viwango vinavyotakiwa kimataifa.”

“Hali ya sasa ya utendaji imeendelea kuwa ya kiwango cha chini ikilinganishwa na Bandari shindani kikanda. Kwa mfano, wastani wa meli kusubiri nangani kwa Bandari ya Dar es salaam ni Siku 5 ikilinganishwa na Siku 1.25 kwa Bandari ya Mombasa na siku 1.6 kwa Bandari ya Durban.”

"Ufanisi mdogo wa Bandari ya Dar umetokana na changamoto ikiwemo kukosekana kwa Mifumo ya kisasa ya TEHAMA, maeneo ya kutosha ndani na nje ya Bandari kwa ajili ya kuhifadhia shehena, Maegesho ya Meli, mitambo ya kutosha na ya kisasa ya kuhudumia shehena ambayo ina gharama kubwa ya Uwekezaji.”

“Meli kutumia muda mrefu kupakia na kupakua shehena gatini kwa wastani wa Siku 5 ikilinganishwa na Siku 1 inayokubalika Kimataifa, pamoja na Meli kubwa kutokuja katika Bandari ya Dar kutokana na kuchukua muda mrefu kuhudumiwa

MSINGI WA MKATABA HUU KUENDANA NA MIKATABA
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema Mkataba wa DP World kuendesha Bandari utakuwa hai mpaka pale ambapo shughuli za Miradi zitasitishwa au kuisha kwa muda wa Mikataba ya Nchi mwenyeji na Mikataba ya miradi

Amesema "Msingi wa Mkataba huu kuendana na Mikataba ya miradi ni kutokana na kwamba unaweka msingi unaowezesha kuingia na kutekelezwa kwa Mikataba 10 Nchini."

KAMPUNI YA DP WORLD INA UZOEFU WA KUENDESHA BANDARI BARANI AFRIKA
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi amesema Kampuni ya DP World ina uzoefu katika uendeshaji wa shughuli za Bandari Barani Afrika, Asia, Ulaya na Amerika ya Kaskazini na Kusini

Amesema "Baadhi ya Kampuni zilizowasilisha nia ya kuwekeza Bandarini hazina wakati Kampuni ya DP World inaendesha takriban Bandari 6 Afrika na Bandari zaidi ya 30 Duniani kote kwa ufanisi mkubwa.”

DP WORLD INATAKIWA KUENDELEZA AJIRA ZA WATUMISHI WALIOPO
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema “Uwepo wa ajira za Watanzania hususani Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam ni kipaumbele kikubwa cha Serikali sio tu katika Azimio hili bali katika kila aina ya uwekezaji ambao Nchi itaufanya.”

Amesema “Ibara ya 13 ya Mkataba huu inaitaka DP World kuendeleza ajira za Watumishi wote waliopo, kuwaajiri Watanzania pamoja kuwaendeleza kitaaluma.”

TAUHIDA: KIONGOZI ANAYETAMKA KAULI ZA UBAGUZI TUNAMSHANGAA SANA

Mbunge Tauhida Gallos Nyimbo amesema “Nikimuona kiongozi anayewaongoza watu anatamka kauli ya kibaguzi tunamshangaa sana, mimi natokea Songea, mama yangu ni Mzaramu lakini ni Mbunge wa #Zanzibar.”

Ameongeza “Serikali haikatai kukosolewa, ikikosolewa inafanya uboreshaji zaidi.”

MDEE: MKATABA WA DP WORLD UMETAJA VITU KIJUMLAJUMLA
Akizungumzia mkataba wa #Tanzania na Kampuni ya #DPWorld, Mbunge #HalimaMdee amesema “Tuna nafasi ya kubadilisha baadhi ya vitu katika Mkataba huu lakini najua hatutabadilisha

Ameongeza “Kama Mkataba huu unagusa Mtwara, Tanga, Mwanza, Dar es Salaam na Kigoma kwani usizungumzwe kwa mapana yake? Tukiupitisha unaenda kuwa mkataba wa Kimataifa, chochote ambacho kimetajwa kijumlajumla kuhusu Bandari kitahusika.”

BOFYA HAPA KUSOMA: Maoni ya Kamati ya Pamoja Kuhusu Azimio la Bunge Kuridhia Makubaliano Kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali Ya Dubai Kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii Kwa Ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji Wa Utendaji Kazi wa Bandari Tanzania la Mwaka 2023

Mm ninaamini hapa sio bungeni ni mnadani.
 
Mimi (Involved) ni mgeni sana kwenye haya mambo ya mikataba ya kimataifa! Ila swali langu ni moja tuu, baada ya Bunge letu kupitisha muswaada huu kwa maelezo mazuri.

Je kwa upande wa mwekezaji nao bunge la huko (baraza la mapinduzi ya Dubai) nao walikaa kujadili hoja ya kuja kuwekeza Tanzania!

Naomba mwenye majibu ya Kitaalamu atujulishe kwa hilo !!!!!
Jibu hapana, sisi tulienda kuwaambia wane kuwekeza. Wao wametoa msharti yao, hayo masharti ili yasifungamane na Sheria za ndani ndio inabidi bunge kuridhia(ratification)
 
Nape ameshindwa kujibu hoja ya Mbowe kuwa kwanini bandari za Zanzibar kwanini hazijahusishwa? Nape alivyo mjinga eti wanapanga kumuadhibu Mbowe….mpuuzi huyu…

Nape ni mjinga kabisa kuwai kutokea eti anamtisha Mbowe hahaha
Nape ni mshamba tu wa lindi huko hana uwezo na hawez kumtisha freeman mbowe mtoto WA mjini born town wa kitambo. Nape ni mwendawazimu tu
 
Niwaulize ndugu zangu Watanganyika,Je kwani hakuna Zanzibar na wazanzibar ??

Je Zanzibar hawana nchi yao na serikali yao ??

Katiba yao ndio msingi wa kujibagua
Hakuna mtanganyika mbaguzi bali ni wazanzibar ndio wanajibagua kwa kila kitu kwa mujibu wa katiba yao wenyewe,Someni katiba ya Zanzibar.
 
Mimi (Involved) ni mgeni sana kwenye haya mambo ya mikataba ya kimataifa! Ila swali langu ni moja tuu, baada ya Bunge letu kupitisha muswaada huu kwa maelezo mazuri.

Je kwa upande wa mwekezaji nao bunge la huko (baraza la mapinduzi ya Dubai) nao walikaa kujadili hoja ya kuja kuwekeza Tanzania!

Naomba mwenye majibu ya Kitaalamu atujulishe kwa hilo !!!!!
Mkuu wao ni kufanya sherehe tu utaskia habibi come to Dubai, maana wanajua wabongo tumeingia cha kike wanakuja kuvuna tuu
 
Back
Top Bottom